Ngoja
nianze na story hii, kuna mtu mmoja alikuwa anauza vile vipulizo vya watoto.
Kila siku alikuwa akivijaza upepo na kuvirusha juu angani. Katika vipulizo
hivyo alivyokuwa anarusha angani vilikuwa vya rangi nyekundu, njano, blue na
kijani.
Kila
akirusha vipulizo hivyo angani, watoto wanakimbilia na kuvinunua.
Siku
moja akiwa anafanya hivyo, mtoto mmoja alikuja nyuma yake na kumuuliza:
“Ukirusha
kipulizo cheusi kitaruka angani kweli”
Yule
baba akajibu
“Mwanangu,
kinachosababisha vipulizo hivyo viruke angani si rangi yake bali kile kilicho
ndani yake”
Naomba
kuuliza, nini umetunza ndani yako?
Una
imani kiasi gani kuhusu uwezekano wa wewe kufanikiwa?
Kinachoamua
hatima ya maisha yako si mapito unayopitia kwa nje bali kile kilicho ndani
yako.
Ubarikiwe
sana Na nakuomba nisaidie kuishare kwa marafiki zako ili na wao wajifunze Neno
la Mungu.
Ni mimi ndugu yako; Mwl Nicholaus Simon.
Kiungo katika mwili wa kristo.
Kwa msaada zaidi na ushauri.
Mawasiliano: +255 766 635 382
pataufahamu@gmail.com
Post A Comment:
0 comments: