Karibu mpendwa mtu wa Mungu,
Ujifunze somo zuri kutoka kwa mwl Fred. S. Mwabulambo, andaa tu moyo wako ili
uweze kupokea kitu muda huu unapo soma.
Maandiko: 1 pet 1:14-16,
Lawi 11:44, Waeb 12: 14
Waebrania 12:4 (BHN) "Maana katika kupambana na dhambi, nyinyi hamjapigana
mpaka kiasi cha kumwaga damu yenu."
Mambo ya Walawi 11:44 "Kwa kuwa mimi ni Bwana, Mungu wenu; takaseni
nafsi zenu basi; iweni watakatifu, kwa kuwa mimi ni Mtakatifu; wala msitie
uchafu nafsi zenu kwa kitu kitambaacho cha aina yo yote, kiendacho juu ya nchi."
UTANGULIZI
A: Nini
maana ya neno “Utakatifu”
Ni
ile hali ya kuwa safi mbele za Mungu, kumhofu yeye na kumwogopa yeye na
kujitenga mbali na dhambi.
Neno “ Mtakatifu”
lina maana mbili katika moja; Yaani kutengwa na dhambi kabisa na pili kuwekwa
wakfu/ maalumu kwa ajili ya kazi/matumizi ya Bwana.
Hivyo: Utakatifu ni kutengwa na
kujitenga na dhambi.
· Tumeitiwa
utakatifu, na lazima tuwe watakatifu katika mwenendo wote (i)
Mbele ya watu (ii) sirini
B: Kipimo
kikuu cha utakatifu
(ii) Yale yanayotendeka sirini.
Rum
2:16, Luka 12: 2, Kumb 29:29
Rum 2:16 "katika siku ile Mungu atakapozihukumu siri za
wanadamu, sawasawa na injili yangu, kwa Kristo Yesu."
Luka 12:2 "Lakini hakuna neno lililositirika ambalo halitafunuliwa,
wala lililofichwa ambalo halitajulikana."
Kumbu 29:29 "Mambo ya siri ni ya Bwana, Mungu wetu; lakini
mambo yaliyofunuliwa ni yetu sisi na watoto wetu milele, ili tuyafanye maneno
yote ya sheria hii."
· Yanayotendeka
sirini ndiyo kipimo kikuu cha utakatifu
· Mungu
anajua wanadamu wanaweza kufanya mema machoni pa watu (Sirini
wameshindwa, wanapokuwa peke yao).
Math 6:1"Angalieni msifanye wema wenu machoni pa watu, kusudi
mtazamwe na wao; kwa maana mkifanya kama hayo, hampati thawabu kwa Baba yenu
aliye mbinguni."
· Hata
nyakati za kwanza katika kanisa la karne ya kwanza, watu walitenda mambo ya
aibu ndani ya kanisa kwa siri.
Efeso 5:12, Efeso 1:1 (Paulo
anaongea na watakatifu).
Efeso 1:1 "Paulo, mtume wa Kristo Yesu, kwa mapenzi ya Mungu; kwa
watakatifu walioko [Efeso] wanaomwamini Kristo Yesu."
Efeso 5:12 "kwa kuwa yanayotendeka kwao kwa siri, ni aibu
hata kuyanena."
· Mtu
anaweza kuongea na wewe na kwa tabasamu zuri usoni, lakini moyoni ni vita kali
Zaburi 55:21 "Kinywa chake ni laini kuliko siagi, Bali moyo
wake ni vita. Maneno yake ni mororo kuliko mafuta, Bali hayo ni panga
wazi."
· Mwanadamu
anafikiri Mungu ni kama mwanadamu mwenye ukomo katika kila jambo, Mungu anaona
mpaka mawazo ya moyoni mwetu.
(Luka 6:7-8,
Yoh 1:47-49)
Luka 6:7-8 "7 Na waandishi na Mafarisayo walikuwa
wakimvizia, ili waone kwamba ataponya siku ya sabato; kusudi wapate neno la
kumshitakia."
"8 Lakini yeye akayatambua mawazo yao, akamwambia yule mwenye mkono uliopooza, Ondoka, simama katikati; akaondoka akasimama."
"8 Lakini yeye akayatambua mawazo yao, akamwambia yule mwenye mkono uliopooza, Ondoka, simama katikati; akaondoka akasimama."
· Usimfiche
Bwana chochote kile, yeye anaona yote
Isaya 29: 15, katika vifaa vya kiteknolojia tunatumia Password kuficha
mambo yetu, Mungu hafichwi na password.
C: Jambo la
kufanya ni hili
· Uwe
mtu mwenye hofu kama Daudi
Zaburi
139: 7-12, Mithali 28: 14
Mithali
28:14 14 "Mwanadamu
mwenye kicho yu heri sikuzote; Bali mshupavu wa moyo ataangukia madhara."
· Usifanye
dhambi kwa kusudi Hesabu 15:30-31, Waeb 10:26
· Ungama
na kutubu mbele za Bwana kwa maana ya kuacha kabisa
(Kiri kosa/confess).
Mithali
28: 13, 2pet 3:9
2petro 3:9 "Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake, kama wengine
wanavyokudhani kukawia, bali huvumilia kwenu, maana hapendi mtu ye yote apotee,
bali wote wafikilie toba."
Mithali 28:13 "Afichaye dhambi zake hatafanikiwa; Bali yeye
aziungamaye na kuziacha atapata rehema."
D: kanuni ya
uchaguzi ( 7 selection principles of what to do and not to do)
Ili kujua kipi nifanye na kipi
nisifanye ziko kanuni saba (7) zinazomwongoza mtu wa Mungu kuishi maisha
matakatifu ya bila lawama katika ulimwengu huu wa uovu. Ni maswali 7 muhimu.
1. Kabla ya kufanya jambo lolote inapaswa mtu ajiulize; je kama Yesu angekuwepo
katika mwili pamoja nami akiniangalia; je ningefanya jambo hilo ninalotaka
kufanya au je? angekubaliana na kitu hicho? kama jibu ni ndiyo, basi fanya na
kama jibu siyo, basi usifanye kitu hicho, Yesu yupo anakuona katika kila
usemalo, tabia na mwenendo wako wote uko wazi mbele zake. Kumbuka wewe siyo wa
ulimwengu huu (Yoh 17:14-15)
Yohana
17:14-15 "14 Mimi nimewapa neno lako; na ulimwengu
umewachukia; kwa kuwa wao si wa ulimwengu, kama mimi nisivyo wa
ulimwengu." "15 Mimi siombi kwamba uwatoe katika ulimwengu;
bali uwalinde na yule mwovu."
2.
Kanuni ya pili ni je kitu hicho kinasaidia kukuza imani yako katika Mungu? kama
kitu hicho kinarudisha imani yako nyuma, hata kama kina Faida kiasi gani,
lazima ukiache. Mfano Daniel na wenzake 1:12-16,
walikataa chakula cha Mfalme, wakawa tayari kula mtama na maji tu.
3. Tatu ni je? kitu hicho kinawakwaza wengine? Je, kina mfanya mwingine
ashindwe kumuona Mungu katika maisha yake au kumrudisha nyuma aliyekwisha mjua
Yesu? (Rum 14:21).
Rum
14:21 "Ni vyema kutokula nyama wala kunywa divai wala kutenda
neno lo lote ambalo kwa hilo ndugu yako hukwazwa."
4. Nne ni je? kitu hicho kina haribu ushuhuda? (Luka 6:46). Kama kitu
hicho kwa kukifanya watu watashindwa kumwona Yesu katika maisha.
Luka 6:46 "Na kwa nini mnaniita, Bwana, Bwana, walakini
hamyatendi nisemayo?"
5. yao basi usifanye.Usifanye kitu chochote ambacho kitafanya watu watilie
mashaka wokovu wako.
6. Ya tano, ni je? Kitu hicho kina haribu afya
yako? au mwili wako?
(1 Kor 3:16-17, 6:19).
Biblia inasema wewe si mali yako mwenyewe (You are not of your own). Mwili wako
ni hekalu la Mungu, hivyo ukiliharibu, Mungu atakuharibu wewe. Mabadiliko
yoyote dhidi ya asili ya uumbaji wa Mungu hayakubaliki.Kumbuka Mungu alifurahia
kazi yake ya uumbaji (Mwanzo 1:31).
Mwanzo 1:31 "Mungu akaona kila kitu alichokifanya, na
tazama, ni chema sana. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya sita."
7. Kanuni ya sita, ni je? ni cha lazima? (Isaya 55:2)je, kitu
ninachotaka kufanya ni cha lazima? Kuna vitu vingine siyo lazima na havina
umuhimu na ukilazimisha kuvifanya vitaleta matatizo, utatenda dhambi; subiri
wakati wa Mungu. Mahitaji ya lazima ni chakula, malazi na mavazi ( 1
Tim 6: 7-8).
1Timotheo 6:7-8
"7 Kwa maana hatukuja na kitu duniani, tena hatuwezi kutoka na kitu;"
"8 ila tukiwa na chakula na nguo tutaridhika na vitu hivyo."
"7 Kwa maana hatukuja na kitu duniani, tena hatuwezi kutoka na kitu;"
"8 ila tukiwa na chakula na nguo tutaridhika na vitu hivyo."
8. Mwisho ni je? kitu hicho kitageuka kuwa Bwana wako? au
kitakufanya kuwa mtumwa? (Rumi 6: 16, Yak 1:15) jihadhari sana na vitu
ambavyo baadae vitakuwa Bwana na kukufanya kuwa mtumwa. Achana navyo vinginevyo
utaharibu ukristo wako.
Rumi
6:16 "Hamjui ya kuwa kwake yeye ambaye mnajitoa nafsi zenu
kuwa watumwa wake katika kumtii, mmekuwa watumwa wake yule mnayemtii, kwamba ni
utumishi wa dhambi uletao mauti, au kwamba ni utumishi wa utii uletao
haki."
Yakobo
1:15 "Halafu ile tamaa ikiisha kuchukua mimba huzaa dhambi, na
ile dhambi ikiisha kukomaa huzaa mauti."
Ni mimi ndugu yako; Mwl Nicholaus Simon.
Kiungo katika mwili wa kristo.
Kwa msaada zaidi na ushauri.
Mawasiliano: +255 766 635 382
pataufahamu@gmail.com
Ubarikiwe sana Na nakuomba nisaidie kuishare kwa marafiki zako ili na
wao wajifunze Neno la Mungu.
Somo zuri sana hasa kwa vijana
JibuFuta