Popote palipo na ushindi lazima kuwe na nguvu iliyotumika katika kuleta ushindi ule.Nguvu ile inaweza kuwa nguvu ya kifkra ,silaha,maneno na ibada.Ukristo mpaka ulipo hapa leo na ulivyo leo hii si kwamba umefika fika tu ,kuna nguvu kubwa ilitumika katika kuueneza,wengi walisimama kuupinga,na hata wengi waliumizwa ,kwa kuteswa na  kuuwawa kwa vifo vya kutisha.
Kwa mfano, ukifuatilia historia utaona kuwa Yakobo yule mkubwa aliuawa kwa kukatwa kichwa na herode mfalme(rejea mdo 12:1-2) ,mtume Petro aliuawa kwa kusurubiwa miguu juu , kichwa chini na Kaisaria Nero mwaka 67 B.K  na mtume paulo aliuawa kwa kukatwa kichwa na kaisaria Nero mwaka wa 65 B.K na wengine wengine waliofuatia kutokana na utawala dharimu wa Kirumi.Hata hivyo nguvu ya kushinda iliyokuwemo ndani ya Mitume ilikuwa kubwa sana kuriko hofu na changamoto zilizokuwa zinazunguka huduma zao.Mtume paulo anaeleza mateso mengi aliyapata kutokana na kujitahidi kwake kuieneza injili,anasema kuwa “Lakini,ndugu zangu,nataka mjue ya kuwa mambo yote yaliyonipata yametokea  zaidi kwa kuieneza injili.hata vifungo vyangu vimekuwa dhahiri katika Kristo,miongoni mwa askari,na kwa wengine wote pia” Wafilipi 1:12 pia katika ,2kor 11:23-27 “katika taabu kuzidi sana ;katika vifungo kuzidi sana ;katika mapigo kupita kiasi,na katika mauti  mara nyingi.Kwa Wayahudi mara tano nalipata mapigo arobaini kasoro moja.mara tatu nalipigwa na bakora;mara moja nalipigwa kwa mawe;mara tatu nalivunjikiwa na jahazi;kuchwa kucha nimepata kukaa kilindini;katika kusafiri mara nyingi;hatari za mito;hatari za wanyang’anyi;hatari kwa taifa langu;hatari kwa mataifa mengine;hatari za mijini;hatari za jangwani;hatari za baharini;hatari kwa ndugu za uongo;katika taabu na masumbufu;katika kukesha mara nyingi;katika njaa na kiu;katika kufunga mara nyingi;katika baridi na kuwa uchi”.Paulo anadhihirisha pia kuwa utendaji wake wa kazi ulikuwa unatokana na nguvu iliyokuwemo ndani yake,ukisoma,Kol 1:29.
Kwahiyo katika safari ya maisha lazima kila mwanadamu ajenge nguvu ya kushinda kwani bila hivyo atajikuta ameondolewa katika ulimwengu kama mwanasayansi Charles Darwin aliyeleta hoja ya “survive for the fittest” yaani “ishi kwa uzuri/uimara” akidai ya kuwa, uzuri au uimara wa mtu ndio unaomwezesha aendelee kuishi duniani kwasababu utamsaidia kujipatia mahitaji yake ya mhimu ya kumwezesha aendelee kuwa hai.
                Kuna msemo wa kiswahili husema kuwa “ukiona vyaelea, jua vimeundwa” maana yake nini? Hii inatuonyesha kuwa kila kitu tunachokiona humu duniani kuna nguvu fulani ilitumika ili kukitengeneza ,hata Mungu alipokuwa anaumba duniani ,hakuitokeza tu,alitumia nguvu ya kinywa kuweza kuiumba.
                Tukumbuke kuwa, Adamu baada ya kutenda lile kosa la kula tunda katika bustani ya edeni,alipewa jukumu la kufanya kazi ili aweze kuishi duniani,nalo ni la kutumia nguvu,baada ya kuambiwa kuwa “atakula kwa jasho lake(Mwanzo 3:17-19)”.
  Nguvu ile ndiyo inayomwezesha mwanadamu kufanya kazi,wanasaikolojia wanaiita ile nguvu”libido”.

Katika safari ya maisha tumekuwa tukipitia maisha ya aina mbalimbali,lakini yamegawanyika katika sehemu mbili ambazo ni masha ya kushinda na maisha ya kushindwa.








Tunaweza kujiuliza kwanini wakati mwingine tunashinda na kwanini wakati mwingine tumekuwa tukishindwa  huenda ni jambo lile lile? Au tunaweza kujiuliza kwanini watu wengine wamekuwa mbele yetu katika mambo mbalimbali ya kimaisha?
  Nguvu ya kushinda ni uwezo unaomwezesha mtu ili aweze kushinda anapokuwa anatembea katika dunia hii akipitia maisha mbalimbali.Maisha yetu yamegawanyika katika sehemu kuu mbili ,sehemu ya kwanza ni maisha ya furaha baada ya ushindi na upendo na maisha ya huzuni baada ya kushindwa kutokana na ugonjwa ,kifo,ajari.
Kumbuka kuwa uwezo wa kushinda umekaa ndani ya akili ya mtu mwenyewe,mwanafalsafa mmoja alisema kuwa “kiwango cha mafanikio ya mtu kinapimwa au kinajengwa katika fikra za mtu” maana yake, jinsi mtu anavyowaza ndivyo atakavyofanikiwa. Ninaweza kusemakuwa, aina ya mafanikio na kiwango cha mafanikio aliyonayo mtu ni matokeo ya fikra na juhudi za mtu katika kuyawaza yale mafanikio na kujitahidi kuyapigania mpaka kuyapata.
   Yapo mambo mengi yanayochangia kuunda nguvu ya kushinda kama yakifuatwa.
 Jambo la kwanza na kubwa kuriko yote ni, Neema ya Mungu maishani mwa mtu, tunaweza kuzania  ya kuwa baada ya mwanadamu kuondolewa katika bustani ya edeni akapewa jukumu la kutafuta mahitaji yake kwa nguvu zake,huenda Mugu alimwacha mwanadamu pekee yake asimsaidie hata kidogo,lakini ukweli ni kwamba bado Mungu amekuwa akiachilia nguvu zake kwa mwandamu ili kumsaidia katika harakati zake za kujitafutia mahitaji yake.    
 Mtume Paulo katika kitabu cha Waraka wa pili kwa wakorintho sura ya kumi na tano mstari wa kumi, anasema kuwa ameweza kufanikiwa kupita hata mitume waliomtangulia kutokana na neema ya Mungu inayoizunguka huduma yake  “Lakini kwa neema ya Mungu nimekuwa hivi nilivyo;na neema yake iliyo kwangu ilikuwa si bure,bali nalizidi sana kufanya kazi kupita wao wote;wala si mimi ,bali ni neema ya Mungu pamoja nami”.1Kor 15:10.
       Hapa ninaposema neema ya Mungu ninamaanisha nguvu ya uwezo anayopewa mtu na Mungu au miungu kutokana na kufuata taratibu za ibada au kutokana na upendo wa Mungu au miungu. Kuna wakati mwingine tunaweza kuwashuhudia marafiki zetu wakifanikiwa sana au waking’ara sana tukashindwa kuelewa kuwa ni kwa sababu gani.Lakini hii ndiyo neema ya Mungu au miungu ,kumbuka, hata shetani naye ana neema yake anayoiachilia kwa watu wanaomwabudu kama anavyomwambia Bwana wetu Yesu Kristo katika Luka4:6- 7  akisema “Ibilisi akamwambia ,nitakupa wewe enzi hii yote,na fahari yake ,kwa kuwa imo mikononi mwangu,nami humpa ye yote kama nipendavyo.Basi ,wewe ukisujudia mbele yangu  yote yatakuwa yako”.
Kwa hiyo si kwamba tunapoona watu wanafanikiwa tunazania huenda ni kwasabu ya uwezo wao wa kufikiria au juhuda zao ,la, bali ni nguvu fulani  iliyonyuma yao.Ndiyo maana leo tunasikia mara Freemasons na wengine mara wanaenda kwa waganga wa kienyeji, na wengine kuombewa, yote haya ni kwa ajiri ya kutafuta usaidizi wa Mungu au miungu.Kumbuka kuwa uwezo wa mwanadamu unampaka au unamwisho.Kuna mwanafalsafa mwingine alisema kuwa “maisha ya mwandamu yako chini ya uangalizi au usimamizi wa Mungu,miungu”.Labda niweke sawa hapa kuwa ,kwa kila mtu  ipo neema ambayo Mungu huiachilia kwake ili kumsaidia kudumu katika dunia hii au kushinda upinzani unaojitokeza katika maisha yake,kinachotofautiana ,ni aina ya neema ,kiwango cha utendaji wa ile neema na jinsi mtu anavyoitumia ile neema.
               
Hili  nilieleze kwa kukumbusha kuwa, wakati ukiwa bado uko darasani au kazini kwako ,kwanini kuna  wanafunzi wenzetu wamekuwa wakiwa na uwezo mkubwa kimasomo na hata tukitumia nguvu nyingi sana lakini bado hatuwezi kufikia uwezo wao. Lakini makazini tunaweza kujiuliza juu ya uwezo  wa wafanyakazi wenzetu ,wapo wamekuwa na uwezo mkubwa wa kufanya kazi na kuzisaidia taasisi au makampuni kuweza kukua kwa haraka sana.Lakini kibiashara tunaweza kujiuliza kwanini biashara za watu wengine zinakuwa kwa kasi sana na zetu zinakuwa kwa kasi kidogo au inatokeaje mtu kukubalika kwa watu na mwingine kukataliwa na watu?
                Hapa ndipo tunapoongelea neema ya Mungu, inakupa nguvu ya kufanikisha jambo Fulani kwa wakati Fulani kwa kukupa kibali mbele za watu kwa kazi unayoifanya au kuzidisha juhudi yako ya kupigania mafanikio.Kuna mtu mmoja alisema hivi “uweza na utajiri wa mwanadamu ni matunda ya neema ya Mungu” .
.Mfano ,tunaona viongozi ,wasanii ,wachezaji na wafanyabiashara waking’aa, si kwa juhudi zao tu bali kwa ile neema ya Mungu inayoandamana nao.
   Kwahiyo kwa kifupi “mwanadamu amekuwa vile alivyo kutokana na kiwango na aina ya neema inayomzunguka”
.

Jambo la pili ni mtazamo.Mtazamo ni jinsi unavyowaza na kuhisi juu ya kitu Fulani.Watu wengi wameshindwa kutimiza ndoto zao au kufikia katika mafanikio ambayo wamekuwa wakiyaota kutokana na mitazamo yao juu ya hayo mafanikio ,hii inaweza kuwa ni kutokana na mapito wanayopitia ,mfano wakati mwingine tumekuwa tuna ndoto nyingi sana lakini kutokana na maisha magumu au changamoto tunazokumbana nazo tumefikia kipindi tumekata tamaa.
Lakini pia mazingira ya kuyafikia hayo mafanikio yamekuwa yakichangia watu kukata tamaa.Kulingana na ugumu ulioko mbele ya safari ya mafanikio tunayoyaendea yamekuwa yakitufanya tubadili mitazamo yetu ,mfano, wanafunzi wengi wanaacha kusoma masomo ya sayansi kutokana na kusikia kuwa ni magumu na watu ambavyo wamekuwa wakiyasema. au kutokana na kuwa kuna kazi zingine ukisoma unapata kazi moja kwa moja, watu wengine wameacha kusomea kozi ambazo wanazipenda kwasababu ya hofu ya ajira.Mwanasaikolojia Wiliam James anaseama ,kuwa, “wanadamu wanaweza kugeuza maisha yao ,kwa kugeuza mitazamo ya akili zao”.Mitazamo yetu inatakiwa kuendana na ndoto zetu au kule tunakotaka kufika.
                 Kwahiyo jinsi unavyowaza na kujisikia juu ya mafanikio ndivyo utakavyokuwa. Ingawa kunaweza kuwa na ukinzani lakini mtazamo wako juu ya yale mafanikio yatakufanya ufikie mafanikio.Kumbuka kuwa, changamoto si kwamba inakutuzuia tusiweze kufikie mafanikio yetu ,bali inapunguza kasi yetu kuelekea mafanikio ,ni sawa na milima na mabonde ,hayaizuii gari kuendelea na safari bali yanapunguza kasi kuelekea nwisho wa safari.
  Mtazamo wa mafanikio unakupa nguvu ya kuendelea kupigania mafanikio na pia unakufanya uvumilie.
                Tatu, kubali kubadilika,katika safari ya kuelekea katika mafanikio unatakiwa wakati mwingine kuwa kama kinyonga ,ninaposema kubadilika si manisha kuondoka au kuacha njia uliyokuwa unaipita bali pia kuboresha ile njia .Kwa mfano kama ulikuwa unafanya kazi kwa masaa sita lakini unaona kabisa kuwa masaa hayo hayatoshi kukufanya ufanikiwe unatakiwa kuongeza masaa mengine,mfano uanze kufanya kwa masaa tisa.Kwa mwanafunzi kama ulikuwa unatenga muda wa masaa mawili kwa ajili ya kujisomea unapaswa kuongeza lisaa moja.Kwa mwombaji kama ulikuwa unaomba mara mbili kwa siku unatakiwa kuongeza iwe mara tatu kwa siku au kama ulikuwa unafunga kwa masaa kumi na mbili unatakiwa kufunga kwa masaa ishirini na nne. si hivyo tu, unaweza ukatafute njia nzingine za kuongeza kipato,mfano kama wewe ni mwalimu,unaweza ukaanzisha kilimo au ufugaji wa kuku. Unaweza kuanzisha kampuni wakati ukiwa umeajiriwa, lengo ni kukuza kipato chako.
                Ubunifu unatuwezesha kushinda changamoto mbalimbali tunazokumbana nazo katika safari yetu ya maisha.
 Nne ,kutumia fursa,Katika maisha ,watu wengi wamekuwa wakishindwa kutimiza ndoto zao kutokana na sababu ya kwamba wameshindwa kutumia fursa zinazokuja mbele yao.Kwa mfano watu wengi wanalia leo hii kwasababu ya kuchezea fursa ya kupata elimu,kwa kuacha shule au kuacha kujituma katika masomo na hatimaye kushindwa mitihani au kuendekeza tabia zisizofaa na hatimaye kufukuzwa shule.Siku moja nikiwa sehemu moja jijini Arusha nikinyolewa,kinyozi aliyekuwa akininyoa alikuwa akilalamika sana kwa kudai kuwa anajuta kwa kukataa kusoma kutokana na ushawishi wa rafiki zake,wakaendekeza madawa ya kulevya. Lakini leo hii anatamani apate mtu atakayemwambia arudi shuleni, atafurahi sana na ataenda kujituma ili atimize ndoto zake.
Katika maisha zipo fursa nyingi zinazojitokeza katika maisha yetu,kama ,fursa za elimu,ajira na fursa za kutumia mali asili.
Katika nchi nyingi za Afrika ,kuna tatizo kubwa la serikali kushindwa kutumia fursa zilizopo ili kukuza kipato cha nchi kwa mfano katika taifa letu la Tanzania kuna tatizo kubwa la kushindwa kutumia fursa za mali asili kama madini,gesi na misitu.Ndiyo maana kipato cha nchi kimekuwa kidogo kiasi cha kwamba kuifanya serikali kutegemea kukopa kwenye benki za duniani au nchi za magharibi ili kupata pesa za bajeti.
Ukiangalia nchi nyingi za ulaya ziliweza kuendelea kwa kasi sana kutokana na kutumia fursa zilizokuwa mbele yao ,hasa ardhi kwa kilimo na ufugaji ,karne ya tano baada ya kuanguka kwa utawala wa Rumi.Walifanya kazi kwa bidii na kwa ushindani sana,tofauti na nchi zetu za Afrika ,leo hii ingawa watu ni maskini ,lakini hawajitumi kabisa katika kazi,uvivu na uzembe kazini ni mkumbwa.Wengi wetu tunapenda starehe  tu kuriko kazi utazania tuko peponi.
Lakini pia ,Wakati, Mwanadamu hupita katika nyakati za aina mbalimbalia kama inavyosema katika mhubiri 3:1-8 imeandikwa”Kwa kila kila jambo kuna majira yake,na wakati wa kila kusudi chini ya mbingu. Wakati wa kuzaliwa ,na wakati wa kufa;wakati wa kupanda,na wakati wa kung’oa yaliyopandwa;wakati wa kuua,na wakati wa kupoza;wakati wakubomoa na wakatiwa kujenga;wakati wa kulia na wakati wa kucheka;wakati wa kuomboleza na wakati wa kucheza…..wakati wa kutafuta na wakati wa kupoteza…”.
Kwa maana hiyo kuna wakati tumekuwa tukishindwa kutokana na sababu ya kuwa tupo katika wakati wa kushindwa. Inawezekana usinielewe vyema lakini ukikaa chini na kutafakari utaelewa,j iulize kwanini kuna wakati biashara yako ilichangangaya,ukafurahi sana ,lakini kwanini kuna wakati biashara yako ilikwama ukaanza kuhuzunika ,ukitaka kutafuta hata mchawi.Kwanini inafikia kipindi tunakwama katika mambo yetu tunayoyafanya?j ibu ni kwamba ,wakati.

      Zaidi ,Uvumilivu,Uvumilivu ni kitendo cha kuwa na subira au kustahimili ukinzani anaokumbana nao mtu.Kama nilivyosema hapo mwanzo kuwa, safari ya maisha ni safari inayochangayikana na changamoto,kwahiyo kama unataka kushinda lazima uzishinde changamoto.Ninaweza kusema kuwa “katika kila hatua moja unayotaka kuvuka ya kimaisha ili uingie hatua nyingine ya kimaisha unatakiwa kutegemea kukutana na changamoto”.
Unapovuka changamoto moja si kwamba ndio umekuwa salama unatakiwa kujua kuwa unapovuka changamoto moja kuingia hatua nyingine ya mafanikio,kuna changamoto nyingine katika hatua hiyo,kwa hiyo jiandae kuikabili.Kwa kifupi ,katika kila hatua ya maisha ipo changamoto yake.D.k Robert H.Schuller anatufundisha kuwa “wakati mgumu huwa haudumu bali watu wagumu au wenye nguvu ndio wanaodumu”.Kwa hiyo katika maisha changamoto utakutana nazo tu,lakini weka katika akili yako kuwa,hiyo changamoto haitadumu milele,ipo siku itazimika kama mshumaa.Walter Chrysler ,yeye anasema kuwa “siri ya mafanikio ni kuwa na shauku”.
Kwahiyo shauku yetu juu ya mafanikio inatakiwa kuzidi kuwa kubwa hata tunapokutana na mapingamizi ya kila namna.Hapo mwanzo tumeona kuwa Mtume Paulo alikutana na changamoto za kila  namna ,hata hivyo hakukata tamaa,hii inatokana na shauku yake ya kuieneza injili na kukamilisha huduma yake.Anasema kuwa aanendelea kukaza mwendo ,bila kuangalia ya  jana ,ila yeye anayachuchumilia yaliyo mbele(Wafilipi 3:12-13).
                 Na,Uthubutu, watu wengi wanashidwa kuvuka hatua moja ya mafaniko kwenda mbele kutokana na kujaza maneno ya “siwezi” ndani ya fikra zao.Hiii inatokana na hofu kubwa iliyojaa ndani ya mioyo yao.Watu wengi hutamani kujua ngazi zote wanazopaswa kuzipanda,lakini Mkuu Martin Luther King jr mwanafalsafa na mwanaharakati wa watu weusi amerika anasema kuwa “chukua hatua ya kwanza kwa imani,si lazima uone ngazi zote,chukua tu hatua ya kwanza”.Methali ya wachina inasema kuwa “safari ya maili elfu,huanza kwa hatua moja”.Kwahiyo lazima tushinde hofu inayotuzuia kuanza kwani bila kuanza hatuwezi kufika tunakotaka kufika. Rais wa kwanza wa Afrika Kusini kutokana na kuhangaika kwingi na hatimaye kushinda, alisema kuwa “Nimejifunza kwamba,ujasiri si kwamba haukuwa na hofu ndani yake,lakini shangwe ndani yake.Mtu shujaa si kwamba hana hofu ,bali ni Yule anayeishinda hofu”.
                Kwahiyo tunapotaka kuchukua hatua na mazingira yetu yanayotuzunguka yanatudokeza  kuwa, hatuwezi si kwamba tukate tamaa bali tutafute namna ya kuanza, hata kama ni kwa unyonge sana. Unapoanzisha kitu Fulani si lazima kiwe kimetimilika kwa asilimia mia,bali hicho ambacho hakijakamilika kinawezakuwa mtaji wakukupeleka katika kitu kilichokamilika.Mfano; unapotaka kuanzisha biashara Fulani ,si lazima uwe umekamilika kila kona,hiyo hiyo biashara nyonge inaweza kuwa mtaji wa kupata biashara kubwa.Mfano siku moja katika kipindi cha televisheni cha klauds fm kinachoitwa “siz kitaa” kuna bwana mmoja alisimulia namna ambavyo aliweza kupata mafanikio makubwa(kuwa na kiwanda),anasema kuwa alianza  kwa magunia matano tu ya mpunga,lakini baada ya jitihada kubwa ,sasa anakiwanda.
                Hivyo, katika kile ulichonacho unaweza kukitumia kuwa mtaji wa kukufanya ufike pale ambapo umekuwa ukiota.Watu wengi wameshindwa kufika katika mafanikio ambayo huyatamani kwasababu ya kushindwa kutumia mitaji waliyonayo kwa kuona kuwa ni midogo sana, mfano kujenga nyumba.
                Nakumbuka baba yangu mzazi alipokuwa akishauriwa kujenga nyumba, alikataa sana kwa kudai kuwa hana pesa, kwani yeye alitaka apate pesa ya kujenga moja kwa moja na si kidogo kidogo,kipindi hicho mimi nilikuwa bado mdogo sana.Lakini baada ya mama yangu kuamua kuanza ujenzi yeye kama yeye ,naye ameamua kuungana naye ,ingawa kidogo kidogo ,kutokana na kuwa na pesa kidogo,hata hivyo hivi sasa wako mbioni kumaliza ujenzi wote.
                Kama ulikuwa hufahamu ,nikudokeze siri hii,mara nyingi unapoanzisha jambo,ndipo hata akili ya namna ya kuliendeleza huja na hata milango hufunguka kwa ajiri ya kufanikisha jambo hilo.
 Rais marafu sana wa sasa duniani,nikimaanisha Baraka Obama alisema kuwa,”mabadiliko hayatakuja kama tukisubiri wakati mwingine au watu wengine,sisi ndio tuliosubiriwa kwa ajiri ya hayo,sisi ndio mabadiliko tunayoyatafuta”

                Nihitimishe kwa kusema kuwa kila mtu anao utajiri  wa mafanikio na nguvu,inategemea ni jinsi gani anautumia huo utajiri na kwa namna gani ili kupata matokeo chanya.
IMEANDALIWA NA Emmanuel & Jonathan.

                                     
Axact

Axact

Vestibulum bibendum felis sit amet dolor auctor molestie. In dignissim eget nibh id dapibus. Fusce et suscipit orci. Aliquam sit amet urna lorem. Duis eu imperdiet nunc, non imperdiet libero.

Post A Comment:

2 comments:

  1. Brother i'm much blessed with such a post so nive and very powerful doctrine emerging people to get onto their knees and pray. God bless you. Endelea usikate tamaa.

    JibuFuta
  2. Amen, mtu wa Mungu nitajitahidi zaidi kuweka machapisho kama hayo.

    JibuFuta