Swali: "Biblia Inasema Nini Juu Ya Kushirikiana Katika Ngono Kabla Kuoana?"

Jibu: 
Pamoja na matendo mengine ya uchafu, kufanya kitendo cha mapenzi kabla kuoana kumekatazwa katika maandiko; -

Matendo 15:20;
 bali tuwaandikie kwamba wajiepushe na unajisi wa sanamu, na uasherati, na nyama zilizosongolewa, na damu.” 

 Warumi 1:29;
“Wamejawa na udhalimu wa kila namna, uovu na tamaa na ubaya; wamejawa na husuda, na uuaji, na fitina, na hadaa; watu wa nia mbaya, wenye kusengenya,”

2Wakorintho 12:21;
“nami nitakapokuja tena, Mungu wangu asije akanidhili kwenu, nami nikawasikitikia wengi waliokosa tangu hapo, wasiutubie uchafu, na uasherati, na ufisadi walioufanya.

Wagalatia 5:19;
Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi,” 

Waefeso 5:3;
Lakini uasherati usitajwe kwenu kamwe, wala uchafu wo wote wa kutamani, kama iwastahilivyo watakatifu; 
Wakolosai 3:5;
Basi, vifisheni viungo vyenu vilivyo katika nchi, uasherati, uchafu, tamaa mbaya, mawazo mabaya, na kutamani, ndiyo ibada ya sanamu; 

1Wathesalonike 4:3;
“Maana haya ndiyo mapenzi ya Mungu, kutakaswa kwenu, mwepukane na uasherati;” 

Yuda 1:7).
“Kama vile Sodoma na Gomora na miji iliyokuwa kando-kando, waliofuata uasherati kwa jinsi moja na hawa, wakaenda kufuata mambo ya mwili yasiyo ya asili, imewekwa kuwa dalili, wakiadhibiwa katika moto wa milele. 
waebrania 13:4
“Ndoa na iheshimiwe na watu wote, na malazi yawe safi; kwa maana waasherati na wazinzi Mungu atawahukumia adhabu.

Utaongezea: 1Wakorintho 5:1; 6:13, 7:2; 10;8;

Biblia inasisitiza kuepuka kitendo hicho kabla ya ndoa. hii ina maana ya kuwa ni dhambi kama ya uzinifu kwa kuwa hujaunganishwa na unayefanya naye kitendo hicho. Mapenzi baina ya mume na mke waliooana ndiyo mapenzi yanayokubalika mbele za Mungu.

Kushirikiana katika ngono kabla ndoa kumeenea sana kwa sababu nyingi kwanza Mapenzi yanastarehesha. Mungu aliyaumba hivyo. Anawataka wanaume na wanawake wafurahie kitendo cha ngono (ndani ya ndoa). Hata hivyo, lengo la msingi la ngono si starehe bali kuzaana tukaongezeke. Hivyo tunazuiwa kufanya kitendo cha ngono kabla ndoa ili tusijipatie watoto tusiowatarajia. Kujizuia kunaokoa maisha, kunalinda watoto wachanga na kuleta ladha halisi ya ngono pamoja na heshima kwa Mungu.


Tafakari hayo kwa kina.
Nikutakie Wakati mwema ndugu yangu.
By; Counselor Nicholaus Simon.
Source:jifunzenauelimike

Axact

Axact

Vestibulum bibendum felis sit amet dolor auctor molestie. In dignissim eget nibh id dapibus. Fusce et suscipit orci. Aliquam sit amet urna lorem. Duis eu imperdiet nunc, non imperdiet libero.

Post A Comment:

1 comments: