Mtu wa Mungu tambua, Mungu alikuumba kwa kusudi. Yawezekana bado hujui lile kusudi, na hilo ni sawa. Mungu alikuumba na ujuzi na vipaji. anapo kutazama anaona kuwezekana kwa mambo kusiko na ukomo.  Mojawapo ya makusudi ya Mungu kwako, ni wewe kuwa na uhusiano na Yesu. Uhusiano huo unafungua fursa nyingi maishani mwako. 
Mfano Yesu akiwa mtoto, utaona Wazazi wake walimchukua mtoto ambaye ni  Yesu, wakaenda naye Yerusalemu ili wamweke mbele ya Bwana. Wakati huo huko Yerusalemu kulikuwa na mtu mmoja, mwema na mcha Mungu, jina lake Simeoni, Roho Mtakatifu alikuwa amemhakikishia kwamba hatakufa kabla ya kumwona kristo wa Bwana. Basi akiongozwa na Roho Mtakatifu, Simeoni aliingia hekaluni; na wazazi wa Yesu walipomleta hakaluni mtoto wao, Simeoni alimpokea mtoto Yesu mikononi mwake huku akimtukuza Mungu, akisema: sasa Bwana, ametimiza ahadi yake, umruhusu mtumishi wako aende kwa amani. ‘’Kwa maana kwa macho yangu nimeuona wokovu ulioleta. Ambao umeutayarisha uonekane na watu wote’’ Baba yake Yesu na mama yake walikuwa wakistaajabia maneno aliyosema simeoni juu ya mtoto. Simeoni akawabarikia, akamwambia Maria mama yake, ‘‘Naye atakuwa ishara itakayopingwa na watu; nawe mwenyewe, uchungu ulio kama upanga mkali utauchoma moyo wako.’’
Jambo kubwa ambao nimeona vyema nikushirikishe kuwa ,hakuna mtu anaye jua uwezo uliopo ndani yako ila Mungu peke yake, yawezekana katika maisha kila unapo fanya jambo watu huanza kukubeza na kusema huwezi fanikiwa, wayasemayo si yakweli kwasababu hawajui uwezo uliopo ndani yako, ‘‘Tambua Nabii akubaliki kwao’’ hata wewe si lahisi kukubalika katika jamii inayo kuzunguka ukianzia katika familia, majilani na ndugu kiujumla wote hawa hawawezi kujua hatima ya maisha yako. hata Yesu Katika jamii yake hawakumjua na ndomana walimsulubisha kama wangemjua wasingeweza kumsulubisha.
Nikutie moyo kuwa wewe ni mtu wa thamani sana katika hii dunia na hakuna mtu kama wewe na hata kuwepo. kwahiyo jisikie vizuri kuwepo duniani, na utambue kuwa haupo kwa bahati mbaya bali upo kutimiza agizo au kusudi la Mungu kwako katika maisha yako.
Tukisoma kitabu cha zaburi utamwona mtumishi wa Mungu Daudi akimshukuru Munu kwa jinsi alivvyo .
Zaburi 139:14-18 ‘’Nitakushukuru kwa kuwa nimeubwa kwa jinsi ya ajabu ya kutisha. Matendo yako ni ya ajabu, Na nafsi yangu yajua sana, Mifupa yangu haikusitirika kwako, Nilipoumbwa kwa siri, Nilipoungwa kwa ustadi pande za chini za nchi; Macho yako yaliniona  kabla sijakamilika ; Chuoni mwako ziliandikwa zote pia, siku zilizo amriwa kabla hazijawa bado. Mungu fikira zako zina thamani nyingi kwangu; Jinsi ilivyo kubwa jumla yake.  Kma ningezihesabu ni nyingi  kuliko mchanga; Niamkapo nikali pamoja nawe’’.
Hakika wewe ni wathani sana tena sana, Umeubwa kwa jinsi ya ajabu na kutisha na siku zako za kuishi zote zimehesabiwambele za Mungu. Katika maisha yako jitahidi sana kugundua una kipaji au huduma gani ambayo Mungu ameweka ndani yako kwasababu kupitia hiyo, ndiyo yenye mafaniko yako.

MUHIMU:waliofanikiwa sana ni wale wote wanaotumia vipawa ambavyo Mungu ameweka ndani yao.
  
NJIA 10 ZA KUJIANGALIA NA KUJIHISI BORA.
1. Mfahamu aliyekuumba.
2. Lala vyakutosha. Kutolala vya kutosha husababisha siku zisizo na ufanisi an kudhoofisha kinga ya mwili.
3. Punguza kutumia sukari, ila kunywa maji sana.
4. Furahia mafanikio yaw engine,usijiangalie wewemwenyewe tu.
5. Jitunze vizuri. Uliubwa kwa mikono ya Mungu.
6. Kuwa wewe halisi. Hakuna haja ya kuigiza.
7. Usijijenge kwa kuwashusha wengine.
8. Usikae tu, fanya kazi na maziezi.
9. Vaa tabasamu.
10. Tunza mwonekano wako, kwasababu ni wewe tu unayeweza.


Ni mimi ndugu yako; Mwl Nicholaus Simon.
Kiungo katika mwili wa kristo.
Kwa msaada zaidi na ushauri.
Mawasiliano: +255 766 635 382
pataufahamu@gmail.com

Ubarikiwe sana Na nakuomba nisaidie kuishare kwa marafiki zako ili na wao wajifunze Neno la Mungu.

Axact

Axact

Vestibulum bibendum felis sit amet dolor auctor molestie. In dignissim eget nibh id dapibus. Fusce et suscipit orci. Aliquam sit amet urna lorem. Duis eu imperdiet nunc, non imperdiet libero.

Post A Comment:

0 comments: