Wiki
hii tuwe na tafakari hii Nimeinakili kutoka group la WhatsApp na kuiboresha
kidogo. Simjui mwandishi ila ameandika kitu cha muhimu sana. Japo ningefurahi
kumjua mwandishi ili nimpe zawadi yake. Nimeona na wadau wa Pata ufahamu Blog
tuongeze ufahamu kupitia fuzo hili.
Michael
Jackson alikuwa ni binadamu mwenye ndoto nyingi lakini Ndoto zake 2 kuu
maishani zilikuwa ni:
1.
Kwanza ni kuwa mwanamziki mkubwa zaidi duniani wa Pop.
2.
Kuishi miaka 150.
Baada
ya kuifanikisha ndoto yake ya kwanza kwa ufanisi mkubwa akiwa na miaka 25 tu
aliamua kuanza kuwekeza kwenye ndoto yake ya pili ambayo kwa wakati huo ilikuwa
ndiyo takwa lake kubwa.
Ili
aweze kuishi miaka 150 (Karne moja na nusu) aliamua kufanya mambo yafuatayo:
1.
Aliajiri madaktari binafsi 12 wa kumchunguza mwili wake wote hadi nywele na
kucha kila siku.
2.
Ilikuwa ni lazima chakula chake kipitie maabara kupimwa kabla hajala.
3.
Aliwaajiri wataalamu 15 kufuatilia mazoezi, kazi na kila jambo alilofanya kila
siku.
4.
Alitengeneza kitanda maalumu kilichokuwa na uwezo wa kufanya 'regulation' ya
hewa.
5.
Watu 50 waliwekwa tayari kujitolea viungo vyao kama angepata dharura yoyote.
Aliwalisha watu hao, aliwatunza na kuwalipa mshahara kila mwezi kwa kazi hiyo.
Baada
ya kufanya hayo alikuwa na uhakika wa kuishi karne moja na nusu bila mashaka
yoyote. Lakini June 25, mwaka 2009 akiwa na miaka 50 tu moyo wake ulizima
ghafla na ndoto yake ikawa imefika mwisho.
Timu
ya madaktari wake bingwa 12 haikuweza kuzuia pumzi yake isiondoke. Wale watu 50
waliowekwa 'standby' kumpa viungo hawakuweza kumsaidia. Akazima ghafla kama taa
ya umeme iliyoishiwa luku.
Pamoja
na juhudi za madaktari wengine kutoka Calfornia na Los Angeles hawakuweza pia
kuokoa maisha yake. Mtu ambaye kwa miaka 25 alikuwa hawezi kunyanyua unyayo
wake bila ushauri na ruhusa ya madaktari akawa kafika mwisho bila kutimiza
ndoto yake ya kuishi miaka 150.
Safari
ya mwisho ya Michael Jackson ilishuhudiwa moja kwa moja na zaidi ya watu
milioni 3, rekodi ambayo haijavunjwa hadi sasa. Ndiye mtu aliyepata kuagwa na
watu wengi zaidi katika historia ya dunia tangu enzi za Pontio Pilato.
Siku
aliyofariki mitandao mikubwa ya Wikipedia, Twitter, Yahoo, AOL's instant
messenger ilielemewa na mzigo wa watumiaji waliokuwa wakisaka taarifa za kifo
hiki hadi ikaacha kufanya kazi. Google pia ilivunja historia ya matumizi yake
kwa siku ile.
Michael
Jackson alitaka kupambana na kifo lakini hakuweza hata kufikia nusu ya umri
aliopenda kuuishi. Mtu aliyekuwa na uwezo wa kufanya lolote ili aweze kuishi
umri autakao lakini alizima kama mshumaa upulizwapo na upepo. Biblia inasema ni
yupi kwenu ambaye akijisumbua aweza kujiongeza kimo chake hata mkono mmoja?
Hakuna. (Mathayo 6:27).
Ikiwa
hatuwezi kuongeza hata kimo chetu basi hatuwezi kufanya lolote kuhusu hatma ya
maisha yetu. Michael Jackson alifanya yote yaliyowezekana ili aishi miaka 150
lakini hakufika hata nusu ya umri huo. Lakini kuna mzee asiye na uhakika wa
milo mitatu kule Tandahimba, Rombo, Ngara au Tukuyu ameishi umri mkubwa hata
mara mbili ya Michael Jackson. Ni kwa neema tu.
Uhai
na uzima tulionao ni zawadi kutoka kwa Mungu. Sio kwamba tunastahili kuliko
wengine, hapana! Sio kwamba tumejitunza kuliko wengine, hapana! Ni kwa neema
tu. Hata hatma ya maisha yetu ipo mikononi mwa MUNGU mwenyewe.
Hapa
duniani hatuna mji udumuo bali sote twautafuta ule ujao. Ishi kwa upendo na
amani na watu wote. Maandiko yanasema mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke siku
zake za kuishi si nyingi (Ayubu 14:1). Tumuombe Mungu atuepushe na kiburi,
atujaze upendo. Mungu atufundishe kuzihesabu siku zetu na kutujalia mwisho
mwema.!
Ila
Jambo moja la muhimu sana ambalo unaweza kulifanya likakupa uhakika wa Maisha yako
ni
Kumwamini
Yesu kristo kuwa Bwana na Mwokozi wa Maisha yako, hakika utakuwa upo kwenye eneo
zuri san ahata pale utakapo ondoka hapa duniani utakuwa umejiandalia eneo
salama la kufikia, Mwamini yesu leo upate uzima wa milele.
Fuatisha
sala hii:
Nihurumie, Ee
Mungu, kadiri ya fadhili zako; ufutilie mbali makosa yangu, kadiri ya wingi wa
huruma yako. Unioshe kabisa hatia yangu; unisafishe dhambi yangu. Nakiri kabisa
makosa yangu, daima naiona waziwazi dhambi yangu. Nimekukosea wewe peke yako,
nimetenda yaliyo mabaya mbele yako. Uamuzi wako ni wa haki hukumu yako haina
lawama. Mimi ni mkosefu tangu kuzaliwa kwangu, mwenye dhambi tangu tumboni mwa
mama yangu. Naomba unifute jina langu kwenye kitabu cha hukumu na
uandike jina loangu kwenye kitabu cha Uzima, kwa Jina la Yesu kristo….Amen
Hongera
kwa kuokoka
Ni mimi ndugu yako; Mwl Nicholaus Simon.
Kiungo katika mwili wa kristo.
Kwa msaada zaidi na ushauri.
Mawasiliano: +255 766 635 382
pataufahamu@gmail.com
Ubarikiwe sana Na nakuomba nisaidie kuishare kwa marafiki zako ili na
wao wajifunze Neno la Mungu.
Post A Comment:
0 comments: