Jusus
Counselor Nicholaus
Kwanini tujifunze somo hili.
1.  Wengi hawajifahamu vizuri jinsi walivyo. 
2.  Mara nyingi tuonavyo wanadamu ni tofauti sana na Mungu aonavyo. 
3Shetani hutumia udhaifu wetu kutushinda hasa kwasababu hatujifahamu.
Tuanze kwa kuangalia Kwa undani jinsi binadamu alivyo.
Binadamu ni kiumbe kilichoubwa na Mungu ambacho kina nafsi, roho na mwili ila kubwa Zaidi ni utashi ulio ndani yake ambao unamtofautisha na viumbe wengine kama ng’ombe, mbuzi n.k
Utashi ni uwezo unaoongoza katika hali ya asili ya mwanadamu, uwezo wa kuamua, au wa kuchagua.
1 Wathesalonike 5:23 nafsi zenu na roho zenu na miili yenu mhifadhiwe mwe kamili, bila lawama, wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo.”
Ebu tupitie maeneo haya maeneo matatu (3)
      1. Mwili.
Neno“mwili” katika lugha ya Kiyunani ni “Soma” humaanisha “gamba la nje, au mavumbi ya ardhi yaliyofunika pumzi ya Mungu”. Mwili ni hili gamba la nje la mwanadamu lionekanalo. Mwili waweza kupendeza na pia waweza kuchukiza inategemea na sababu nyingi (Sababu za kiroho na za kimwili). Kiimani, kila aufuatae mwili anataka kufa. Siku zote Roho hupingana na mwili. Wagalatia 5:16-17 kwa hiyo nasema, mruhusuni Roho atawale maisha yenu na msitafute kutimiza tamaa za mwili. Kwa maana tamaa za mwili hushindana na Roho; na Roho hushindana na tamaa za mwili. Roho na mwili hupingana, na kwa sababu hiyo ninyi hamwezi kufanya yale mnayotaka.


2. Nafsi
Kwanza, tuzungumzie nafsi. Huenda unakumbuka kwamba mwanzoni Biblia iliandikwa katika Kiebrania na Kigiriki. Waandishi wa Biblia walitumia neno neʹphesh la Kiebrania au psy·kheʹ la Kigiriki walipoandika kuhusu nafsi. Maneno hayo mawili yanapatikana zaidi ya mara 800 katika Maandiko, na Tafsiri ya Ulimwengu Mpya huyatafsiri yote kuwa “nafsi.” Unapochunguza jinsi neno “nafsi” linavyotumiwa katika Biblia, utaona kwa wazi kwamba neno hilo humaanisha (1) watu, (2) wanyama, au (3) uhai wa mtu au mnyama.
Watu. “Katika siku za Noa. wachache, yaani, nafsi nane, walichukuliwa salama kupitia maji.” 1 Petro 3:20 watu wasiotii hapo zamani, uvumilivu wa Mungu ulipokuwa ukingoja, siku za Nuhu, safina ilipokuwa ikitengenezwa; ambamo ndani yake wachache, yaani, watu wanane, waliokoka kwa maji.
 Kwa wazi neno “nafsi” katika andiko hilo linamaanisha watu, yaani, Nuhu, mkewe, wanawe watatu, na wake zao. Andiko la Kutoka 16:16 lina maagizo kwa Waisraeli kuhusu kuokota mana. Waliambiwa: “Okoteni kiasi chake.  kulingana na hesabu ya nafsi ambazo kila mmoja wenu anazo katika hema lake.” Kwa hiyo, kiasi cha mana kilichookotwa kilitegemea kiasi cha watu katika kila familia. Maandiko yafuatayo ya Biblia yanaonyesha matumizi ya neno “nafsi” kumaanisha watu, Mwanzo 46:18 Hao ndio wana wa Zilpa, ambaye Labani alimpa Lea, binti yake, naye akamzalia Yakobo hao, nafsi kumi na sita.
Matendo 27:37 Na sisi tuliokuwa ndani ya merikebu tulipata watu mia mbili na sabini na sita.  ; na
Waruma 13:1 Kila mtu na aitii mamlaka iliyo kuu; kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu; na ile iliyopo umeamriwa na Mungu.
Wanyama. Tunasoma hivi katika masimulizi ya Biblia kuhusu uumbaji: “Mungu akaendelea kusema: ‘Maji na yajawe na nafsi hai na viumbe vinavyoruka viruke juu ya dunia kwenye uso wa anga la mbingu.’ Mungu akaendelea kusema: ‘Dunia na itokeze nafsi zilizo hai kulingana na aina zake, mnyama wa kufugwa na mnyama anayetambaa na mnyama-mwitu wa dunia kulingana na aina yake.’ Ikawa hivyo.”
Mwanzo 1:20, 24 Mungu akasema, Maji na yajawe kwa wingi na kitu kiendacho chenye uhai, na ndege waruke juu ya nchi katika anga la mbingu. Mungu akasema, Nchi na izae kiumbe hai kwa jinsi zake, mnyama wa kufugwa, nacho kitambaacho, na wanyama wa mwitu kwa jinsi zake; ikawa hivyo.  
Katika andiko hilo, samaki, wanyama wa kufugwa, na wanyama-mwitu wote wanaitwa kwa neno lilelile—“nafsi.” Ndege na wanyama wengine wanaitwa nafsi kwenye.
Mambo ya Walawi 11:46 Hii ndiyo sheria katika hao wanyama, na ndege, na kila kiumbe kilicho hai, kiendacho ndani ya maji, na kila kiumbe kitambaacho juu ya nchi.
Hesabu 31:28 kisha uwatoze hao watu wa vita waliotoka kwenda vitani sehemu kwa ajili ya Bwana; mmoja katika mia tano, katika wanadamu, na katika ng'ombe, na katika punda, na katika kondoo;.
Uhai wa mtu. Wakati mwingine neno “nafsi” humaanisha uhai wa mtu. Yehova alimwambia Musa: “Watu wote waliokuwa wakiiwinda nafsi yako wamekufa.”
Kutoka 4:19 Bwana akamwambia Musa huko Midiani, Haya, nenda, karudi Misri; kwa kuwa wale watu wote waliokutaka uhai wako wamekwisha kufa. Adui za Musa walikuwa wakiwinda nini? Walitaka kumuua Musa. Raheli alipokuwa akimzaa mwanawe Benyamini, ‘nafsi yake ilitoka (kwa sababu alikufa).’ Mwanzo 35:16-19 Wakasafiri kutoka Betheli, hata ukabaki mwendo wa kitambo tu kufika Efrathi, Raheli akashikwa na utungu wa kuzaa, na utungu wake ulikuwa mzito. Ikawa alipokuwa anashikwa sana na utungu, mzalisha akamwambia, Usiogope, maana sasa utamzaa mwanamume mwingine. Ikawa hapo katika kutoa roho yake, maana alikufa, akamwita jina lake Benoni, lakini babaye alimwita Benyamini. Akafa Raheli, akazikwa katika njia ya Efrathi, ndio Bethlehemu.  Wakati huo Raheli alipoteza uhai wake. Fikiria pia maneno ya Yesu: “Mimi ndiye mchungaji mwema; mchungaji mwema huitoa nafsi yake kwa ajili ya kondoo.”
Yohana 10:11Mimi ndimi mchungaji mwema. Mchungaji mwema huutoa uhai wake kwa ajili ya kondoo’.Yesu alitoa nafsi au uhai wake kwa ajili ya wanadamu. Katika maandiko hayo ya Biblia, ni wazi kwamba neno “nafsi” linamaanisha mtu. Utapata mifano mingine yenye maana hiyo ya neno “nafsi” kwenye 1 Wafalme 17:17-23;
Yohana 15:13 Hakuna aliye na upendo mwingi kuliko huu, wa mtu kuutoa uhai wake kwa ajili ya rafiki zake;
Matendo 20:10 Paulo akashuka, akamwangukia, akamkumbatia, akasema, Msifanye ghasia, maana uzima wake ungalimo ndani yake.
Ezekieli 18:4, 20 Tazama, roho zote ni mali yangu; kama vile roho ya baba ni mali yangu, ndivyo ilivyo roho ya mwana mali yangu; roho ile itendayo dhambi itakufa., Roho itendayo dhambi, ndiyo itakayokufa; mwana hatauchukua uovu wa baba yake, wala baba hatauchukua uovu wa mwanawe, haki yake mwenye haki itakuwa juu yake, na uovu wake mwenye uovu utakuwa juu yake. Kwa hiyo, katika Biblia mtu ambaye amekufa huitwa ‘nafsi iliyokufa.

      3.  Roho.
Hebu tuzungumzie jinsi Biblia inavyotumia neno “roho.” Watu fulani hufikiri kwamba “roho” ni neno lingine linalomaanisha “nafsi.” Lakini, si kweli. Biblia inaonyesha wazi kwamba “roho” na “nafsi” ni vitu viwili tofauti. Vinatofautianaje?
Waandishi wa Biblia walitumia neno la Kiebrania ruʹach au neno la Kigiriki, pneuʹma waliporejelea “roho.” Maandiko yenyewe yanaonyesha maana ya maneno hayo. Kwa mfano, andiko la Zaburi 104:29 Wewe wauficha uso wako, Wao wanafadhaika; Waiondoa pumzi yao, wanakufa, Na kuyarudia mavumbi yao, linasema: “Yehova ukiiondoa roho ruʹach yao, wanakata pumzi, na kurudi katika mavumbi yao.” Andiko la Yakobo 2:26 Maana kama vile mwili pasipo roho umekufa, vivyo hivyo na imani pasipo matendo imekufa.  linasema kwamba “mwili bila roho [pneuʹma] umekufa.” Katika andiko hilo “roho” inamaanisha kile ambacho huupa mwili uhai. Bila roho, mwili umekufa. Kwa hiyo, katika Biblia neno ruʹach halitafsiriwi tu “roho” bali pia “nguvu” au kani ya uhai. Kwa mfano, Mungu alisema hivi kuhusu Mafuriko ya siku ya Nuhu: “Ninaleta gharika ya maji duniani ili kuharibu kutoka chini ya mbingu wote wenye mwili walio na nguvu [ruʹach] za uhai ndani yao.” (Mwanzo 6:17; 7:15, 22-23) Hivyo, “roho” inarejelea nguvu isiyoonekana, inayotendesha viumbe vyote vilivyo hai.
 
Redio ambayo haina betri wala haijaunganishwa kwa umeme.


Redio ambayo imeunganishwa na betri.

Nafsi na roho hutofautiana. Mwili unahitaji roho kama vile redio inavyohitaji umeme ili kufanya kazi. Kwa mfano, unapotia betri katika redio na kuiwasha, nguvu zilizo katika betri huiwezesha redio kufanya kazi. Hata hivyo, redio haiwezi kufanya kazi bila betri. Hali kadhalika, redio ambayo imeondolewa kwenye umeme haiwezi kufanya kazi. Vivyo hivyo, roho ni nguvu ambayo hutendesha mwili wetu. Kama umeme, roho haiwezi kuhisi wala kufikiri. Ni nguvu isiyo na utu. Lakini bila roho au kani ya uhai, “tunakata pumzi na kurudi kwenye udongo,” kama mtunga-zaburi alivyosema.
Andiko la Mhubiri 12:7 Nayo mavumbi kuirudia nchi kama yalivyokuwa, Nayo roho kumrudia Mungu aliyeitoa. linasema hivi linapozungumzia kifo cha mwanadamu: “Mavumbi [mwili wake] huirudia nchi kama yalivyokuwa, nayo roho yenyewe humrudia Mungu wa kweli aliyeitoa.” roho au kani ya uhai inapoondoka mwilini, mwili hufa na kurudi ulipotoka, yaani, kwenye udongo. Vivyo hivyo, nguvu ya uhai hurudi ilipotoka, yaani, kwa Mungu.
Hiyo haimaanishi kwamba nguvu ya uhai huenda mbinguni kihalisi. Badala yake, inamaanisha kwamba mtu akifa, tumaini lolote la kuishi tena linamtegemea Mungu muumbaji. Ni kana kwamba uhai wake uko mikononi mwa Mungu. Ni kupitia nguvu za Mungu tu ndipo roho au nguvu ya uhai inaweza kurudishwa ili mtu aweze kuishi tena.
Inafariji kama nini kujua kwamba hivyo ndivyo Mungu atakavyofanya kwa wote wanaopumzika ndani ya “makaburi ya ukumbusho!” Yohana 5:28, 29 Msistaajabie maneno hayo; kwa maana saa yaja, ambayo watu wote waliomo makaburini wataisikia sauti yake. Nao watatoka; wale waliofanya mema kwa ufufuo wa uzima, na wale waliotenda mabaya kwa ufufuo wa hukumu. Wakati wa ufufuo, Yehova atamfanyizia mwili mpya yule anayelala katika kifo na kuuhuisha kwa kutia roho, au nguvu ya uhai ndani yake. Itakuwa siku ya shangwe sana.
Source: Online
 
MUHIMU: Kwahiyo tunapo kuzungumzia wewe tambua ni kiumbe wa tofauti sana, Zaidi ya wanyama wengine wote duniani.
Ukisoma ZABURI 139:13- 18 Maana Wewe ndiwe uliyeniumba mtima wangu, Uliniunga tumboni mwa mama yangu. Nitakushukuru kwa kuwa nimeumbwa Kwa jinsi ya ajabu ya kutisha. Matendo yako ni ya ajabu, Na nafsi yangu yajua sana,  Mifupa yangu haikusitirika kwako, Nilipoumbwa kwa siri, Nilipoungwa kwa ustadi pande za chini za nchi; Macho yako yaliniona kabla sijakamilika; Chuoni mwako ziliandikwa zote pia, Siku zilizoamriwa kabla hazijawa bado.Mungu, fikira zako zina thamani nyingi kwangu; Jinsi ilivyo kubwa jumla yake! Kama ningezihesabu ni nyingi kuliko mchanga; Niamkapo nikali pamoja nawe.
Usiruhusu kujidharau, tambua uko hapa duniani kutimiza makusudi ya Mungu.
Usiishi ilimradi siku ziende.
Mithali 23:7 Maana aonavyo nafsini mwake, ndivyo alivyo. Akuambia, Haya, kula, kunywa; Lakini moyo wake hauwi pamoja nawe.  
Wafilipi 4:8 Hatimaye, ndugu zangu, mambo yo yote yaliyo ya kweli, yo yote yaliyo ya staha, yo yote yaliyo ya haki, yo yote yaliyo safi, yo yote yenye kupendeza, yo yote yenye sifa njema; ukiwapo wema wo wote, ikiwapo sifa nzuri yo yote, yatafakarini hayo.
MUHIMU: kila mtu anajinsi anavyo ipatia akili maarifa mbalimbali.
Njia za kulisha Akili zetu.    
       1.  Kusiki. Mithali 1:8 Mwanangu, yasikilize mafundisho ya baba yako, Wala usiiache sheria ya mama yako.
       2.  Kuona. 2Samweli 11:2 Ikawa wakati wa jioni, Daudi akaondoka kitandani, akatembea juu ya dari ya jumba la mfalme; na alipokuwa juu ya dari aliona mwanamke anaoga; naye huyo mwanamke alikuwa mzuri sana, wa kupendeza macho.
Pointi zote hizi mbili hukufanya vile ulivyo sasa.

è Maranyingi tuonavyo wanadamu ni tofauti na Mungu aonavyo.
Binadamu wengi hudhani Mungu humlazimisha mtu machaguo lakini si sahihi.
Mungu ni wautaratibu sana, huweka kanuni ili zifutwe na Binadamu wenye utashi. ALAZIMISHI
Mfano: kubarikiwa baadhi ya wapendwa wengi huwa hawasomi vizuri katika kitabu cha
Kumb 28:1 Itakuwa utakaposikia sauti ya Bwana, Mungu wako, kwa bidii, kutunza kuyafanya maagizo yake yote nikuagizayo leo, ndipo Bwana, Mungu wako, atakapokutukuza juu ya mataifa yote ya duniani.
Mungu anaitaji uwajibike kwanza na afanye kitu kwako. Neno linasema itakuwa utakaposikia sauti ya Bwana, maana yake utakapo wajibika kwanza.
MUHIMU: Ivyo ulivyo ni kwasababu hujawajibika.
è Shetani hutumia elimu hii ili kutushinda.
Hasa katika eneo la mtizamo.
Luka 16:8 Yule bwana akamsifu wakili dhalimu kwa vile alivyotenda kwa busara; kwa kuwa wana wa ulimwengu huu katika kizazi chao wenyewe huwa na busara kuliko wana wa nuru.

Aina za Mtizamo.
1.      Mtizamo chanya
2.      Mtizamo hasi
Usikubali Mtizamo hasi UKUSHINDE.

Kati ya (12) watu kumi na mbili wawili (2) wawili tu ndo ambao walifanikiwa kuingia kanani, kilicho wafanikisha ni MTIZAMO CHANYA.
Kwahiyo Mtizamo hasi ni sumu mbaya sana.
MUHIMU: wewe binafsi unauwezo wa kubadilisha mtizamo hasi unapo amua.
NINI UKIFANYE
      Badilisha Vyanzo vya taarifa zako.
Katika maeneo mawili haya;- Unacho kisikia na unacho kiona si kila kitu lazima ukione na Unacho soma, si kila kitu unapaswa usome.
hakika ukifanikiwa hapo utakuwa zaidi ya Mtizamo wako, maana yake ni kwamba utakuwa na uwezo wa kujitawala hasa kwenye eneo la mtizamo.
 
Ni mimi ndugu yako Counselor Nicholaus Simon
Kiungo katika mwili wa kristo.
Kwa msaada na ushauri hasa kwenye eneo hilo la Maombi.
whatsap 0654-623 492. & Call: 0766-635 382
pataufahamu@gmail.com
Ubarikiwe sana na nakuomba nisaidie kushare kwa marafiki zako ili na wao wajifunze Neno la MUNGU.



                                                                                                                                  
Axact

Axact

Vestibulum bibendum felis sit amet dolor auctor molestie. In dignissim eget nibh id dapibus. Fusce et suscipit orci. Aliquam sit amet urna lorem. Duis eu imperdiet nunc, non imperdiet libero.

Post A Comment:

0 comments: