BIBLIA ISEMAVYO KUHUSU UTATU NA DR MWALUSAMBO

Utatu wa Mungu ni moja ya mafundisho yenye utata mkubwa sana katika Biblia, ingawa ni fundisho maarufu sana katika madhehebu mbalimbali. Neno „Utatu‟ halipatikani katika Biblia, bali ni neno lililoumbika kifikira tu (imagination). Kutokana na kukosekana kwa maandiko yanayozungumzia utatu wa Mungu moja kwa moja, fundisho hili limekuwa na maswali mengi sana yasiyo na majibu. Biblia inamwelezea Mungu kwa majina matatu, yaani Baba, Mwana au Yesu Kristo na Roho Mtakatifu; majina haya matatu yanajulikana kama „nafsi‟ tatu katika Mungu mmoja; na hiki ndicho chanzo cha utata wa somo hili.

Jambo kubwa la kuzingatia ni hili: Biblia nzima ina umoja wa ajabu sana usioweza kuvunjwa na mwanadamu; yeyote anayejaribu kufanya hivyo, kamwe hawezi kupata maana halisi ya makusudi ya Mungu katika kitabu hiki, yaani Biblia. Ili kuipata maana halisi iliyokusudiwa na Agano la kale, msomaji anapaswa kulinganisha na Agano jipya; kadhalika, ili kupata maana halisi iliyofichwa katika Agano jipya, msomaji anapaswa kulinganisha na Agano la kale. Hii ni kanuni muhimu sana kwa kila msomaji yeyote anayetaka kuielewa Biblia na umoja wake usioweza kutenganishwa kamwe.

Kuna mafundisho mbalimbali ndani ya makanisa ambayo yamerithiwa kutoka kwa waasisi wa madhehebu, yaliyojengwa bila kuzingatia kanuni ya umoja wa Biblia ambayo ina umoja wake unaokubaliana, na majibu yake yasiyopingana; iwe ni Agano la kale, au Agano jipya. Lakini sasa mambo yamekuwa tofauti kabisa! Kuna maswali mengi ambayo yanaonekana kuwa hayana majibu ingawa si kweli. Hii inatokana na kwamba kanuni za Biblia zinavunjwa, na kupata majibu yanayotokana na hisia za wanadamu tu, na wala si kutoka katika Biblia.

Swali la kwanza linalojitokeza kuhusiana na utatu wa Mungu ni hili: “Ikiwa kuna nafsi tatu katika Mungu mmoja, kwa nini isijulikane kuwa ni miungu watatu?”

Kwa Maswali au Ushauri Wasiliana nasi kwa:

+255 754 041 599, +255 766 635 382

Email: info@mwalusambo.or.tz

Next
This is the most recent post.
Previous
Taarifa za zamani
Axact

Axact

Vestibulum bibendum felis sit amet dolor auctor molestie. In dignissim eget nibh id dapibus. Fusce et suscipit orci. Aliquam sit amet urna lorem. Duis eu imperdiet nunc, non imperdiet libero.

Post A Comment:

0 comments: