Mwalimu Christopher Mwakasege
Siku ya kwanza; Tar 10 Oktoba 2016, Uwanja wa Ollotu, Mbeya.


LENGO LA SOMO
NI KUIMARISHA UHUSIANO WAKO NA MUNGU KATIKA KRISTO YESU

Katika hali ya kawaida masomo haya si rahisi sana kuyapata. Na Mungu aliponiruhusu kuanza kufundisha si somo ambalo nililichangamkia sana kuanza kufundisha na sikuwa na uhakika sana juu ya upokeaji wa watu wa somo hili. 


Na tutaendelea vizuri kadri Mungu atakavyokuwa ananiambia. 



JAMBO LA KWANZA
Usidharau au usipuuzie ndoto uliyoota
Ni kwa sababu ndoto ni lango la Kiroho ambalo Mungu na Shetani wanalitumia kumfikia mwanadamu. Katika Ulimwengu wa roho kuna ukuta ambao Mungu aliuweka ambao ni mbingu na nchi, na baada ya dhambi kuingia ilitengeneza ukuta kati ya Mungu na mwanadamu. Ndipo Mungu alitengeneza njia za mawasiliano kwa njia ya malango na miongoni mwa malango mengine ni Ndoto. Ukisoma biblia utaona malango mengi sana. 



Muda ni lango Mungu yupo kwenye hali ya umilele na aliposema hapo Mwanzo  katika Mwanzo 1:1 ina maana aliukata umilele na alifungua lango la Muda. Yesu ni alfa na Omega yaani Mwanzo na mwisho. Japo yeye hana mwanzo na mwisho . Ili aweze kutusaidia kutembea katika muda, ukiweza kujua namna bora ya kutembea katika muda utakuwa umefaulu sana katika hali ya kimwili na Kiroho. 



Ndoto ni lango
Mfano
Mwanzo 41:1-7 Ikawa, mwisho wa miaka miwili mizima, Farao akaota ndoto; na tazama, amesimama kando ya mto. Na tazama, ng'ombe saba wazuri, wanono, walipanda kutoka mtoni, wakajilisha manyasini.
Na tazama, ng'ombe saba wengine wakapanda nyuma yao kutoka mtoni, wabaya, wamekonda, wakasimama karibu na wale ng'ombe wengine ukingoni mwa mto. Kisha hao ng'ombe wabaya waliokonda wakawala wale ng'ombe saba wazuri, wanono. Basi Farao akaamka. Akalala, akaota ndoto mara ya pili. Tazama, masuke saba yalimea katika bua moja, makubwa, mema. Na tazama, masuke saba membamba, yamekaushwa na upepo wa mashariki, yakatokeza baada yao. Kisha hayo masuke membamba saba yakayala yale masuke saba makubwa yaliyojaa. Basi Farao akaamka, kumbe! Ni ndoto tu.



Farao alipoamka akasema kumbe ni ndoto tu.  Ina maana alikuwa ameidharau lakini bado ilimletea mfadhaiko. Angalia mstari wa nane,  ndoto ya pili aliyoota ya masuke ndiyo iliyomletea mahangaiko sana na kumfanya atafute waganga na wachawi. Lakini hawakuweza kumsaidia, na nisawa na watu wengine ambao wakiota ndoto wanapambana kwenye ndoto na wakijakungundua kumbe ilikuwa ni ndoto wanaona afadhali na hawafuatilii na hata wakifutalia hawajui waombeje kwa sababu hata kujua maana yake inakuwa ni shida. 



Farao angeweza kupuuzia na gharama yake ingekuwa ni kubwa sana.  Na Yusufu ndiyo aliweza kutafsiri ndoto yake baada ya waganga na wachawi kushindwa.  Na kupuuzia ndoto ile kungefanya Dunia nzima kwenda vizuri sana kwa miaka 7 na baada ya hapo miaka 7 mingine wangepitia kipindi kigumu sana. Na watu wangejiuliza mbona Mungu hujasema na sisi kumbe aliwaambia. 



Mwanzo 41:53-57 Miaka ile saba ya shibe ikaisha katika nchi ya Misri, ikaanza kuja miaka ile saba ya njaa, kama vile Yusufu alivyosema. Kukawa na njaa katika nchi zote, bali katika nchi yote ya Misri palikuwa na chakula. Na nchi yote ya Misri ilipoona njaa, watu walimlilia Farao awape chakula. Farao akawaambia Wamisri wote, Enendeni kwa Yusufu; atakavyowaambia, fanyeni. Njaa ikawa katika dunia yote pia. Yusufu akazifungua ghala zote, akawauzia Wamisri. Njaa ikawa nzito katika nchi ya Misri. Watu wa nchi zote wakaja Misri kwa Yusufu; ili wanunue nafaka; kwa sababu njaa imekuwa nzito katika dunia yote 



Yusufu mume wake Mariam alipewa maelezo kwenye ndoto mara nne na alitii, fikiria angepuuzia ingekuaje...



Mfano wa pili

Ayubu 33:14-19 Kwa kuwa Mungu hunena mara moja, Naam, hata mara ya pili, ajapokuwa mtu hajali. 
Katika ndoto, katika maono ya usiku, Usingizi mzito uwajiliapo watu, Katika usingizi kitandani; Ndipo huyafunua masikio ya watu, Na kuyatia muhuri mafundisho yao, Ili amwondoe mtu katika makusudio yake, Na kumfichia mtu kiburi; Yeye huizuia nafsi yake isiende shimoni
Kazi ya ndoto ni kuyafunua masikio yako ya ndani ili waweze kuondoka kwenye makusudia yao yasiyo ya kimungu ndani yao. Na pia kuweza kuwaondoa kwenye mafundisho yasiyo sahihi.  


Mfano Kuna mtu mmoja alinisimulia, alipookoka si unajua kunakuwa na mto wa kutafuta chakula na alikuwa anasali hapa na pale, na alikuwa anasali kanisani kwake na akitoka pale alikuwa anaenda na mahali pengine na pengine. Hata katikati ya wiki utakuta anaenda kanisa hili na lile ilia pate mafundisho. Sasa alikutana na kanisa moja akaona limechangamka sana na aliazima kuhamia pale moja kwa moja. Usiku aliota ndoto kuwa Yule mchungaji yupo kwenye njia na watu wanamfuata, mara baada ya muda kidogo akawaona wameingia kwenye majani na mchungaji akiwa mbele , na yeye mwenyewe akawa anawafuata kwa nyuma sasa kabla nae hajaingia kwenye majani akaamka usingizini. Baada ya hapo alijua kuwa ni Mungu anamuambia kuwa asihamie lile kanisa. 



Ukiangalia tena Ayubu 33 : 17-19, Mungu anamuondoa mtu kwenye kiburi na kwenye mapenzi yako. Maana kuna watu wanakuwa na kiburi moyoni mwao na wanaanza kuona wao ndio wao na kuna baadhi ya mambo ya kumuuliza Mungu na mengine sio ya kumuuliza Mungu. Kwa sababu hiyo wanakuwa na vikundi vyao na vinakuwa vitovu vya nidhamu na wanakuwa na misimamo yao na kuona hiyo ndio bora sana na hata wanapoteza maana ya wokovu kwa sababu wanakuwa a kiburi sana. Mungu hutumia ndoto ili kuwatoa kwenye mapenzi yao na kuwarudisha kwenye njia nzuri.  Kwa hiyo Mungu anatumia ndoto kufikia nafsi ya mtu na mwili wa mtu. 



Kumbukumbu 13:1-4 Kukizuka katikati yako nabii, au mwotaji wa ndoto, akikutolea ishara au ajabu, ikatukia hiyo ishara au hiyo ajabu aliyokuambia akisema, Na tuifuate miungu mingine usiyoijua, tuitumikie hiyo; wewe usiyasikize maneno ya nabii yule, au yule mwotaji wa ndoto, kwa kuwa Bwana, Mungu wenu, yuawajaribu, apate kujua kwamba mwampenda Bwana, Mungu wenu, kwa mioyo yenu yote na roho zenu zote. Tembeeni kwa kumfuata Bwana, Mungu wenu; mcheni na kushika maagizo yake na kuisikia sauti yake, nanyi mtumikieni na kushikamana naye.



Hesabu 12:6 Kisha akawaambia , sikilizeni basi maneno yangu, akiwapo nabii kati yenu mimi Bwana nitajifunua kwake katika maono nitasema naye katika ndoto.



Aliyeumba lango la ndoto ni Mungu mwenyeshe na shetani anaiga maana yeye hajaumba kitu, bali anatumia malango yaliyoko.  Na malango haya yaliumbwa kwa ajili yetu na biblia inasema tunatakiwa tumiliki malango ya adui. Na sisi kazi yetu ni kuyajua hao malango na kudhibiti shetani asipite hapo. 



Mungu anaweza akasema na watumishi wake kwa ndoto, na pia ukitaka kujua ulichoota kwenye ndoto haijalishi kimetokea kiasi gani bali angali matokeo yake maana kama yanakupeleka karibu na Mungu ni sawa ila kama yanakutoa nje ya Mungu basi ujue si ya Mungu hata kama yanatokea kwa ishara kubwa sana na za kutisha, ila kama zinakutoa mbali na Mungu kaa mbali nazo.
Unakuta watu wanajipa vyeo na kuona kuwa ni Mungu kawapa hizo ndoto. Na wakiota ndoto zikitokea katika maisha yao wanasema mimi Bwana nikiota ndoto huwa zinatokea. Na hawaangali mwisho wao,kwa mfano Mungu kakuonesha jambo baya na wewe unaanza kusema kuna hili na litatokea lakini lengo la Mungu kukuonesha doto hiyo ni ili ujue na uweze kuomba ili kupangua hicho kinachotarajiwa kutokea ulichoota. 


Watu wengi huwa wanafuata miujiza na ona baada ya miujiza kuomba kwao kunapotea sana, na wanaanza kuwa wazito wa kusoma neno la Bwana. Na hata wakisoma hawaelezi. Muuujiza ni kwa ajili ya Mungu na sio wako ni kwa ajili ni kwa ajili ya Mungu.Wana wa Israel walikula Mana  jangwani na walipovuka kwenda kanani Mungu aliwaambia washike jembe walime. 



Mungu aliwaelekeza kwenye maji machungu ili ajifunue kama Yehova Rafa,muujiza umebeba ujumbe, muujiza una sauti ndani,na ndio maana Mungu alikuwa anarudia tena ili waweze kusikia tena. 



Ndio maana biblia inasema haijalishi ndoto unayoota ila cheki matokeo yake, au kama umepewa unabii au muujiza isikupe shida ukitokea ila cheki mwisho wake yaani matokeo yake. Ukiona inakupeleka mbali na Mungu wako ujue kuna shida Fulani. 



Shetani akija kama shetani inaweza ikawa ni rahisi sana kumjua ila sasa anachofanya anakuja kama malaika wa Nuru  lengo lake ni kukupotosha kwa hiyo kuwa makini sana usiamini kila kitu kama unafuata huo msimamo ulioupata ambao shetani kauleta unakuleta kwenye kiburi na ndio maana na Mungu nae anatumia ndoto ili kukuondoa kwenye hayo makusudi yako yaliyo nje ya mapenzi ya Mungu. 



Pia ukipuuzia ndoto ya shetani itakugharimu sana. Kuna watu hawatembei kwenye msimamo wa kanisa la Laiodokia unaosema kumbuka ulipoanguka ukatabu na usipofanya hivyo basi Yesu atakuja kukiondoa kile Kinara chako. Na ujue kuondolewa Kinara ni gharama kubwa sana. 



1 Jambo la Kwanza, Jambo unaloota linaweza kujitokeza kwenye nafsi, kwenye mwili wako na nafsi yako.



2 Likiwa na maelekezo na ukayafuata utaona matokeo yake katika maisha yako. Kama ilivyokuwa kwa Farao, Ayubu na katika Kumbukumbu la Torati. 



Baada ya kuona ndoto  na nimesoma  ndoto nyingi na wengi hawazilewi na shida kubwa sana niliyoiona ni namba ya kuziombea hizo ndoto.
Na mwingine kwa kutokuwajibika anajipachika cheo kuwa kila nikiota ndoto huwa zinatokea, ila hajui kuwa Mungu anataka upangue hiyo ndoto na badala yake wewe unaanza kutangaza. 


MIFANO YA NDOTO MBALI MBALI



1 Kuna mama mmoja mume wake aliota ndoto anakula bui bui na baada ya siku chache alipatwa na kikohozi ambacho alikuwa haponi na alitafuta kila dawa hakupona na alisikia kuwa tunafundisha semina hizi ndipo akaandika ndoto yake akiomba msaada. 



2 Mwingine aliota ndoto ya kugongwa na Nyoka, na katika ndoto aliona katika ndoto kuwa kidole chake kinatoa damu, na aliposhtuka usingizini aliona kweli kidole chake kitoa damu. Na Maisha yake yaliporomoka saa hiyo hiyo. 



3 Mwingine aliota ndoto anagombana  na mwenzie kwenye ndoto na huyo mwenzie alimng’ata mkono na alipoamka aliona alama kwenye mkono wake, 



4  Mwingine aliota ndoto kuwa kuna mtu kaja kwenye ndoto alipokuwa amelala na baada ya kupita muda kidogo alienda hospitali na alikutwa na uvimbe tumboni. 



5 Na mwingine aliota kang’atwa na nyoka kwenye mkono wake wenye pete ya ndoa. Na Baada ya hapo aliona anapata maumivu na akaamua kumuachia yule nyoka kwenye ndoto. Baada ya muda kidogo ndoa yake ilivurugika. Na tulipokuwa tunaomba alikuwa anatusikiliza kwenye redio tukiomba alitapika kitu cheupe . 



Wangapi hapa huwa wanaota ndoto wanakula kwenye ndoto? Na wengine hawajui maana yake ni nini. 1 Wakorintho 10:  15-22 Nasema kama na watu wenye akili; lifikirini ninyi ninenalo. Kikombe kile cha baraka tukibarikicho, je! Si ushirika wa damu ya Kristo? Mkate ule tuumegao, si ushirika wa mwili wa Kristo? Kwa kuwa mkate ni mmoja, sisi tulio wengi tu mwili mmoja;

kwa maana sisi sote twapokea sehemu ya ule mkate mmoja. Waangalieni hao Waisraeli walivyokuwa kwa jinsi ya mwili; wale wazilao dhabihu, je! Hawana shirika na madhabahu? Basi niseme nini? Ya kwamba kile kilichotolewa sadaka kwa sanamu ni kitu? Au ya kwamba sanamu ni kitu? Sivyo, lakini vitu vile wavitoavyo sadaka wavitoa kwa mashetani, wala si kwa Mungu; nami sipendi ninyi kushirikiana na mashetani. Hamwezi kunywea kikombe cha Bwana na kikombe cha mashetani. Hamwezi kushirikiana katika meza ya Bwana na katika meza ya mashetani. Au twamtia Bwana wivu? Je! Tuna nguvu zaidi ya yeye?
Lazima ucheki vizuri unakula nini 



1. Chakula kwenye ndoto inawezeka kabisa ni ushirika wa kimaagano, kati ya mwotaji wa ndoto na hao aliowaota kwenye ndoto na wanaunganishwa na ndoto hiyo na madhabahu iliyobeba ndoto hivyo na madhabahu iliyobeba agano husika. 



Damu ni uhai, hunapelekwa na kunywa kwenye ndoto wengi huwa wanashiriki hivi na kutokujua kuwa wanashiriki agano bila wao kujua. 



Na matokeo yake unaanza kuwa mzito kutoa sadaka, kwa sababu maeneo yote ambayo watu wanatoa sadaka kwa mizimu au miungu. Wanaanza kuwa wazito kutoa sadaka kwa Mungu wetu.  Ila sasa watu hao hao ukiwaita kwenye kikao cha harusi ona hela watakazo toa utashangaa sana. Hali ya kiroho ya mwotaji wa ndoto anaanza kuwa mzito kumtumia Mungu. 



Ndoto inakujulisha kwa kuna agano la kurithi. Ivi unajua kuwa Ibrahimu alifunga agano kwenye ndoto na Mungu fuatilia Kwenye Mwanzo 15:1-21 kwa hiyo agano linaweza fungwa kwenye ndoto. 


Unajua kwanini wana Israel  walipoabudu ndama walitoa sadaka ya Amani na miungu mingine, wanafanya hilo agano na wanashiriki na Ibada ya miungu mingine. Na vitu vya ndoto ni halisi kabisa. Na kwanza kutumika kwenye ndoto Petro , aliona katika maono kwa njia hiyo ndipo alianza kuhubiri injili kwa mataifa. 



MFANO

Sitasahau siku moja nilikuwa na Maswali, niliyokuwa namuuliza Mungu kuhusu baba yangu. Na Mungu alitumia ndoto kunijibu  na siku moja usiku niliota ndoto ya kuwa nimeenda hotelini, na baada ya muda kidogo nikamwona mhubiri mmoja wa marekani anakula chakula. Nikamwambia yule mhudumu niletee chauka pale alipokaa yule mhubiri na nilisogea pale alipo na nikavuta kiti nikakaa pale pale.  Na akainuka na nikamuona ni baba yangu. Alimaliza kula na sahani yake ikawa imesha chakula na akanipa vijiko alivyokuwa anavitumia kula chakula.  Na nikasikia sauiti ikaniambia nitakushibisha kwa wingi wa siku   na neno hili unalipata Zaburi 91:16 Kwa siku nyingi nitamshibisha, Nami nitamwonyesha wokovu wangu  na ndipo nilielewa kuwa baba yangu aliomba kwa Mungu kuwa aondoke kwa sababu alibakiza miaka mitatu tuliyokubaliana. 



NOTE Kitu cha muhimu kujua ni kuwa si kila mara ukitokewa na watu waliokufa kwenye ndoto ina maana ni shetani. Na angalia anakumabia nini, Yesu alipokuwa anaomba alitokewa na Musa na Elia wakati walikuwa wamekufa. 



Tutafanya zoezi hapa na kuombea watu wote waliokula chakula kwenye ndoto. 



Glory to God Glory to God.  Tumwamini Mungu. 

Be blessed.
Axact

Axact

Vestibulum bibendum felis sit amet dolor auctor molestie. In dignissim eget nibh id dapibus. Fusce et suscipit orci. Aliquam sit amet urna lorem. Duis eu imperdiet nunc, non imperdiet libero.

Post A Comment:

0 comments: