TRENDING NOW

 


BIBLIA ISEMAVYO KUHUSU UTATU NA DR MWALUSAMBO

Utatu wa Mungu ni moja ya mafundisho yenye utata mkubwa sana katika Biblia, ingawa ni fundisho maarufu sana katika madhehebu mbalimbali. Neno „Utatu‟ halipatikani katika Biblia, bali ni neno lililoumbika kifikira tu (imagination). Kutokana na kukosekana kwa maandiko yanayozungumzia utatu wa Mungu moja kwa moja, fundisho hili limekuwa na maswali mengi sana yasiyo na majibu. Biblia inamwelezea Mungu kwa majina matatu, yaani Baba, Mwana au Yesu Kristo na Roho Mtakatifu; majina haya matatu yanajulikana kama „nafsi‟ tatu katika Mungu mmoja; na hiki ndicho chanzo cha utata wa somo hili.

Jambo kubwa la kuzingatia ni hili: Biblia nzima ina umoja wa ajabu sana usioweza kuvunjwa na mwanadamu; yeyote anayejaribu kufanya hivyo, kamwe hawezi kupata maana halisi ya makusudi ya Mungu katika kitabu hiki, yaani Biblia. Ili kuipata maana halisi iliyokusudiwa na Agano la kale, msomaji anapaswa kulinganisha na Agano jipya; kadhalika, ili kupata maana halisi iliyofichwa katika Agano jipya, msomaji anapaswa kulinganisha na Agano la kale. Hii ni kanuni muhimu sana kwa kila msomaji yeyote anayetaka kuielewa Biblia na umoja wake usioweza kutenganishwa kamwe.

Kuna mafundisho mbalimbali ndani ya makanisa ambayo yamerithiwa kutoka kwa waasisi wa madhehebu, yaliyojengwa bila kuzingatia kanuni ya umoja wa Biblia ambayo ina umoja wake unaokubaliana, na majibu yake yasiyopingana; iwe ni Agano la kale, au Agano jipya. Lakini sasa mambo yamekuwa tofauti kabisa! Kuna maswali mengi ambayo yanaonekana kuwa hayana majibu ingawa si kweli. Hii inatokana na kwamba kanuni za Biblia zinavunjwa, na kupata majibu yanayotokana na hisia za wanadamu tu, na wala si kutoka katika Biblia.

Swali la kwanza linalojitokeza kuhusiana na utatu wa Mungu ni hili: “Ikiwa kuna nafsi tatu katika Mungu mmoja, kwa nini isijulikane kuwa ni miungu watatu?”

Kwa Maswali au Ushauri Wasiliana nasi kwa:

+255 754 041 599, +255 766 635 382

Email: info@mwalusambo.or.tz


The Bible is the most wonderful book in the world. Why? It is because the name itself means books or God's library, with a total of sixty-six books. Again, the Bible has about forty authors, who were used by God to write the Bible at different times, between 1500 and 1600 years, guided by God himself, thus making the Bible have only one author, namely God.

Another amazing thing, God used writers from different fields, environments and times, including prophets, kings, farmers, breeders, fishermen, tax collectors, doctors, builders, etc. k; However, the Bible has a wonderful unity, without contradictions that arise from circumstances or times. This unity proves to us that the author of the Bible is one, who has existed in all times of the world's history, namely God.

"For prophecy was not brought anywhere by the will of man; but men spoke what came from God, led by the Holy Spirit(2 Pet. 2:21).

God is the Alpha and the Omega, that is, the beginning and the end,(Uf. 1:17); "He who is and who was and who will come(Uf.4:4), "I Am Who I Am"Exodus 3:14; Yoh. 8:58. This is the one who gave writers the words to write in all generations. Another amazing thing about this book is that it is the only book that has spread all over the world and is read by many people. It is also a book that separated people and divided them more than any other book in the world; but at the same time it is a book with answers to more questions of people in the world than any other book.

In order to understand the Bible well, it is necessary to use principles that will protect the unity of the Bible and bring meanings that do not contradict each other. All the important subjects in the world such as science or mathematics and others, are taught using special principles to maintain their accuracy; otherwise everyone would have different answers. Since we know that the Bible is a very important subject than all subjects in the world, it must be read and interpreted according to specific principles to protect its unity, and avoid the effects of losing the real meaning of God intended; while using our human mind. There are many conflicts when we enter into matters of faith, caused by teachings that do not follow the principles of reading and interpreting the Bible. God is faithful to give revelation through the Spirit about His Word(Yoh.6:63; 1Kor.2:13,16). But since revelation is a spiritual and secret matter between man and his God, no other outsider can know what is going on. This has been the reason for many people to claim that they have been revealed by God when it is their own thoughts. To avoid these effects, God has given us his rules that can help anyone, even those who do not know the revelations of the Spirit; because rules are rules, it doesn't matter if you're saved or not! As with any other matter that needs to be implemented using principles, whether you believe it or not, principles will do their job!

Let me use a few examples of addition and multiplication calculations with two digits: 25+25, if you add from left to right, the answer will be 410; but if you add from right to left, his answer will be 50. Both answers are correct if there is no mathematical rule to add. Neither of these two will have the courage to criticize the other for being wrong if there is no principle that assures him that he is right. But since the principle of this calculation is addition from right to left, then he will be sure that the correct answer is 50. The certainty of this answer is based on the principle of addition calculations!

Another example: When you want to ensure the accuracy of the multiplication calculation, it is necessary to divide the answer with one of the two digits used to multiply, for example, 6 x 8= 48; and if you divide 48 by 8, the answer will be 6; then you are sure that your answer is correct. Therefore, without having a rule to ensure the correctness of your answer, you cannot know whether you are correct or not. From these two examples, we see how important it is to read and interpret the Bible using its principles, in order to be sure of what we read and teach, not to teach error. "Every Word of God is guaranteed; he is the shield of the believers. Do not add a word to his words; lest he blame you, you will be seen as a liar"(Prov. 30:5,6).

Where will we find the principles to enable us to read and interpret the Bible? The answer to this question is simple because these principles are found in this wonderful book, the Bible. Therefore, it is not appropriate for someone to stand up and give the meaning of the holy scriptures using his thoughts and intellect; or by saying, "I think, maybe, of course" or using the positions of a religion, or a certain leader in a religion, or the belief of a sect by saying, "our religion says this" instead of using the position of the main author of the Bible who is God. "If you know this word first, that there is no prophecy in the scriptures to be interpreted according to someone's will" (2Pet.1:2).

Jesus helped us a lot to give us guidance to understand the Bible and its purposes when he said, "Do not think that I came to abolish the Torah or the prophets, I did not come to abolish, but to fulfill." Because, amen, I say to you, until heaven and earth pass away, not one jot or one dot of the Torah will pass away, until all is fulfilled"(Math.5:17,18).

"....These are my words that I told you when I was with you, that all that was written to me in the law of Moses, and in the prophets and the Psalms must be fulfilled. Then he opened their minds to understand the scriptures" (Luke 24:44,45).

"You examine the scriptures, because you think that you have eternal life in them; and that is what testifies to me. Because if you believed in Moses, you would believe in me; because he wrote about me. But if you don't believe his scriptures, where will you believe my words?" (John 5:39, 46, 47).

"....Warning them about Jesus, with the words of the law of Moses and the prophets, from morning until evening. Some believed what was said, others did not" (Acts 28:23, 24).

In all the scriptures above, we find the following truth:

 1. The Torah, the Psalms and the Prophets, were written for Jesus.

 2. Jesus came to fulfill all that was written to him in the Torah, Psalms and Prophets.

 3. All that is written will continue to be fulfilled until the heavens and the earth depart (the second coming of Jesus)

 4. His disciples did not know this secret until their minds were revealed by Jesus, after his resurrection.

Here we see that, the Old Testament has been like a map of a drawn house; The new testament builds God's plan by following the blueprint drawn by God himself in the old testament, like a master craftsman. A washi craftsman needs to know how to read the map well, in order to build the house as intended by the painter without losing the dimensions or shape of the house. Apostles, prophets, evangelists, pastors and teachers, they are all builders of God's church. "Because no other foundation can be laid, except the one that has already been laid, that is, Jesus Christ"(1Kor.3:11). We cannot build using the teachings that Jesus did not leave to us, being his church; and he is the fulfiller of the Torah, the Psalms and the Prophets; we will be like the washi craftsman who stops reading the map given to him and starts drawing his own map. It should also be noted that, even in our environment, there are many builders of ordinary houses, who are unable to read a drawn map, although they can build without using a map.

Jesus said,"The Torah and the prophets existed until John; from that time, the good news of the kingdom of God is proclaimed, and everyone enters with strength" (Luke 16:16).

He said again, "For all the Prophets and the Torah prophesied until the time of John"(Math. 11:13). In these two scriptures we see that all the Torah and all the Prophets, their message was aimed at reaching the time of John the Baptist, which was also the time of Jesus himself on earth; but after that time has passed, what remains is the time for the implementation of all that was written in the Old Testament. Jesus carried out what concerned him in his time; the rest was carried out by the apostles; after that, the church has continued to implement all that is left and about it, it will continue with that work until the time of Jesus' second coming, that is, the end of the world. John was the end of prophecy; no other prophecies were given after John the Baptist, except the Gospels of Jesus, the letters of the apostles and revelation, in which we find an explanation or read the map of the Old Testament, drawn to the end of the age, that is, the second coming of Jesus, or the end of the world. In other words, it is to say that no other map has been drawn or will be drawn after John the Baptist, but it is a construction that will continue. Moreover, it is to say that, even the book of John's revelation does not bring anything new, which was not spoken by the Torah, Psalms, Prophets, Jesus and apostles. “…..And on this rock I will build my church; and the gates of hell will not prevail against it" (Mat.16:18).

The Old Testament has three main parts which are Torah, Psalms and Prophets; Also, the New Testament has three main parts that explain the Old Testament, and they are the Gospel, the Epistles and the Revelation. These parts must agree in the sense of what we are looking for. Because of the unity of the Bible, it should not be separated into pieces, even losing its meaning. By making that mistake, we will cause one scripture to be interpreted in many different meanings, and build weak teachings in the church of Jesus Christ, and make it fail by being attacked by the gates of hell. Jesus had mercy on his church!

When the reader knows the secret of the unity of the Bible, and how it cannot differ from text to text; or author and writer; or centuries and centuries; because the main author is the same. Knowing this will help the reader not to misunderstand the Bible, or to find a meaning that will contradict other scriptures. If you take the cork of a bottle and put it in the bottle by mistake, you will fail to close even if you think it is not the cork. If you force it to close without knowing that you have made a mistake in setting it as required, eventually even when opening it may fail, and you will have to break it. The problem is not with the cork, the problem is with the installer who did not know how to make it sit as needed. Likewise, it is in the Word of God! Many readers think that the Bible is very difficult to understand; although there is truth in this matter, because it will be recognized in the way of the spirit; but the big problem is that a person reads the Bible with personal thoughts and religious traditions in mind, thus failing to connect it to find the correct meaning.

The Jews knew a lot about the scriptures and boasted about it; but when Jesus came, they failed to connect the words of the Torah with those of Jesus, making them two different things, and completely failing to understand who Jesus is. They claimed to know Jesus, but they rejected Jesus when he called himself God. Examples:Which. 8:3 alreadyMath.4:4; Isa.6:9,10 alreadyMath.13:14,15; Deuteronomy 18:15 and John 5:47; Psalm 82:6 and John 10:34; Joel 2:28,29 and Acts 2:16-21; Psalm 16:8-11 andActs 2:25-28; Psalm 110:1 alreadyLuke 20:41-44; Luke 24:44-46. These are some of the few scriptures that Jesus reminded the Jews that, what they were reading in the Torah, Psalms and Prophets, were about him and they could not separate him from those scriptures. Therefore, those who read the old testament without seeing Jesus, and those who saw and heard him, and we who are reading now, there is no difference. Paul in his epistle says, "Even so, from now on we do not know anyone according to the flesh. Although we have recognized Christ in the form of the body, but we do not recognize him like this anymore"(2Cor. 5:16).

The apostle John also says in his document, "That which was from the beginning, which we heard, which we saw with our eyes, which we looked at, and which our hands touched, concerning the Word of life; and that life was manifested, and we have seen, and we testify, and preach to you that eternal life, which was with the Father, was manifested to us. What we saw and heard, we preach to you; so that you too can cooperate with us; and our fellowship is with the Father, and with his Son Jesus Christ"(1Yoh.1:1-3).

The apostle Peter also says, "And you loved him, even though you did not see him; whom although you do not see now, you believe; and rejoiced greatly, with unspeakable, glorious joy.... They were revealed that it was not for themselves, but for you that they ministered in those things, which have now been preached to you by those who preached the Gospel to you by the Holy Spirit sent from heaven. Angels desire to look at those things."(1Pet.1:8,12).

The author of the book of Hebrews writes by saying, "God who spoke in the past to our fathers through the prophets in many places and in many ways, at the end of these days has spoken to us in a son, whom he made the heir of all things, and through him he made the world."(Ebr.1:1).

"And when all those people were witnessed because of their faith, they did not receive the promise; because God had already prepared something better for us, so that they would not be completed without us"(Ebr.11:39,40).

All these authors admit the same thing, that there is no difference between the people who heard the Torah of Moses, the psalms, the prophets and those who heard Jesus in person and saw him; and we who believed in him without seeing him in the flesh. We have all received the same word through faith in Christ Jesus. Our God cannot change in His words; he is the same, yesterday and today and forever. This is the unity of the Bible that is strong and cannot be shaken by any human being. The apostle Paul warned the Christians of Colossae about this combination of teachings that are introduced by the cunning of people by saying, "See that no one takes you captive with his empty knowledge and empty deceptions, according to the traditions of men, according to the previous teachings of the world, nor not in the manner of Christ"(Col. 2:8).

God has been revealing himself to his people in different ways according to season and time; but if he is the same. He revealed himself to the ancients as God the Father, Almighty, Jehovah, I am that I am, Creator of heaven and earth, God of Abraham, Isaac and Jacob, Eternal Father, and many others; but recently he has revealed himself as the Son, and all those names are also his, showing that he is the same God. He made the old covenant, nowadays he has made a new covenant, but God is the same. Therefore, these two covenants do not contradict each other, but each brings a good interpretation to the other. To understand the old covenant well, you need to understand the new covenant; Likewise, in order to understand the new covenant well, it is necessary to understand the old covenant well, since the author of these covenants is the same.

Our lesson will continue another time.

Don't forget to follow, comment, like and share with other loved ones.

Source: Mwalusambo International Ministry

I am your brother: Counselor Nicholaus Simon.

For help advice or questions

Whatsapp: +255 766 635 382

Email: pataufahamu@gmail.com/  info@mwalusambo.or.tz

 




Biblia ni kitabu cha ajabu kuliko vitabu vyote duniani. Kwa nini? Ni kwa sababu jina lenyewe lina maana ya vitabu au maktaba ya Mungu, yenye jumla ya vitabu sitini na sita. Tena, Biblia ina waandishi wapatao arobaini, waliotumiwa na Mungu kuiandika Biblia kwa vipindi tofauti, kati ya muda wa miaka 1500 na 1600, wakiongozwa na Mungu mwenyewe, hivyo kuifanya Biblia iwe na mwandishi mmoja tu, yaani Mungu.

Jambo lingine la ajabu, Mungu aliwatumia waandishi wa fani mbalimbali, mazingira na nyakati tofauti wakiwemo manabii, wafalme, wakulima, wafugaji, wavuvi, watoza ushuru, madaktari, wajenzi n. k; hata hivyo Biblia imekuwa na umoja wa ajabu, bila kuhitilafiana kunakotokana na mazingira wala nyakati. Umoja huu unatuthibitishia kuwa mwandishi wa Biblia ni mmoja, ambaye amekuwako nyakati zote za historia ya dunia, yaani Mungu.

“Maana unabii haukuletwa popote kwa mapenzi ya mwanadamu; bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu(2Pet. 2:21).

Mungu ndiye Alfa na Omega, yaani mwanzo na mwisho, (Uf. 1:17); “Aliyeko na aliyekuwako na atakayekuja (Uf.4:4), “Niko ambaye Niko” Kut.3:14; Yoh. 8:58. Huyu ndiye aliyewapa waandishi maneno ya kuandika katika vizazi vyote. Jambo lingine la ajabu kuhusu kitabu hiki ni kwamba, ni kitabu peke ambacho kimeenea duniani pote na kusomwa na watu wengi. Pia ni kitabu kilichowatenganisha watu na kuwafarakanisha kuliko kitabu kingine chochote duniani; lakini wakati uo huo ni kitabu chenye majibu ya maswali mengi ya wanadamu duniani kuliko kitabu kingine chochote.

Ili kuielewa Biblia vema, ni sharti kutumia kanuni ambazo zitalinda umoja wa Biblia na kuleta maana zisizohitilafiana na kupingana. Masomo muhimu yote duniani kama vile sayansi au hisabati na mengineyo, yanafundishwa kwa kutumia kanuni maalumu ili kutunza usahihi wake; vinginevyo kila mmoja angekuwa na majibu yake tofauti na mwingine. Kwa kuwa tunajua kuwa Biblia ni somo muhimu sana kuliko masomo yote duniani, sharti isomwe na kufasiriwa kwa kanuni maalumu ili kulinda umoja wake, na kuepuka athari za kupoteza maana halisi ya Mungu iliyokusudiwa; huku tukitumia akili zetu za kibinadamu. Kuna mitafaruku mingi sana tunapoingia katika masuala ya imani, inayosababishwa na mafundisho yasiyozingatia kanuni za kusoma na kufasiri maandiko ya Biblia. Mungu ni mwaminifu kutoa ufunuo kwa njia ya Roho kuhusu Neno lake (Yoh.6:63; 1Kor.2:13,16). Lakini kwa kuwa ufunuo ni suala la kiroho na siri kati ya mwanadamu na Mungu wake, hakuna mtu mwingine wa pembeni awezaye kujua kinachoendelea. Hii imekuwa sababu ya watu wengi kudai kwamba wamefunuliwa na Mungu wakati ni mawazo yao wenyewe. Ili kuepuka athari hizi, Mungu ametupa kanuni zake ambazo zinaweza kumsaidia mtu yeyote hata yule asiyejua mambo ya ufunuo wa Roho; kwa sababu kanuni ni kanuni, haijalishi umeokoka au la! Kama ilivyo kwa masuala mengine yoyote yanayohitaji kutekelezwa kwa kutumia kanuni, haijalishi kuwa unaamini au la, kanuni itafanya kazi yake!

Hebu nitumie mifano michache ya hesabu za kujumlisha na kuzidisha zenye tarakimu mbili: 25+25, ukijumlisha kuanzia kushoto kwenda kulia, jawabu lake litakuwa 410; lakini ukijumlisha kuanzia kulia kwenda kushoto, jawabu lake litakuwa 50. Majawabu yote mawili ni sahihi iwapo hakuna kanuni ya hisabati ya kujumlisha. Hakuna mmoja kati ya hawa wawili atakayekuwa na ujasiri wa kumkosoa mwenzake kuwa amekosea iwapo hakuna kanuni inayomhakikishia yeye kuwa yuko sahihi. Lakini kwa kuwa kanuni ya hesabu hii ni kujumlisha kutoka kulia kwenda kushoto, basi atakuwa na uhakika kuwa jawabu sahihi ni 50. Uhakika wa jibu hili unatokana na kanuni ya hesabu za kujumlisha!

Mfano mwingine: Unapotaka kuhakikisha usahihi wa hesabu ya kuzidisha, ni sharti kugawa jawabu na tarakimu mojawapo kati ya mbili zilizotumika kuzidisha, kwa mfano, 6 x 8= 48; na 48 ukigawa kwa 8, jawabu litakuwa 6; hapo unakuwa na uhakika wa jawabu lako kuwa ni sahihi. Kwa hiyo, bila kuwa na kanuni ya kuhakikisha usahihi wa jawabu lako, huwezi kujua kama uko sahihi au la. Kutokana na mifano hii miwili, tunaona jinsi ilivyo muhimu kusoma na kuifasiri Biblia kwa kutumia kanuni zake, ili kuwa na uhakika wa yale tunayoyasoma na kuyafundisha, tusifundishe upotofu. “Kila Neno la Mungu limehakikishwa; yeye ni ngao ya wamwaminio. Usiongeze neno katika maneno yake; asije akakulaumu, ukaonekana u mwongo” (Mith.30:5,6).

Je, tutazipata wapi kanuni za kutuwezesha kusoma na kufasiri Biblia? Jibu la swali hili ni rahisi kwa sababu, kanuni hizi zinapatikana katika kitabu hiki cha ajabu, yaani Biblia. Kwa hiyo, haifai mtu fulani kuinuka na kutoa maana ya maandiko matakatifu kwa kutumia mawazo na akili zake; au kwa kusema, “nadhani, huenda, bila shaka” au kutumia misimamo ya dini, au mkuu fulani katika dini, au imani ya madhehebu kwa kusema, “dini yetu inasema hivi” badala ya kutumia msimamo wa mwandishi mkuu wa Biblia ambaye ni Mungu. “Mkijua neno hili kwanza, ya kwamba hakuna unabii katika maandiko upatao kufasiriwa kama apendavyo mtu fulani tu” (2Pet.1:2).

Yesu alitusaidia sana kutupa mwongozo wa kuielewa Biblia na makusudi yake aliposema, “Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii la, sikuja kutangua, bali kutimiliza. Kwa maana, amin, nawaambia, mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka, yodi moja wala nukta moja ya torati haitaondoka, hata yote yatimie” (Math.5:17,18).

“…..Hayo ndiyo maneno yangu niliyowaambia nilipokuwa nikali pamoja nanyi, ya kwamba ni lazima yatimizwe yote niliyoandikiwa katika torati ya Musa, na katika manabii na Zaburi. Ndipo akawafunulia akili zao wapate kuelewa na maandiko” (Luka 24:44,45).

“Mwayachunguza maandiko, kwasababu mnadhani kwamba ninyi mna uzima wa milele ndani yake; na hayo ndiyo yanayonishuhudia. Kwasababu kama mngemwamini Musa, mngeniamini mimi; kwa sababu yeye aliandika habari zangu. Lakini msipoyaamini maandiko yake, mtayaamini wapi maneno yangu?” (Yoh.5:39, 46, 47).

“…..Akiwaonya mambo yake Yesu, kwa maneno ya sheria ya Musa na ya manabii, tangu asubuhi hata jioni. Wengine waliamini yale yaliyonenwa, wengine hawakuyaamini” (Mdo 28:23, 24).

Katika maandiko yote haya hapa juu, tunaupata ukweli ufuatao:

 1. Torati, Zaburi na Manabii, ziliandikwa kwa ajili ya Yesu.

 2. Yesu alikuja kuyatimiza yote aliyoandikiwa katika Torati, Zaburi na Manabii.

 3. Yote yaliyoandikwa yataendelea kutimizwa mpaka hapo mbingu na nchi zitakapoondoka (kuja kwa Yesu mara ya pili)

 4. Wanafunzi wake hawakuijua siri hii mpaka walipofunuliwa akili zao na Yesu, baada ya kufufuka kwake.

Hapa tunaona kuwa, Agano la kale limekuwa kama ramani ya nyumba iliyochorwa; Agano jipya linajenga mpango wa Mungu kwa kufuata ramani iliyochorwa na Mungu mwenyewe katika Agano la kale, kama fundi stadi. Fundi washi anahitaji kujua jinsi ya kuisoma ramani vema, ili kujenga nyumba kama ilivyokusudiwa na mchoraji bila kupoteza vipimo au sura ya nyumba. Mitume, manabii, wainjilisti, wachungaji na waalimu, hao wote ni wajenzi wa kanisa la Mungu. “Maana msingi mwingine hakuna mtu awezaye kuuweka, isipokuwa ni ule uliokwisha kuwekwa, yaani Yesu Kristo” (1Kor.3:11). Hatuwezi kujenga kwa kutumia mafundisho ambayo Yesu hakutuachia sisi, tukiwa ndio kanisa lake; naye ndiye mtimizaji wa Torati, Zaburi na Manabii; tutakuwa sawa na fundi washi anayeacha kuisoma ramani aliyopewa na kuanza kuchora ramani yake. Pia ikumbukwe kwamba, hata katika mazingira yetu, kuna wajenzi wengi wa nyumba za kawaida, wasio na uwezo wa kusoma ramani iliyochorwa, ingawa wanaweza kujenga bila kutumia ramani.

Yesu alisema, “Torati na manabii vilikuwepo mpaka Yohana; tangu wakati huo, habari njema ya ufalme wa Mungu hutangazwa, na kila mtu hujiingiza kwa nguvu” (Luka 16:16).

Alisema tena, “Kwa maana Manabii wote na Torati walitabiri mpaka wakati wa Yohana” (Math. 11:13). Katika maandiko haya mawili tunaona kuwa Torati yote na Manabii wote, ujumbe wao ulilenga kufikia wakati wa Yohana mbatizaji, ambao pia ulikuwa ni wakati wa Yesu mwenyewe duniani; lakini baada ya muda huo kupita, unaobaki ni muda wa utekelezaji wa yale yote yaliyoandikwa katka Agano la kale. Yesu alitekeleza yale yaliyomhusu kwa wakati wake; yaliyosalia yalitekelezwa na mitume; baada ya hapo, kanisa limeendelea kutekeleza yote yaliyobaki na kulihusu, litaendelea na kazi hiyo mpaka wakati wa kuja Yesu mara ya pili, yaani mwisho wa dunia. Yohana alikuwa ndio mwisho wa unabii; hakuna unabii mwingine uliotolewa baada ya Yohana mbatizaji, isipokuwa Injili za Yesu, nyaraka za mitume na ufunuo, ambamo ndani yake tunapata ufafanuzi au kuisoma ramani ya Agano la kale, iliyochorwa kuishia mwisho wa dahari, yaani kuja kwa Yesu mara ya pili, au mwisho wa dunia. Kwa maneno mengine ni kusema kwamba, hakuna ramani nyingine iliyochorwa au itakayochorwa baada ya Yohana mbatizaji, bali ni ujenzi utakaoendelea. Zaidi ya hayo ni kusema kuwa, hata kitabu cha ufunuo wa Yohana hakileti jambo lolote lililo jipya, ambalo halikunenwa na Torati, Zaburi, Manabii, Yesu na mitume. “…..Na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda” (Math.16:18).

Agano la kale lina sehemu kuu tatu ambazo ni Torati, Zaburi na Manabii; pia Agano jipya lina sehemu kuu tatu zinazofafanua Agano la kale, nazo ni Injili, Nyaraka na Ufunuo. Ni lazima sehemu hizi zikubaliane katika maana ya kile tunachokitafuta. Kwa sababu ya umoja wa Biblia ulivyo, haifai kuitenganisha vipande vipande, hata kupoteza maana yake. Kwa kufanya kosa hilo, tutasababisha andiko moja kufasiriwa kwa maana nyingi zilizo tofauti, na kujenga mafundisho dhaifu ndani ya kanisa la Yesu Kristo, na kulifanya lishindwe kwa kushambuliwa na milango ya kuzimu. Yesu alirehemu kanisa lake!

Msomaji anapoijua siri ya umoja wa Biblia, na jinsi ambavyo haiwezi kutofautiana kutoka andiko hata andiko; au mwandishi na mwandishi; au karne na karne; maana mwandishi mkuu ni mmoja yule yule. Kujua huku kutamsaidia msomaji kutokuielewa vibaya Biblia, au kupata maana ambayo itapingana na maandiko mengine. Ukichukua kizibo cha chupa halafu ukakosea kukikalisha katika chupa, utashindwa kufunga hata ukadhani sio kizibo chake. Kama utalazimisha kufunga bila kujua kwamba umekosea kukikalisha inavyotakiwa, hatimaye hata wakati wa kufungua unaweza kushindwa, na ukalazimika kukivunja. Tatizo si la kizibo, tatizo ni la mfungaji ambaye hakujua jinsi ya kukikalisha inanyotakiwa. Vivyo hivyo, ndivyo ilivyo katika Neno la Mungu! Wasomaji wengi wanadhani kuwa Biblia ni ngumu sana kuielewa; ingawa kuna ukweli katika jambo hili, kwa sababu yatambulikana kwa jinsi ya roho; lakini tatizo kubwa ni kwamba mtu anaisoma Biblia huku akiwa ametanguliza mawazo binafsi na mapokeo ya kidini, hivyo kushindwa kuiunganisha ili kuipata maana iliyo sahihi.

Wayahudi waliyajua sana maandiko ya torati na kujisifu katika jambo hilo; lakini Yesu alipokuja walishindwa kuyaunganisha maneno ya torati na ya Yesu, wakiyafanya kuwa ni vitu viwili tofauti, na kushindwa kabisa kumwelewa Yesu ni nani. Walidai kumjua Yesu, lakini walimkataa Yesu alipojiita kuwa ni Mungu. Mifano: Kumb.8:3 na Math.4:4; Isa.6:9,10 na Math.13:14,15; Kumb.18:15 na Yoh.5:47; Zab.82:6 na Yoh.10:34; Yoeli 2:28,29 na Mdo 2:16-21; Zab.16:8-11 na Mdo 2:25-28; Zab.110:1 na Luka 20;41-44; Luka 24:44-46. Haya ni baadhi ya maandiko machache ambayo Yesu aliwakumbusha Wayahudi kwamba, yale waliyokuwa wakiyasoma katika Torati, Zaburi na Manabii, yalimhusu yeye na wasingeweza kumtenganisha na maandiko hayo. Kwa hiyo, waliosoma agano la kale bila kumwona Yesu, na wale waliomwona na kumsikia, na sisi tunaosoma sasa, hakuna tofauti yoyote. Paulo katika waraka wake anasema, “Hata imekuwa, sisi tangu sasa hatumjui mtu awaye yote kwa jinsi ya mwili. Ingawa sisi tumemtambua Kristo kwa jinsi ya mwili, lakini hatumtambui hivi tena” (2Kor.5:16).

Mtume Yohana naye katika waraka wake anasema, “Lile lililokuwako tangu mwanzo, tulilolisikia, tuliloliona kwa macho yetu, tulilolitazama, na mikono yetu ikalipapasa, kwa habari ya Neno la uzima; na uzima huo ulidhihirika, nasi tumeona, tena twashuhudia, na kuwahubiri ninyi ule uzima wa milele, uliokuwa kwa Baba, ukadhihirika kwetu. Hilo tuliloliona na kulisikia, twawahubiri na ninyi; ili nanyi pia mpate kushirikiana nasi; na ushirika wetu ni pamoja na Baba , na pamoja na Mwana wake Yesu Kristo” (1Yoh.1:1-3).

Mtume Petro naye anasema, “Naye mwampenda, ijapokuwa hamkumwona; ambaye ijapokuwa hamwoni sasa, mnamwamini; na kufurahi sana, kwa furaha isiyoneneka, yenye utukufu….Wakafunuliwa ya kuwa si kwa ajili yao wenyewe, bali kwa ajili yenu walihudumu katika mambo hayo, ambayo sasa yamehubiriwa kwenu na wale waliowahubiri ninyi Injili kwa Roho Mtakatifu aliyetumwa kutoka mbinguni. Mambo hayo malaika wanatamani kuyachungulia.” (1Pet.1:8,12).

Mwandishi wa kitabu cha Waebrania anaandika kwa kusema, “Mungu ambaye alisema zamani na baba zetu katika manabii kwa sehemu nyingi na kwa njia nyingi, mwisho wa siku hizi amesema na sisi katika mwana , aliyemweka kuwa mrithi wa yote, tena kwa yeye aliufanya ulimwengu” (Ebr.1:1).

“Na watu hao wote wakiisha kushuhudiwa kwa sababu ya imani yao, hawakuipokea ahadi; kwa kuwa Mungu alikuwa ametangulia kutuwekea sisi kitu kilicho bora, ili wao wasikamilishwe pasipo sisi” (Ebr.11:39,40).

Waandishi hawa wote wanakiri jambo moja lile lile kwamba, hakuna tofauti kati ya watu walioisikia torati ya Musa, zaburi, manabii na wale waliomsikia Yesu ana kwa ana na kumwona; pia na sisi tuliomwamini bila kumwona kwa jinsi ya mwili. Sisi sote tumelipokea neno lile lile lililo sawa kwa njia ya imani iliyo katika Kristo Yesu. Mungu wetu hawezi kubadilika-badilika katika maneno yake; ni yeye yule, jana na leo na hata milele. Huu ndio umoja wa Biblia ulio imara na hauwezi kuyumbishwa na mwanadamu yeyote. Mtume Paulo aliwaonya wakristo wa Kolosai kuhusu mchanganyo huu wa mafundisho yanayoingizwa kwa ujanja wa watu kwa kusema, “Angalieni mtu asiwafanye mateka kwa elimu yake ya bure na madanganyo matupu, kwa jinsi ya mapokeo ya wanadamu, kwa jinsi ya mafundisho ya awali ya ulimwengu, wala si kwa jinsi ya Kristo” (Kol.2:8).

Mungu amekuwa akijifunua kwa watu wake kwa njia tofauti-tofauti kulingana na majira na wakati; lakini akiwa ni yeye yule. Alijidhihirisha kwa watu wa kale kama Mungu Baba, Mwenyezi, Yehova, Niko ambaye niko, Muumba wa mbingu na nchi, Mungu wa Ibrahimu, Isaka na Yakobo, Baba wa milele, na mengine mengi; lakini zamani hizi amejidhihirisha kama Mwana, na majina hayo yote pia ni yake, kuonyesha kwamba ni Mungu yeye yule. Alifanya agano la kale, zamani hizi amefanya agano jipya, lakini Mungu ni yeye yule. Kwa hiyo maagano haya mawili hayapingani, bali kila moja linaleta tafsiri nzuri kwa lingine. Ili kulielewa vema agano la kale, unahitaji kulielewa agano jipya; kadhalika, ili kulielewa vema agano jipya, unahitajika kulielewa vema agano la kale, kwa kuwa mwandishi wa maagano haya ni yule yule mmoja.

Somo letu litaendelea wakati mwingine……………………

Usisahahu kufollower, comment, like na kushare kwa wapendwa wengine.

Source: Mwalusambo International Ministry

Ni Mimi ndugu yako Counselor Nicholaus Simon.

Kiungo katika mwili wa kristo.

Kwa msaada ushauri au maswali

Whatsap: +255 766 635 382/+255 659 990 111

Email: pataufahamu@gmail.com/  info@mwalusambo.or.tz

  


 

Mafundisho ya udanganyifu na uzushi ndani ya makanisa yamezidi kuongezeka , ambayo huwaaminisha waumini  mambo ambayo si ya kweli.

Gharama Tsh. 15,000/ =

Kitabu hiki kinapatikana kwa mawakala wetu.

Mbeya: +255 754 041 599

Iringa: +255 766 635 382

Dar es Salaam: +255 658 499 078


 

Kitabu hiki Hujibu maswali yote kuhusu Utatu wa Mungu, Je, Biblia inafundisha Utatu? Je, Mungu ana nafsi tatu au anajidhihirisha mara tatu?

Gharama Tsh. 5,000/ =

Kitabu hiki kinapatikana kwa Mawakala wetu.

Mbeya: +255 754 041 599

Iringa: +255 766 635 382

Dar es Salaam: +255 658 499 078

 

 

 


Translate

About

Site Links

Follow on Facebook