Articles by "MAHUSIANO"
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo MAHUSIANO. Onyesha machapisho yote

@Ujana wenye matokeo

A. KIMWILI
Wimbo 2:7, 8:4.(NEN)
“Binti za Yerusalemu, ninawaagiza kwa paa na kwa ayala wa shambani: Msichochee wala kuamsha mapenzi hata yatakapotaka yenyewe.”
"Binti za Yerusalemu, ninawaagiza: msichochee wala kuamsha mapenzi hata yatakapotaka yenyewe."

MUHIMU: 
Katika ujana, changamoto kuu ni kuyaamsha/kuchochea mapenzi kabla ya wakati wake”

Fahamu mambo kadhaa yanayo sababisha hali hiyo:-
Jambo la kufahamu ni kwamba Mungu ameweka wakati maalumu kwa kila jambo.
Mhubiri 3:1“Kwa kila jambo kuna majira yake, Na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu.”

MAMBO YANAYOWEZA KUAMSHA/KUCHOCHEA MAPENZI KABLA YA WAKATI
1   1. Maongezi Mabaya. 
1Kor 15:33,“Msidanganyike; Mazungumzo mabaya huharibu tabia njema.”
 1Tim 4:7 “Bali hadithi za kizee, zisizokuwa za dini, uzikatae; nawe ujizoeze kupata utauwa.”
2Tim 2:16a,23 “Jiepushe na maneno yasiyo na maana, ambayo si ya dini; kwa kuwa wataendelea zaidi katika maovu,Walakini uyakatae maswali ya upumbavu yasiyo na elimu, ukijua ya kuwa huzaa magomvi.”
Maneno yasiyofaa yana mchango mkubwa kumpeleka kijana sehemu isiyofaa, vijana leo;unaweza kukuta wanawajadili wanawake mfano mguu, sura za wadada/wakaka.

2. Nyimbo za kidunia/tamthilia za mapenzi. 
Mithali 4:23, “Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo; Maana ndiko zitokako chemchemi za uzima.”, “Be careful how you think;your life is shaped by your thoughts. (Today English Version)” 
Rumi 12:2,  “Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.”
“Do not conform to the pattern of this world, but be transformed by the renewing of your mind. Then you will be able to test and approve what God’s will is—his good, pleasing and perfect will. New International Version (NIV)”

Elewa kuwa nyimbo yoyote/mziki ina mambo makubwa 3
i.                 Ina nguvu na uwezo wa kuathiri nafsi,moyo/roho(vinaweza kujazwa furaha au huzuni)

ii.                  Ina uwezo wa kuathiri hisia zako na kukuumbia tabia Fulani/roho Fulani.

iii.                Ipo nguvu ya kuponya/kuharibu

3. Kuzoeana kupita kiasi/ukaribu
Hii ni hatari mfano, kijana wa kike na wakiume kutembeleana tena wakiwa wawili.
Efeso 5:15-16, “Basi angalieni sana jinsi mnavyoenenda; si kama watu wasio na hekima bali kama watu wenye hekima; mkiukomboa wakati kwa maana zamani hizi ni za uovu.”

     4. Mizaha kupita kiasi kati ya jinsia mbili tofauti.
        Zaburi 1:1c, “Heri mtu yule asiyekwenda Katika shauri la wasio haki; Wala hakusimama katika njia ya wakosaji; Wala hakuketi barazani pa wenye mizaha.”
Mizaha ni matendo ya masihara,kejeli,au ukosefu wa umakini katika kufanya au kusema jambo, mfano eti kijana wa kiume anataniana na binti eti wahi nyumbani Mama ukanipikie chakula basi.

      5. Picha za ngono. 
       Ayubu 31:1,“ Nilifanya agano na macho yangu; Basi nawezaje kumwangalia msichana?”
      2kor 7:1,“Basi, wapenzi wangu, kwa kuwa tuna ahadi hizo, na tujitakase nafsi zetu na uchafu wote wa mwili na roho, huku tukitimiza utakatifu katika kumcha Mungu.”
Hizi zimechangia hata hali ya kumpenda Mungu imeshuka, ufaulu mashuleni umeshuka na pia kupelekea Vijana kujiingiza kwenye maswala ya upigaji punyeto(musterbation), na kwa mabinti hali ya kujichua.
Hii hupelekea madhara makubwa katika ndoa.

   6. Marafiki wabaya. 
Mithali 13:20,“Enenda pamoja na wenye hekima, nawe utakuwa na hekima; Bali rafiki wa wapumbavu ataumia.”
Iko nguvu kubwa ya kuathiriana kati ya Rafiki na Rafiki. Hivyo ni muhimu kuwa mwangalifu na aina ya Rafiki uliye naye. Je,ana manufaa yoyote kwako?

       7. Mavazi ya kikahaba
      Mithali 7:10, Na tazama, mwanamke akamkuta, Ana mavazi ya kikahaba, mwerevu wa moyo;
Mavazi yanamchango mkubwa sana katika kuchochea mapenzi kwa vijana. Mfano kwa kijana wa kiume yapo maeneo hatari sana akiyaona kwa binti mfano: Mapaja ya binti, matiti, makalio n.k
Ieleweke kwamba kijana wa kiume hisia zake huongozwa kwa macho, na hivyo mara nyingi macho yake anapokutana na binti huanza kumwangalia sehemu ya kifuani(kisaikolojia)

      8. Kutokuwa na mipaka ya kupigiana simu 
       2Tim 2:16a,23 ”Jiepushe na maneno yasiyo na maana, ambayo si ya dini; kwa kuwa wataendelea zaidi katika maovu,Walakini uyakatae maswali ya upumbavu yasiyo na elimu, ukijua ya kuwa huzaa magomvi.”
Mfano: kijana wa kike na wakiume wanapigiana simu saa tano au saa sita, alafu kwa kuwa hawana cha maana cha kuzungumza, wanaanza kuulizana mfano:umelalaje muda huu? Chali au kifudifudi? Unasikia baridi? umevaa nini? Haya yote huchochea hali ya ndani sana ya hisia za mapenzi na kujikuta vijana wengi kufanya uasherati.
                         "Youth’s Pastor: Fred Mwabulambo (TAG ICC LUGALO) 0752 156 304"

    Ni mimi ndugu yako; Mwl Nicholaus Simon.
    Kiungo katika mwili wa kristo.
    Kwa msaada zaidi na ushauri. 
    Mawasiliano: +255 766 635 382
    pataufahamu@gmail.com

    Ubarikiwe sana Na nakuomba nisaidie kuishare kwa marafiki zako ili na wao wajifunze Neno la Mungu.

Somo letu litaendelea.....


Je unaona kama mke wako hakuheshimu? Anahitaji upendo toka kwako. Je mume wako haonyeshi  upendo? Anahitaji heshima toka kwako.
Jinsi wewe na mwenzi wako mnavyotendeana kulingana na kila mmoja anavyohitaji, ndivyo jitihada zenu zitakapoleta matunda na kila mmoja atazidi kutiwa moyo kuendelea kutenda  mazuri kwa mwenzake na kupeelekea kuboresha ndoa yenu. Sasa ili kufanikisha hili kila mmoja wenu lazima ajue kuozungumza lugha ya upendo na heshima kwa mwenzake.
Zitazame tofauti zenu kama mtaji na sio tatizo
Tofauti kati yako na mwenzi wako haimaanishi kuwa mmoja wenu hayuko sahihi. Muombe Mungu aweze kukusaidia kuzikubali tofauti kati yenu na kukuwezesha kuzitumia kusaidiana na kufaidiana. Kumbuka mbele za Mungu wote ni sawa na mna thamani sana.
Muone mwenzi wako kuwa ni mtu mwenye nia njema
Kama mwanadamu mwingine mwenzi wako pia anaweza akafanya mambo yanayoonekana kama ubinafsi. Ni muhimu kuwa na imani kuwa mwenzi wako ana nia njema juu yako hata katika nyakati anaposhindwa kuonyesha upendo na heshima juu yako. Kumbuka kuwa ndani ya moyo wake mwenzi wako anakupenda na hapendi kukuudhi. Muombe Mungu akuwezeshe kumuona mwenzi wako kama yeye anavyomuona.
Chunga maneno yako
Maneno unayoongea yanaonyesha yaliyomo ndani ya moyo wako. Hivyo muombe Mungu aujaze moyo wako upendo na heshima kila siku, na muombe Roho mtakatifu kuifanya upya akili yako ili mawazo yako yawe mema yatakayokupelekea kuongea maneno mema yenye upendo. Kuwa mwangalifu nay ale unayoyasema kwa mwenzi wako na jinsi unavyoyachukulia yale mwenzi wako anayoyasema. Epuka kutumia maneno ambayo yatamuudhi mwenzi wako. Sikiliza kabla ya kujibu na fikiri kwanza kabya ya kuongea. Hakikisha unaongea kwa sauti nzuri ya upole na upendo na pia lugha ya mwili iwe ya upendo na upole pia. Nia kuongea maneno yanayojenga, ya kweli, yenye msamaha, ya kushukuru, ya kiMungu na yenye kutia moyo.
Tambua lugha ya mawasiliano ya mwenzi wako
Wanawake na wanaume wanatofauti kubwa sana ya lugha ya mawasiliano kati yao. Itambue lugha ya mawasiliano ya mwenzi wako, usiwe na hisia tu bali hakikisha unaielewa vyema ili kuepuka migogoro inayotokana na kutokuelewana au tafsiri isiyo sahihi. Sikiliza kwa makini, uliza pale unapokuwa na wasiwasi na azimia kujifunza na kuifahamu lugha ya mawasiliano ya mwrnzi wako. Kumbuka kutokuelewana kwa lugha ya mawasiliano na jinsi ya kuwasiliana hakumaanishi ndoa yenu ni mbaya, bali kunaonyesha tofauti ya matarajio na namna ya kuwasiliana. Jaribuni kwa pamoja kwa msaada wa Mungu kukabiliana na hali hii kwa upendo na maelewano.
Samehe
Tegemea msaada wa Mungu katika kukuwezesha kumsamehe mwenzi wako pale anapokukosea, mara zote. Kumbuka kuwa Mungu amekusamehe makosa yako na hivyo onyesha msamaha kwa mwenzi wako. Pale unapopata msamaha kwa mwenzi wako baada ya kumkosea tambua kuwa kuna uwezekano wa kuhitaji muda wa kuponya jeraha la moyo wake, kuwa muelewa na onyesha kuwa kweli umekubali kosa lako na upo tayari kurekebisha.
Timiza mahitaji ya muhimu ya mwenzi wako
Hakikisha unatumia uwezo wako kuhakikisha unatimiza mahitaji muhimu ya mke wako ya kuwa karibu naye, kuwa muwazi, kumuelewa, kumthamini, kumtunza na kumjali. Anahitaji uwe karibu naye katika hali zote, kuwa muwazi kwake na kushirikiana naye katika mawazo na mipango yako, kumsikiliza bila kujaribu kumbadilisha, kusuluhisha matatizo kwa pamoja, kumheshimu na kila wakati kumhakikishia upendo wako kwake.
Hakikisha unatumia uwezo wako kuhakikisha unatimiza mahitaji muhimu ya mume wako ya uongozi, mahusiano na kimwili. Tambua hitaji lake la kuongoza na usijaribu kuudharau uongozi wake, sikiliza kwa makini mawazo yake na ushauri, thamini hitaji lake la kuwa karibu na wewe na kuwa rafiki yake katika hali zote, na uwe tayari kwa hitaji la kimwili bila vipingamizi.
Tambua kuwa Mungu pekee ndiye anayeweza kutimiza kila hitaji la mwanadamu. Hivyo mwenzi wako anaposhindwa kutimiza baadhi ya mahitaji yako usikasirike wala  kuumia sana. Badala yake mwendee Mungu.
Angalia nia yako
Usitumie vitendo au lugha ya upendo na heshima kama njia ya kumfanya mwenzi wako kufanya kile unaachokitaka. Muombe Mungu akuwezeshe kuwa na nia safi kila wakati ili uweze kufanya jambo jema kwa nia njema na kwa wakati unaofaa, kumfurahisha Mungu na pia mwenzi wako. Onyesha upendo ha heshima kwa mwenzi wako bila kutarajia chochote kama malipo.
Chagua lililo jema bila kuangalia mwenzi wako anasema nini
Hata kama mwenzi wako haonyeshi ushirikiano kwa jitihada zako za kuonyesha upendo na heshima wewe endelea kufanya hivyo kwa moyo wa kupenda. Mungu atazilipa jitihada zako kwa kukubariki. Tamabua kuwa kwa kumwonyesha mwenzi wako upendo na heshima unakuwa unamtumikia Mungu na kumheshimu, hivyo endelea kufanya yaliyo mema bila kujali mwenzi wako anafanya nini. Mungu anaona na atabariki juhudi na jitihada zako.