@Ujana wenye matokeo |
A.
KIMWILI
Wimbo
2:7, 8:4.(NEN)
“Binti za
Yerusalemu, ninawaagiza kwa paa na kwa ayala wa shambani: Msichochee wala
kuamsha mapenzi hata yatakapotaka yenyewe.”
"Binti za Yerusalemu, ninawaagiza: msichochee wala kuamsha
mapenzi hata yatakapotaka yenyewe."
MUHIMU:
Katika
ujana, changamoto kuu ni kuyaamsha/kuchochea mapenzi kabla ya wakati wake”
Fahamu
mambo kadhaa yanayo sababisha hali hiyo:-
Jambo
la kufahamu ni kwamba Mungu ameweka wakati maalumu kwa kila jambo.
Mhubiri
3:1“Kwa
kila jambo kuna majira yake, Na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu.”
MAMBO
YANAYOWEZA KUAMSHA/KUCHOCHEA MAPENZI KABLA YA WAKATI
1 1. Maongezi
Mabaya.
1Kor
15:33,“Msidanganyike;
Mazungumzo mabaya huharibu tabia njema.”
1Tim 4:7 “Bali
hadithi za kizee, zisizokuwa za dini, uzikatae; nawe ujizoeze kupata utauwa.”
2Tim
2:16a,23 “Jiepushe
na maneno yasiyo na maana, ambayo si ya dini; kwa kuwa wataendelea zaidi katika
maovu,Walakini uyakatae maswali ya upumbavu yasiyo na elimu, ukijua ya kuwa
huzaa magomvi.”
Maneno
yasiyofaa yana mchango mkubwa kumpeleka kijana sehemu isiyofaa, vijana
leo;unaweza kukuta wanawajadili wanawake mfano mguu, sura za wadada/wakaka.
2. Nyimbo
za kidunia/tamthilia za mapenzi.
Mithali 4:23, “Linda
moyo wako kuliko yote uyalindayo; Maana ndiko zitokako chemchemi za uzima.”, “Be careful how you think;your life is
shaped by your thoughts. (Today English Version)”
Rumi
12:2, “Wala
msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate
kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.”
“Do
not conform to the pattern of this world, but be transformed by the
renewing of your mind. Then you will be able to test and approve what
God’s will is—his good, pleasing and perfect will. New International
Version (NIV)”
Elewa
kuwa nyimbo yoyote/mziki ina mambo makubwa 3
i. Ina nguvu na uwezo wa kuathiri
nafsi,moyo/roho(vinaweza kujazwa furaha au huzuni)
ii.
Ina uwezo wa kuathiri hisia zako na
kukuumbia tabia Fulani/roho Fulani.
iii.
Ipo nguvu ya kuponya/kuharibu
3. Kuzoeana
kupita kiasi/ukaribu
Hii
ni hatari mfano, kijana wa kike na wakiume kutembeleana tena wakiwa wawili.
Efeso
5:15-16, “Basi angalieni
sana jinsi mnavyoenenda; si kama watu wasio na hekima bali kama watu wenye
hekima; mkiukomboa wakati kwa maana zamani hizi ni za uovu.”
4. Mizaha
kupita kiasi kati ya jinsia mbili tofauti.
Zaburi 1:1c, “Heri
mtu yule asiyekwenda Katika shauri la wasio haki; Wala hakusimama katika njia
ya wakosaji; Wala hakuketi barazani pa wenye mizaha.”
Mizaha
ni matendo ya masihara,kejeli,au ukosefu wa umakini katika kufanya au kusema
jambo, mfano eti kijana wa kiume anataniana na binti eti wahi nyumbani Mama
ukanipikie chakula basi.
5. Picha
za ngono.
Ayubu 31:1,“
Nilifanya agano na macho yangu; Basi nawezaje kumwangalia msichana?”
2kor 7:1, “Basi,
wapenzi wangu, kwa kuwa tuna ahadi hizo, na tujitakase nafsi zetu na uchafu
wote wa mwili na roho, huku tukitimiza utakatifu katika kumcha Mungu.”
Hizi
zimechangia hata hali ya kumpenda Mungu imeshuka, ufaulu mashuleni umeshuka na
pia kupelekea Vijana kujiingiza kwenye maswala ya upigaji
punyeto(musterbation), na kwa mabinti hali ya kujichua.
Hii
hupelekea madhara makubwa katika ndoa.
6. Marafiki
wabaya.
Mithali 13:20,“Enenda
pamoja na wenye hekima, nawe utakuwa na hekima; Bali rafiki wa wapumbavu
ataumia.”
Iko
nguvu kubwa ya kuathiriana kati ya Rafiki na Rafiki. Hivyo ni muhimu kuwa
mwangalifu na aina ya Rafiki uliye naye. Je,ana manufaa yoyote kwako?
7. Mavazi
ya kikahaba.
Mithali 7:10, Na tazama, mwanamke akamkuta, Ana mavazi ya kikahaba, mwerevu wa moyo;
Mavazi
yanamchango mkubwa sana katika kuchochea mapenzi kwa vijana. Mfano kwa kijana
wa kiume yapo maeneo hatari sana akiyaona kwa binti mfano: Mapaja ya binti,
matiti, makalio n.k
Ieleweke
kwamba kijana wa kiume hisia zake huongozwa kwa macho, na hivyo mara nyingi
macho yake anapokutana na binti huanza kumwangalia sehemu ya
kifuani(kisaikolojia)
8. Kutokuwa
na mipaka ya kupigiana simu
2Tim 2:16a,23 ”Jiepushe na maneno yasiyo na maana, ambayo si ya dini; kwa kuwa
wataendelea zaidi katika maovu,Walakini uyakatae maswali ya upumbavu yasiyo na
elimu, ukijua ya kuwa huzaa magomvi.”
Mfano:
kijana wa kike na wakiume wanapigiana simu saa tano au saa sita, alafu kwa kuwa
hawana cha maana cha kuzungumza, wanaanza kuulizana mfano:umelalaje muda huu?
Chali au kifudifudi? Unasikia baridi? umevaa nini? Haya yote huchochea hali ya
ndani sana ya hisia za mapenzi na kujikuta vijana wengi kufanya uasherati.
Ni
mimi ndugu yako; Mwl Nicholaus Simon.
Kiungo katika mwili wa kristo.
Kwa msaada zaidi na
ushauri.
Mawasiliano: +255 766 635 382
pataufahamu@gmail.com
Ubarikiwe sana Na nakuomba
nisaidie kuishare kwa marafiki zako ili na wao wajifunze Neno la Mungu.
Somo letu litaendelea.....
Post A Comment:
0 comments: