Imani |
Maandiko: Marko 9:19-23
19 Akawajibu,
akasema, Enyi kizazi kisichoamini, nikae nanyi hata lini? Nichukuliane nanyi
hata lini? Mleteni kwangu 20 Wakamleta kwake; hata alipomwona, mara yule pepo
alimtia kifafa; naye akaanguka chini, akagaa-gaa, akitokwa na povu. 21
Akamwuliza babaye, Amepatwa na haya tangu lini? Akasema, Tangu utoto. 22 Na
mara nyingi amemtupa katika moto, na katika maji, amwangamize; lakini
ukiweza neno lo lote, utuhurumie, na kutusaidia. 23 Yesu akamwambia, Ukiweza!
Yote yawezekana kwake aaminiye. 24 Mara babaye yule kijana akapaza sauti,
akasema, Naamini, nisaidie kutokuamini kwangu.
Imani ya kweli katika Yesu ni
msingi imara katika maisha ya kiroho. Ni jibu la mambo yote. Ni mkono
unaochukua majawabu ya mahitaji yetu kutoka ulimwengu usioonekana na
kuyafikisha kwenye ulimwengu wa mwili, tukaona kwa macho na kushika kwa mikono
yetu.
Imani ni nini?
Basi imani ni
kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana.
(Ebr 11:1)
Imani
inakuthibitishia kuwa kitu unachokihitaji kimepatikana sasa wakati kinatarijiwa;
imani inakiona:kitu halisi na kukikamata wakati hakipo.
Nchi
ya Israeli ilikumbwa na ukame mbaya sana, ikatokea njaa kali, ikasababisha watu
kula watoto wao, punda na mavi ya njiwa. Katika nyakati hizo za ukame nabii
Elisha aliyekuwa na imani katika Mungu alitangaza kuwa kesho kutapatikana unga
tele na nafaka mbalimbali. .Imani iliona mbali ikavuka mipaka ya ufahamu wa
kibinadamu. Askari wa mfalme aliona kmwili Elisha aliona kiroho.
Elisha
akasema, Lisikieni neno la Bwana; Bwana asema hivi, Kesho panapo saa hii,
kipimo cha unga mzuri kitauzwa kwa shekeli, na vipimo viwili vya shayiri kwa
shekeli, langoni pa Samaria (2Fal
7:1)
Kesho
yake kweli yote yalitimia; soma (2Fal 7:1-20) Askari wa mfalme alikufa kwa kutokuamini.
Imani
inazaliwa na inakua.
Basi imani,
chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo. (Rum 10:17)
Imani
ya kweli inazaliwa kwa kusikia Neno la Kristo. Imani inakua kila wakati
inapotumika kuleta majibu ya mambo magumu. Yesu alifundisha somo la imani
inayoleta matokeo.
(Mathayo
17:20) Yesu
akawaambia, Kwa sababu ya upungufu wa imani yenu. Kwa maana, amini, nawaambia,
Mkiwa na imani kiasi cha punje ya haradali mtauambia mlima huu, Ondoka hapa
uende kule; nao utaondoka; wala halitakuwako neno lisilowezekana kwenu.
Imani
inayoweza kuhamisha milima ya matatizo yako yote, inanza na kiasi cha punje ya
haradali iliyo ndogo kuliko punje ya mchicha. Fahamu kuwa punje hiyo ikipandwa
inaota na kukua hadi kuwa mti mkubwa. Na imani yako itakua kwa kadiri
unavyoitumia kutatua matatizo yanayokukabili siku kwa siku.
Daudi
alikuwa na ujasiri wa kukabiliana na Goliathi kwa sababu imani yake ilikua katika
Bwana kwa kuwaua simba na dubu.
(1Sam17:36 ) Mtumishi wako alimwua simba
na dubu pia; na huyu Mfilisti asiyetahiriwa atakuwa kama mmoja wao, kwa sababu
amewatukana majeshi ya Mungu aliye hai.
Baba
wa kijana tuliyemsoma hapo juu alimwomba Yesu kwa mashaka akisema, “lakini ukiweza neno lo lote, utuhurumie, na
kutusaidia”. Bwana Yesu alimjibu kwa maneno yake , “Ukiweza! Yote yawezekana kwake aaminiye”. Yule baba alitambua
haraka kosa lake akatubu na kuamini. Yesu akamponya mwanawe saa ileile.
Kizazi
chetu tunafanana na baba huyo; tunafahamu kuwa Yesu anaponya, anaokoa na
kutenda miujiza mingi. Inapokuja kwenye mahitaji yako wewe binafsi imani
inapungua. JiulizeYesu amekufanyia nini? na unamtarajia akufanyie nini katika
matatizo yako? Je unaamini kweli
anaweza? Je moyoni mwako mna mahangaiko na kutangatanga kutafuta ufumbuzi?.
Kutokuamini ni dhambi na kunakukosesha majibu ya mahitaji magumu ya moyo wako.
Mungu hashindwi na neno lolote.
Ushuda wa kweli : Umetokea katika nyanda za juu kusini mwa Tanzania.
Mama mmoja alikuwa na tatizo katika kizazi, akafanyiwa upasuaji wa kukiondoa.
Hakuwa amejaliwa mtoto yeyote. Alihuzunika sana kukosa mtoto. Akaamua kumwamini
Mungu atendaye miujiza kupita fahamu za kibinadamu. Akatamka nitazaa mtoto kwa
tumbo langu na kumnyonyesha kwa matiti yangu. Madaktari walimkanusha na watu
wakamdhihaki. Muda si mrefu akayaona anabadilika , miezi tisa akazalishwa mtoto
mzuri na daktari yuleyule aliyeondoa tumbo la uzazi. Mungu ni wa kushangaza
ndiyo sababu anaitwa MUNGU anafanya njia pasipo na njia.
Alimpa
mtoto mama asiye na tumbo la uzazi, atakosaje wewe mtoto uliye na tumbo? muujiza
ni wako wewe, gharama ni imani ya kweli kwa Yesu , anakwambia,” Yote yawezekana kwake aaminiye.”
Rev. Mwl. F.M.Swenya
Mawasiliano:
+255 67 469 595, 0784 469 595
+255 67 469 595, 0784 469 595
Email: swenyaflorian@gmail.com
Post A Comment:
0 comments: