Articles by "MAHUBIRI"
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo MAHUBIRI. Onyesha machapisho yote


UMOJA WA BIBLIA NA DR.MWALUSAMBO - PART 1

Biblia ni kitabu cha ajabu kuliko vitabu vyote duniani. Kwa nini? Ni kwa sababu jina lenyewe lina maana ya vitabu au maktaba ya Mungu, yenye jumla ya vitabu sitini na sita. Tena, Biblia ina waandishi wapatao arobaini, waliotumiwa na Mungu kuiandika Biblia kwa vipindi tofauti, kati ya muda wa miaka 1500 na 1600, wakiongozwa na Mungu mwenyewe, hivyo kuifanya Biblia iwe na mwandishi mmoja tu, yaani Mungu.

Jambo lingine la ajabu, Mungu aliwatumia waandishi wa fani mbalimbali, mazingira na nyakati tofauti wakiwemo manabii, wafalme, wakulima, wafugaji, wavuvi, watoza ushuru, madaktari, wajenzi n. k; hata hivyo Biblia imekuwa na umoja wa ajabu, bila kuhitilafiana kunakotokana na mazingira wala nyakati. Umoja huu unatuthibitishia kuwa mwandishi wa Biblia ni mmoja , ambaye amekuwako nyakati zote za historia ya dunia, yaani Mungu. “Maana unabii haukuletwa popote kwa mapenzi ya mwanadamu; bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu (2Pet. 2:21). Mungu ndiye Alfa na Omega, yaani mwanzo na mwisho, (Uf. 1:17); “Aliyeko na aliyekuwako na atakayekuja (Uf.4:4), “Niko ambaye Niko” Kut.3:14; Yoh. 8:58. Huyu ndiye aliyewapa waandishi maneno ya kuandika katika vizazi vyote. Jambo lingine la ajabu kuhusu kitabu hiki ni kwamba, ni kitabu peke ambacho kimeenea duniani pote na kusomwa na watu wengi. Pia ni kitabu kilichowatenganisha watu na kuwafarakanisha kuliko kitabu kingine chochote duniani; lakini wakati uo huo ni kitabu chenye majibu ya maswali mengi ya wanadamu duniani kuliko kitabu kingine chochote.

Ili kuielewa Biblia vema, ni sharti kutumia kanuni ambazo zitalinda umoja wa Biblia na kuleta maana zisizohitilafiana na kupingana. Masomo muhimu yote duniani kama vile sayansi au hisabati na mengineyo, yanafundishwa kwa kutumia kanuni maalumu ili kutunza usahihi wake; vinginevyo kila mmoja angekuwa na majibu yake tofauti na mwingine. Kwa kuwa tunajua kuwa Biblia ni somo muhimu sana kuliko masomo yote duniani, sharti isomwe na kufasiriwa kwa kanuni maalumu ili kulinda umoja wake, na kuepuka athari za kupoteza maana halisi ya Mungu iliyokusudiwa; huku tukitumia akili zetu za kibinadamu . Kuna mitafaruku mingi sana tunapoingia katika masuala ya imani, inayosababishwa na mafundisho yasiyozingatia kanuni za kusoma na kufasiri maandiko ya Biblia. Mungu ni mwaminifu kutoa ufunuo kwa njia ya Roho kuhusu Neno lake (Yoh.6:63; 1Kor.2:13,16). Lakini kwa kuwa ufunuo ni suala la kiroho na siri kati ya mwanadamu na Mungu wake, hakuna mtu mwingine wa pembeni awezaye kujua kinachoendelea. Hii imekuwa sababu ya watu wengi kudai kwamba wamefunuliwa na Mungu wakati ni mawazo yao wenyewe. Ili kuepuka athari hizi, Mungu ametupa kanuni zake ambazo zinaweza kumsaidia mtu yeyote hata yule asiyejua mambo ya ufunuo wa Roho; kwa sababu kanuni ni kanuni, haijalishi umeokoka au la! Kama ilivyo kwa masuala mengine yoyote yanayohitaji kutekelezwa kwa kutumia kanuni, haijalishi kuwa unaamini au la, kanuni itafanya kazi yake!

Hebu nitumie mifano michache ya hesabu za kujumlisha na kuzidisha zenye tarakimu mbili: 25+25, ukijumlisha kuanzia kushoto kwenda kulia, jawabu lake litakuwa 410; lakini ukijumlisha kuanzia kulia kwenda kushoto, jawabu lake litakuwa 50. Majawabu yote mawili ni sahihi iwapo hakuna kanuni ya hisabati ya kujumlisha. Hakuna mmoja kati ya hawa wawili  atakayekuwa na ujasiri wa kumkosoa mwenzake kuwa amekosea iwapo hakuna kanuni inayomhakikishia yeye kuwa yuko sahihi. Lakini kwa kuwa kanuni ya hesabu hii ni kujumlisha kutoka kulia kwenda kushoto, basi atakuwa na uhakika kuwa jawabu sahihi ni 50. Uhakika wa jibu hili unatokana na kanuni ya hesabu za kujumlisha!   

Mfano mwingine: Unapotaka kuhakikisha usahihi wa hesabu ya kuzidisha, ni sharti kugawa jawabu na tarakimu mojawapo kati ya mbili zilizotumika kuzidisha, kwa mfano, 6 x 8= 48; na 48 ukigawa kwa 8, jawabu litakuwa 6; hapo unakuwa na uhakika wa jawabu lako kuwa ni sahihi. Kwa hiyo, bila kuwa na kanuni ya kuhakikisha usahihi wa jawabu lako, huwezi kujua kama uko sahihi au la. Kutokana na mifano hii miwili, tunaona jinsi ilivyo muhimu kusoma na kuifasiri Biblia kwa kutumia kanuni zake, ili kuwa na uhakika wa yale tunayoyasoma na kuyafundisha, tusifundishe upotofu. “Kila Neno la Mungu limehakikishwa; yeye ni ngao ya wamwaminio. Usiongeze neno katika maneno yake; asije akakulaumu, ukaonekana u mwongo” (Mith.30:5,6).

Je, tutazipata wapi kanuni za kutuwezesha kusoma na kufasiri Biblia? Jibu la swali hili ni rahisi kwa sababu, kanuni hizi zinapatikana katika kitabu hiki cha ajabu, yaani Biblia. Kwa hiyo, haifai mtu fulani kuinuka na kutoa maana ya maandiko matakatifu kwa kutumia mawazo na akili zake; au kwa kusema, “nadhani, huenda, bila shaka” au kutumia misimamo ya dini, au mkuu fulani katika dini, au imani ya madhehebu kwa kusema, “dini yetu inasema hivi” badala ya kutumia msimamo wa mwandishi mkuu wa Biblia ambaye ni Mungu. “Mkijua neno hili kwanza, ya kwamba hakuna unabii katika maandiko upatao kufasiriwa kama apendavyo mtu fulani tu” (2Pet.1:2).

Yesu alitusaidia sana kutupa mwongozo wa kuielewa Biblia na makusudi yake aliposema, “Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii la, sikuja kutangua, bali kutimiliza. Kwa maana, amin, nawaambia, mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka, yodi moja wala nukta moja ya torati haitaondoka, hata yote yatimie” (Math.5:17,18).

“…..Hayo ndiyo maneno yangu niliyowaambia nilipokuwa nikali pamoja nanyi, ya kwamba ni lazima yatimizwe yote niliyoandikiwa katika torati ya Musa, na katika manabii na Zaburi. Ndipo akawafunulia akili zao wapate kuelewa na maandiko” (Luka 24:44,45).

“Mwayachunguza maandiko, kwa sababu mnadhani kwamba ninyi mna uzima wa milele ndani yake; na hayo ndiyo yanayonishuhudia. Kwa sababu kama mngemwamini Musa, mngeniamini mimi; kwa sababu yeye aliandika habari zangu. Lakini msipoyaamini maandiko yake, mtayaamini wapi maneno yangu?” (Yoh.5:39,46,47).

“…..Akiwaonya mambo yake Yesu, kwa maneno ya sheria ya Musa na ya manabii, tangu asubuhi hata jioni. Wengine waliamini yale yaliyonenwa, wengine hawakuyaamini” (Mdo 28:23,24).

Katika maandiko yote haya hapa juu, tunaupata ukweli ufuatao:

1.     Torati, Zaburi na Manabii, ziliandikwa kwa ajili ya Yesu.

2.     Yesu alikuja kuyatimiza yote aliyoandikiwa katika Torati, Zaburi na Manabii.

3.     Yote yaliyoandikwa yataendelea kutimizwa mpaka hapo mbingu na nchi zitakapoondoka (kuja kwa Yesu mara ya pili)

4.     Wanafunzi wake hawakuijua siri hii mpaka walipofunuliwa akili zao na Yesu, baada ya kufufuka kwake.

Hapa tunaona kuwa, Agano la kale limekuwa kama ramani ya nyumba iliyochorwa; Agano jipya linajenga mpango wa Mungu kwa kufuata ramani iliyochorwa na Mungu  mwenyewe katika Agano la kale, kama fundi stadi. Fundi  washi anahitaji kujua jinsi ya kuisoma ramani vema, ili kujenga nyumba kama ilivyokusudiwa na mchoraji bila kupoteza vipimo au sura ya nyumba. Mitume, manabii, wainjilisti, wachungaji na waalimu, hao wote ni wajenzi wa kanisa la Mungu. “Maana msingi mwingine hakuna mtu awezaye kuuweka, isipokuwa ni ule uliokwisha kuwekwa, yaani Yesu Kristo” (1Kor.3:11). Hatuwezi kujenga kwa kutumia mafundisho ambayo Yesu hakutuachia sisi, tukiwa ndio kanisa lake; naye ndiye mtimizaji wa Torati, Zaburi na Manabii; tutakuwa sawa na fundi washi anayeacha kuisoma ramani aliyopewa na kuanza kuchora ramani yake. Pia ikumbukwe kwamba, hata katika mazingira yetu, kuna wajenzi wengi wa nyumba za kawaida, wasio na uwezo wa kusoma ramani iliyochorwa, ingawa wanaweza kujenga bila kutumia ramani.

Yesu alisema, “Torati na manabii vilikuwepo mpaka Yohana; tangu wakati huo, habari njema ya ufalme wa Mungu hutangazwa, na kila mtu hujiingiza kwa nguvu” (Luka 16:16).

Alisema tena, “Kwa maana Manabii wote na Torati walitabiri mpaka wakati wa Yohana” (Math. 11:13). Katika maandiko haya mawili tunaona kuwa Torati yote na Manabii wote, ujumbe wao ulilenga kufikia wakati wa Yohana mbatizaji, ambao pia ulikuwa ni wakati wa Yesu mwenyewe duniani; lakini baada ya muda huo kupita, unaobaki ni muda wa utekelezaji wa yale yote yaliyoandikwa katka Agano la kale. Yesu alitekeleza yale yaliyomhusu kwa wakati wake; yaliyosalia yalitekelezwa na mitume; baada ya hapo, kanisa limeendelea kutekeleza yote yaliyobaki na kulihusu, litaendelea na kazi hiyo mpaka wakati wa kuja Yesu mara ya pili, yaani mwisho wa dunia. Yohana alikuwa ndio mwisho wa unabii; hakuna unabii mwingine uliotolewa baada ya Yohana mbatizaji, isipokuwa Injili za Yesu, nyaraka za mitume na ufunuo, ambamo ndani yake tunapata ufafanuzi au kuisoma ramani ya Agano la kale, iliyochorwa kuishia mwisho wa dahari, yaani kuja kwa Yesu mara ya pili, au mwisho wa dunia. Kwa maneno mengine ni kusema kwamba, hakuna ramani nyingine iliyochorwa au itakayochorwa baada ya Yohana mbatizaji, bali ni ujenzi utakaoendelea. Zaidi ya hayo ni kusema kuwa, hata kitabu cha ufunuo wa Yohana hakileti jambo lolote lililo jipya, ambalo halikunenwa na Torati, Zaburi, Manabii, Yesu na mitume. “…..Na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda” (Math.16:18).

Agano la kale lina sehemu kuu tatu ambazo ni Torati, Zaburi na Manabii; pia Agano jipya lina sehemu kuu tatu zinazofafanua Agano la kale, nazo ni Injili, Nyaraka na Ufunuo. Ni lazima sehemu hizi zikubaliane katika maana ya kile tunachokitafuta. Kwa sababu ya umoja wa Biblia ulivyo, haifai kuitenganisha vipande vipande, hata kupoteza maana yake. Kwa kufanya kosa hilo, tutasababisha andiko moja kufasiriwa kwa maana nyingi zilizo tofauti, na kujenga mafundisho dhaifu ndani ya kanisa la Yesu Kristo, na kulifanya lishindwe kwa kushambuliwa na milango ya kuzimu. Yesu alirehemu kanisa lake!

Msomaji anapoijua siri ya umoja wa Biblia, na jinsi ambavyo haiwezi kutofautiana kutoka andiko hata andiko; au mwandishi na mwandishi; au karne na karne; maana mwandishi mkuu ni mmoja yule yule. Kujua huku kutamsaidia msomaji kutokuielewa vibaya Biblia, au kupata maana ambayo itapingana na maandiko mengine. Ukichukua kizibo cha chupa halafu ukakosea kukikalisha katika chupa, utashindwa kufunga hata ukadhani sio kizibo chake. Kama utalazimisha kufunga bila kujua kwamba umekosea kukikalisha inavyotakiwa, hatimaye hata wakati wa kufungua unaweza kushindwa, na ukalazimika kukivunja. Tatizo si la kizibo, tatizo ni la mfungaji ambaye hakujua jinsi ya kukikalisha inanyotakiwa. Vivyo hivyo, ndivyo ilivyo katika Neno la Mungu! Wasomaji wengi wanadhani kuwa Biblia ni ngumu sana kuielewa; ingawa kuna ukweli katika jambo hili, kwa sababu yatambulikana kwa jinsi ya roho; lakini tatizo kubwa ni kwamba mtu anaisoma Biblia huku akiwa ametanguliza mawazo binafsi na mapokeo ya kidini, hivyo kushindwa kuiunganisha ili kuipata maana iliyo sahihi.

Wayahudi waliyajua sana maandiko ya torati na kujisifu katika jambo hilo; lakini Yesu alipokuja walishindwa kuyaunganisha maneno ya torati na ya Yesu, wakiyafanya kuwa ni vitu viwili tofauti, na kushindwa kabisa kumwelewa Yesu ni nani. Walidai kumjua Yesu, lakini walimkataa Yesu alipojiita kuwa ni Mungu. Mifano: Kumb.8:3 na Math.4:4; Isa.6:9,10 na Math.13:14,15;  Kumb.18:15 na Yoh.5:47; Zab.82:6 na Yoh.10:34; Yoeli 2:28,29 na Mdo 2:16-21; Zab.16:8-11 na Mdo 2;25-28; Zab.110:1 na Luka 20;41-44; Luka 24:44-46. Haya ni baadhi ya maandiko machache ambayo Yesu aliwakumbusha Wayahudi kwamba, yale waliyokuwa wakiyasoma katika Torati, Zaburi na Manabii, yalimhusu yeye na wasingeweza kumtenganisha na maandiko hayo. Kwa hiyo, waliosoma agano la kale bila kumwona Yesu, na wale waliomwona na kumsikia, na sisi tunaosoma sasa, hakuna tofauti yoyote. Paulo katika waraka wake anasema, “Hata imekuwa, sisi tangu sasa hatumjui mtu awaye yote kwa jinsi ya mwili. Ingawa  sisi tumemtambua Kristo kwa jinsi ya mwili, lakini hatumtambui hivi tena” (2Kor.5:16).

Mtume Yohana naye katika waraka wake anasema, “Lile lililokuwako tangu mwanzo, tulilolisikia, tuliloliona kwa macho yetu, tulilolitazama, na mikono yetu ikalipapasa, kwa habari ya Neno la uzima; na uzima huo ulidhihirika, nasi tumeona, tena twashuhudia, na kuwahubiri ninyi ule uzima wa milele, uliokuwa kwa Baba, ukadhihirika kwetu. Hilo tuliloliona na kulisikia, twawahubiri na ninyi; ili nanyi pia mpate kushirikiana nasi; na ushirika wetu ni pamoja na Baba , na pamoja na Mwana wake Yesu Kristo” (1Yoh.1:1-3).

Mtume Petro naye anasema, “Naye mwampenda, ijapokuwa hamkumwona; ambaye ijapokuwa hamwoni sasa, mnamwamini; na kufurahi sana, kwa furaha isiyoneneka, yenye utukufu….Wakafunuliwa  ya kuwa si kwa ajili yao wenyewe, bali kwa ajili yenu walihudumu katika mambo hayo, ambayo sasa yamehubiriwa kwenu na wale waliowahubiri ninyi Injili kwa Roho Mtakatifu aliyetumwa kutoka mbinguni. Mambo hayo malaika wanatamani kuyachungulia.” (1Pet.1:8,12).

Mwandishi wa kitabu cha Waebrania anaandika kwa kusema, “Mungu ambaye alisema zamani na baba zetu katika manabii kwa sehemu nyingi na kwa njia nyingi, mwisho wa siku hizi amesema na sisi katika mwana , aliyemweka kuwa mrithi wa yote, tena kwa yeye aliufanya ulimwengu” (Ebr.1:1).

“Na watu hao wote wakiisha kushuhudiwa kwa sababu ya imani yao, hawakuipokea ahadi; kwa kuwa Mungu alikuwa ametangulia kutuwekea sisi kitu kilicho bora, ili wao wasikamilishwe pasipo sisi” (Ebr.11:39,40).

Waandishi hawa wote wanakiri jambo moja lile lile kwamba, hakuna tofauti kati ya watu walioisikia torati ya Musa, zaburi, manabii na wale waliomsikia Yesu ana kwa ana na kumwona; pia na sisi tuliomwamini bila kumwona kwa jinsi ya mwili. Sisi sote tumelipokea neno lile lile lililo sawa kwa njia ya imani iliyo katika Kristo Yesu. Mungu wetu hawezi kubadilika-badilika katika maneno yake; ni yeye yule, jana na leo na hata milele. Huu ndio umoja wa Biblia ulio imara na hauwezi kuyumbishwa na mwanadamu yeyote. Mtume Paulo aliwaonya wakristo wa Kolosai kuhusu mchanganyo huu wa mafundisho yanayoingizwa kwa ujanja wa watu kwa kusema, “Angalieni mtu asiwafanye mateka kwa elimu yake ya bure na madanganyo matupu, kwa jinsi ya mapokeo ya wanadamu, kwa jinsi ya mafundisho ya awali ya ulimwengu, wala si kwa jinsi ya Kristo” (Kol.2:8).

Mungu amekuwa akijifunua kwa watu wake kwa njia tofauti-tofauti kulingana na majira na wakati; lakini akiwa ni yeye yule. Alijidhihirisha kwa watu wa kale kama Mungu Baba, Mwenyezi, Yehova, Niko ambaye niko, Muumba wa mbingu na nchi, Mungu wa Ibrahimu, Isaka na Yakobo, Baba wa milele, na mengine mengi; lakini zamani hizi amejidhihirisha kama Mwana, na majina hayo yote pia ni yake, kuonyesha kwamba ni Mungu yeye yule. Alifanya agano la kale, zamani hizi amefanya agano jipya, lakini Mungu ni yeye yule. Kwa hiyo maagano haya mawili hayapingani, bali kila moja linaleta tafsiri nzuri kwa lingine. Ili kulielewa vema agano la kale, unahitaji kulielewa agano jipya; kadhalika, ili kulielewa vema agano jipya, unahitajika kulielewa vema agano la kale, kwa kuwa mwandishi wa maagano haya ni yule yule mmoja.

KWA MSAADA WA KIROHO AU KUPATA VITABU:

Mawasiliano: 0769 007 328

Email: mwalusambozephaniah@gmail.com / info@ mwalusambo.or.tz

Youtube: MwalusamboInternationalMinsitry / drmwalusambo

                                     
Mwalimu Christopher Mwakasege
Siku ya kwanza; Tar 10 Oktoba 2016, Uwanja wa Ollotu, Mbeya.


LENGO LA SOMO
NI KUIMARISHA UHUSIANO WAKO NA MUNGU KATIKA KRISTO YESU

Katika hali ya kawaida masomo haya si rahisi sana kuyapata. Na Mungu aliponiruhusu kuanza kufundisha si somo ambalo nililichangamkia sana kuanza kufundisha na sikuwa na uhakika sana juu ya upokeaji wa watu wa somo hili. 


Na tutaendelea vizuri kadri Mungu atakavyokuwa ananiambia. 



JAMBO LA KWANZA
Usidharau au usipuuzie ndoto uliyoota
Ni kwa sababu ndoto ni lango la Kiroho ambalo Mungu na Shetani wanalitumia kumfikia mwanadamu. Katika Ulimwengu wa roho kuna ukuta ambao Mungu aliuweka ambao ni mbingu na nchi, na baada ya dhambi kuingia ilitengeneza ukuta kati ya Mungu na mwanadamu. Ndipo Mungu alitengeneza njia za mawasiliano kwa njia ya malango na miongoni mwa malango mengine ni Ndoto. Ukisoma biblia utaona malango mengi sana. 



Muda ni lango Mungu yupo kwenye hali ya umilele na aliposema hapo Mwanzo  katika Mwanzo 1:1 ina maana aliukata umilele na alifungua lango la Muda. Yesu ni alfa na Omega yaani Mwanzo na mwisho. Japo yeye hana mwanzo na mwisho . Ili aweze kutusaidia kutembea katika muda, ukiweza kujua namna bora ya kutembea katika muda utakuwa umefaulu sana katika hali ya kimwili na Kiroho. 



Ndoto ni lango
Mfano
Mwanzo 41:1-7 Ikawa, mwisho wa miaka miwili mizima, Farao akaota ndoto; na tazama, amesimama kando ya mto. Na tazama, ng'ombe saba wazuri, wanono, walipanda kutoka mtoni, wakajilisha manyasini.
Na tazama, ng'ombe saba wengine wakapanda nyuma yao kutoka mtoni, wabaya, wamekonda, wakasimama karibu na wale ng'ombe wengine ukingoni mwa mto. Kisha hao ng'ombe wabaya waliokonda wakawala wale ng'ombe saba wazuri, wanono. Basi Farao akaamka. Akalala, akaota ndoto mara ya pili. Tazama, masuke saba yalimea katika bua moja, makubwa, mema. Na tazama, masuke saba membamba, yamekaushwa na upepo wa mashariki, yakatokeza baada yao. Kisha hayo masuke membamba saba yakayala yale masuke saba makubwa yaliyojaa. Basi Farao akaamka, kumbe! Ni ndoto tu.



Farao alipoamka akasema kumbe ni ndoto tu.  Ina maana alikuwa ameidharau lakini bado ilimletea mfadhaiko. Angalia mstari wa nane,  ndoto ya pili aliyoota ya masuke ndiyo iliyomletea mahangaiko sana na kumfanya atafute waganga na wachawi. Lakini hawakuweza kumsaidia, na nisawa na watu wengine ambao wakiota ndoto wanapambana kwenye ndoto na wakijakungundua kumbe ilikuwa ni ndoto wanaona afadhali na hawafuatilii na hata wakifutalia hawajui waombeje kwa sababu hata kujua maana yake inakuwa ni shida. 



Farao angeweza kupuuzia na gharama yake ingekuwa ni kubwa sana.  Na Yusufu ndiyo aliweza kutafsiri ndoto yake baada ya waganga na wachawi kushindwa.  Na kupuuzia ndoto ile kungefanya Dunia nzima kwenda vizuri sana kwa miaka 7 na baada ya hapo miaka 7 mingine wangepitia kipindi kigumu sana. Na watu wangejiuliza mbona Mungu hujasema na sisi kumbe aliwaambia. 



Mwanzo 41:53-57 Miaka ile saba ya shibe ikaisha katika nchi ya Misri, ikaanza kuja miaka ile saba ya njaa, kama vile Yusufu alivyosema. Kukawa na njaa katika nchi zote, bali katika nchi yote ya Misri palikuwa na chakula. Na nchi yote ya Misri ilipoona njaa, watu walimlilia Farao awape chakula. Farao akawaambia Wamisri wote, Enendeni kwa Yusufu; atakavyowaambia, fanyeni. Njaa ikawa katika dunia yote pia. Yusufu akazifungua ghala zote, akawauzia Wamisri. Njaa ikawa nzito katika nchi ya Misri. Watu wa nchi zote wakaja Misri kwa Yusufu; ili wanunue nafaka; kwa sababu njaa imekuwa nzito katika dunia yote 



Yusufu mume wake Mariam alipewa maelezo kwenye ndoto mara nne na alitii, fikiria angepuuzia ingekuaje...



Mfano wa pili

Ayubu 33:14-19 Kwa kuwa Mungu hunena mara moja, Naam, hata mara ya pili, ajapokuwa mtu hajali. 
Katika ndoto, katika maono ya usiku, Usingizi mzito uwajiliapo watu, Katika usingizi kitandani; Ndipo huyafunua masikio ya watu, Na kuyatia muhuri mafundisho yao, Ili amwondoe mtu katika makusudio yake, Na kumfichia mtu kiburi; Yeye huizuia nafsi yake isiende shimoni
Kazi ya ndoto ni kuyafunua masikio yako ya ndani ili waweze kuondoka kwenye makusudia yao yasiyo ya kimungu ndani yao. Na pia kuweza kuwaondoa kwenye mafundisho yasiyo sahihi.  


Mfano Kuna mtu mmoja alinisimulia, alipookoka si unajua kunakuwa na mto wa kutafuta chakula na alikuwa anasali hapa na pale, na alikuwa anasali kanisani kwake na akitoka pale alikuwa anaenda na mahali pengine na pengine. Hata katikati ya wiki utakuta anaenda kanisa hili na lile ilia pate mafundisho. Sasa alikutana na kanisa moja akaona limechangamka sana na aliazima kuhamia pale moja kwa moja. Usiku aliota ndoto kuwa Yule mchungaji yupo kwenye njia na watu wanamfuata, mara baada ya muda kidogo akawaona wameingia kwenye majani na mchungaji akiwa mbele , na yeye mwenyewe akawa anawafuata kwa nyuma sasa kabla nae hajaingia kwenye majani akaamka usingizini. Baada ya hapo alijua kuwa ni Mungu anamuambia kuwa asihamie lile kanisa. 



Ukiangalia tena Ayubu 33 : 17-19, Mungu anamuondoa mtu kwenye kiburi na kwenye mapenzi yako. Maana kuna watu wanakuwa na kiburi moyoni mwao na wanaanza kuona wao ndio wao na kuna baadhi ya mambo ya kumuuliza Mungu na mengine sio ya kumuuliza Mungu. Kwa sababu hiyo wanakuwa na vikundi vyao na vinakuwa vitovu vya nidhamu na wanakuwa na misimamo yao na kuona hiyo ndio bora sana na hata wanapoteza maana ya wokovu kwa sababu wanakuwa a kiburi sana. Mungu hutumia ndoto ili kuwatoa kwenye mapenzi yao na kuwarudisha kwenye njia nzuri.  Kwa hiyo Mungu anatumia ndoto kufikia nafsi ya mtu na mwili wa mtu. 



Kumbukumbu 13:1-4 Kukizuka katikati yako nabii, au mwotaji wa ndoto, akikutolea ishara au ajabu, ikatukia hiyo ishara au hiyo ajabu aliyokuambia akisema, Na tuifuate miungu mingine usiyoijua, tuitumikie hiyo; wewe usiyasikize maneno ya nabii yule, au yule mwotaji wa ndoto, kwa kuwa Bwana, Mungu wenu, yuawajaribu, apate kujua kwamba mwampenda Bwana, Mungu wenu, kwa mioyo yenu yote na roho zenu zote. Tembeeni kwa kumfuata Bwana, Mungu wenu; mcheni na kushika maagizo yake na kuisikia sauti yake, nanyi mtumikieni na kushikamana naye.



Hesabu 12:6 Kisha akawaambia , sikilizeni basi maneno yangu, akiwapo nabii kati yenu mimi Bwana nitajifunua kwake katika maono nitasema naye katika ndoto.



Aliyeumba lango la ndoto ni Mungu mwenyeshe na shetani anaiga maana yeye hajaumba kitu, bali anatumia malango yaliyoko.  Na malango haya yaliumbwa kwa ajili yetu na biblia inasema tunatakiwa tumiliki malango ya adui. Na sisi kazi yetu ni kuyajua hao malango na kudhibiti shetani asipite hapo. 



Mungu anaweza akasema na watumishi wake kwa ndoto, na pia ukitaka kujua ulichoota kwenye ndoto haijalishi kimetokea kiasi gani bali angali matokeo yake maana kama yanakupeleka karibu na Mungu ni sawa ila kama yanakutoa nje ya Mungu basi ujue si ya Mungu hata kama yanatokea kwa ishara kubwa sana na za kutisha, ila kama zinakutoa mbali na Mungu kaa mbali nazo.
Unakuta watu wanajipa vyeo na kuona kuwa ni Mungu kawapa hizo ndoto. Na wakiota ndoto zikitokea katika maisha yao wanasema mimi Bwana nikiota ndoto huwa zinatokea. Na hawaangali mwisho wao,kwa mfano Mungu kakuonesha jambo baya na wewe unaanza kusema kuna hili na litatokea lakini lengo la Mungu kukuonesha doto hiyo ni ili ujue na uweze kuomba ili kupangua hicho kinachotarajiwa kutokea ulichoota. 


Watu wengi huwa wanafuata miujiza na ona baada ya miujiza kuomba kwao kunapotea sana, na wanaanza kuwa wazito wa kusoma neno la Bwana. Na hata wakisoma hawaelezi. Muuujiza ni kwa ajili ya Mungu na sio wako ni kwa ajili ni kwa ajili ya Mungu.Wana wa Israel walikula Mana  jangwani na walipovuka kwenda kanani Mungu aliwaambia washike jembe walime. 



Mungu aliwaelekeza kwenye maji machungu ili ajifunue kama Yehova Rafa,muujiza umebeba ujumbe, muujiza una sauti ndani,na ndio maana Mungu alikuwa anarudia tena ili waweze kusikia tena. 



Ndio maana biblia inasema haijalishi ndoto unayoota ila cheki matokeo yake, au kama umepewa unabii au muujiza isikupe shida ukitokea ila cheki mwisho wake yaani matokeo yake. Ukiona inakupeleka mbali na Mungu wako ujue kuna shida Fulani. 



Shetani akija kama shetani inaweza ikawa ni rahisi sana kumjua ila sasa anachofanya anakuja kama malaika wa Nuru  lengo lake ni kukupotosha kwa hiyo kuwa makini sana usiamini kila kitu kama unafuata huo msimamo ulioupata ambao shetani kauleta unakuleta kwenye kiburi na ndio maana na Mungu nae anatumia ndoto ili kukuondoa kwenye hayo makusudi yako yaliyo nje ya mapenzi ya Mungu. 



Pia ukipuuzia ndoto ya shetani itakugharimu sana. Kuna watu hawatembei kwenye msimamo wa kanisa la Laiodokia unaosema kumbuka ulipoanguka ukatabu na usipofanya hivyo basi Yesu atakuja kukiondoa kile Kinara chako. Na ujue kuondolewa Kinara ni gharama kubwa sana. 



1 Jambo la Kwanza, Jambo unaloota linaweza kujitokeza kwenye nafsi, kwenye mwili wako na nafsi yako.



2 Likiwa na maelekezo na ukayafuata utaona matokeo yake katika maisha yako. Kama ilivyokuwa kwa Farao, Ayubu na katika Kumbukumbu la Torati. 



Baada ya kuona ndoto  na nimesoma  ndoto nyingi na wengi hawazilewi na shida kubwa sana niliyoiona ni namba ya kuziombea hizo ndoto.
Na mwingine kwa kutokuwajibika anajipachika cheo kuwa kila nikiota ndoto huwa zinatokea, ila hajui kuwa Mungu anataka upangue hiyo ndoto na badala yake wewe unaanza kutangaza. 


MIFANO YA NDOTO MBALI MBALI



1 Kuna mama mmoja mume wake aliota ndoto anakula bui bui na baada ya siku chache alipatwa na kikohozi ambacho alikuwa haponi na alitafuta kila dawa hakupona na alisikia kuwa tunafundisha semina hizi ndipo akaandika ndoto yake akiomba msaada. 



2 Mwingine aliota ndoto ya kugongwa na Nyoka, na katika ndoto aliona katika ndoto kuwa kidole chake kinatoa damu, na aliposhtuka usingizini aliona kweli kidole chake kitoa damu. Na Maisha yake yaliporomoka saa hiyo hiyo. 



3 Mwingine aliota ndoto anagombana  na mwenzie kwenye ndoto na huyo mwenzie alimng’ata mkono na alipoamka aliona alama kwenye mkono wake, 



4  Mwingine aliota ndoto kuwa kuna mtu kaja kwenye ndoto alipokuwa amelala na baada ya kupita muda kidogo alienda hospitali na alikutwa na uvimbe tumboni. 



5 Na mwingine aliota kang’atwa na nyoka kwenye mkono wake wenye pete ya ndoa. Na Baada ya hapo aliona anapata maumivu na akaamua kumuachia yule nyoka kwenye ndoto. Baada ya muda kidogo ndoa yake ilivurugika. Na tulipokuwa tunaomba alikuwa anatusikiliza kwenye redio tukiomba alitapika kitu cheupe . 



Wangapi hapa huwa wanaota ndoto wanakula kwenye ndoto? Na wengine hawajui maana yake ni nini. 1 Wakorintho 10:  15-22 Nasema kama na watu wenye akili; lifikirini ninyi ninenalo. Kikombe kile cha baraka tukibarikicho, je! Si ushirika wa damu ya Kristo? Mkate ule tuumegao, si ushirika wa mwili wa Kristo? Kwa kuwa mkate ni mmoja, sisi tulio wengi tu mwili mmoja;

kwa maana sisi sote twapokea sehemu ya ule mkate mmoja. Waangalieni hao Waisraeli walivyokuwa kwa jinsi ya mwili; wale wazilao dhabihu, je! Hawana shirika na madhabahu? Basi niseme nini? Ya kwamba kile kilichotolewa sadaka kwa sanamu ni kitu? Au ya kwamba sanamu ni kitu? Sivyo, lakini vitu vile wavitoavyo sadaka wavitoa kwa mashetani, wala si kwa Mungu; nami sipendi ninyi kushirikiana na mashetani. Hamwezi kunywea kikombe cha Bwana na kikombe cha mashetani. Hamwezi kushirikiana katika meza ya Bwana na katika meza ya mashetani. Au twamtia Bwana wivu? Je! Tuna nguvu zaidi ya yeye?
Lazima ucheki vizuri unakula nini 



1. Chakula kwenye ndoto inawezeka kabisa ni ushirika wa kimaagano, kati ya mwotaji wa ndoto na hao aliowaota kwenye ndoto na wanaunganishwa na ndoto hiyo na madhabahu iliyobeba ndoto hivyo na madhabahu iliyobeba agano husika. 



Damu ni uhai, hunapelekwa na kunywa kwenye ndoto wengi huwa wanashiriki hivi na kutokujua kuwa wanashiriki agano bila wao kujua. 



Na matokeo yake unaanza kuwa mzito kutoa sadaka, kwa sababu maeneo yote ambayo watu wanatoa sadaka kwa mizimu au miungu. Wanaanza kuwa wazito kutoa sadaka kwa Mungu wetu.  Ila sasa watu hao hao ukiwaita kwenye kikao cha harusi ona hela watakazo toa utashangaa sana. Hali ya kiroho ya mwotaji wa ndoto anaanza kuwa mzito kumtumia Mungu. 



Ndoto inakujulisha kwa kuna agano la kurithi. Ivi unajua kuwa Ibrahimu alifunga agano kwenye ndoto na Mungu fuatilia Kwenye Mwanzo 15:1-21 kwa hiyo agano linaweza fungwa kwenye ndoto. 


Unajua kwanini wana Israel  walipoabudu ndama walitoa sadaka ya Amani na miungu mingine, wanafanya hilo agano na wanashiriki na Ibada ya miungu mingine. Na vitu vya ndoto ni halisi kabisa. Na kwanza kutumika kwenye ndoto Petro , aliona katika maono kwa njia hiyo ndipo alianza kuhubiri injili kwa mataifa. 



MFANO

Sitasahau siku moja nilikuwa na Maswali, niliyokuwa namuuliza Mungu kuhusu baba yangu. Na Mungu alitumia ndoto kunijibu  na siku moja usiku niliota ndoto ya kuwa nimeenda hotelini, na baada ya muda kidogo nikamwona mhubiri mmoja wa marekani anakula chakula. Nikamwambia yule mhudumu niletee chauka pale alipokaa yule mhubiri na nilisogea pale alipo na nikavuta kiti nikakaa pale pale.  Na akainuka na nikamuona ni baba yangu. Alimaliza kula na sahani yake ikawa imesha chakula na akanipa vijiko alivyokuwa anavitumia kula chakula.  Na nikasikia sauiti ikaniambia nitakushibisha kwa wingi wa siku   na neno hili unalipata Zaburi 91:16 Kwa siku nyingi nitamshibisha, Nami nitamwonyesha wokovu wangu  na ndipo nilielewa kuwa baba yangu aliomba kwa Mungu kuwa aondoke kwa sababu alibakiza miaka mitatu tuliyokubaliana. 



NOTE Kitu cha muhimu kujua ni kuwa si kila mara ukitokewa na watu waliokufa kwenye ndoto ina maana ni shetani. Na angalia anakumabia nini, Yesu alipokuwa anaomba alitokewa na Musa na Elia wakati walikuwa wamekufa. 



Tutafanya zoezi hapa na kuombea watu wote waliokula chakula kwenye ndoto. 



Glory to God Glory to God.  Tumwamini Mungu. 

Be blessed.