Mtu
wa Mungu tambua, Mungu alikuumba kwa kusudi. Yawezekana bado hujui lile kusudi,
na hilo ni sawa. Mungu alikuumba na ujuzi
na vipaji. anapo kutazama anaona
kuwezekana kwa mambo kusiko na ukomo. Mojawapo ya makusudi ya Mungu kwako, ni wewe
kuwa na uhusiano na Yesu. Uhusiano huo unafungua fursa nyingi maishani
mwako.
Mfano
Yesu akiwa mtoto, utaona Wazazi wake walimchukua mtoto ambaye ni Yesu, wakaenda naye Yerusalemu ili wamweke
mbele ya Bwana. Wakati huo huko Yerusalemu kulikuwa na mtu mmoja, mwema na mcha
Mungu, jina lake Simeoni, Roho Mtakatifu alikuwa amemhakikishia kwamba hatakufa
kabla ya kumwona kristo wa Bwana. Basi akiongozwa na Roho Mtakatifu, Simeoni
aliingia hekaluni; na wazazi wa Yesu walipomleta hakaluni mtoto wao, Simeoni
alimpokea mtoto Yesu mikononi mwake huku akimtukuza Mungu, akisema: sasa Bwana,
ametimiza ahadi yake, umruhusu mtumishi wako aende kwa amani. ‘’Kwa maana kwa
macho yangu nimeuona wokovu ulioleta. Ambao umeutayarisha uonekane na watu wote’’
Baba yake Yesu na mama yake walikuwa wakistaajabia maneno aliyosema simeoni juu
ya mtoto. Simeoni akawabarikia, akamwambia Maria mama yake, ‘‘Naye atakuwa
ishara itakayopingwa na watu; nawe mwenyewe, uchungu ulio kama upanga mkali
utauchoma moyo wako.’’
Jambo
kubwa ambao nimeona vyema nikushirikishe kuwa ,hakuna mtu anaye jua uwezo
uliopo ndani yako ila Mungu peke yake, yawezekana katika maisha kila unapo
fanya jambo watu huanza kukubeza na kusema huwezi fanikiwa, wayasemayo si
yakweli kwasababu hawajui uwezo uliopo ndani yako, ‘‘Tambua Nabii akubaliki
kwao’’ hata wewe si lahisi kukubalika katika jamii inayo kuzunguka ukianzia
katika familia, majilani na ndugu kiujumla wote hawa hawawezi kujua hatima ya
maisha yako. hata Yesu Katika jamii yake hawakumjua na ndomana walimsulubisha
kama wangemjua wasingeweza kumsulubisha.
Nikutie
moyo kuwa wewe ni mtu wa thamani sana katika hii dunia na hakuna mtu kama wewe
na hata kuwepo. kwahiyo jisikie vizuri kuwepo duniani, na utambue kuwa haupo
kwa bahati mbaya bali upo kutimiza agizo au kusudi la Mungu kwako katika maisha
yako.
Tukisoma
kitabu cha zaburi utamwona mtumishi wa Mungu Daudi akimshukuru Munu kwa jinsi
alivvyo .
Zaburi 139:14-18
‘’Nitakushukuru kwa kuwa nimeubwa kwa
jinsi ya ajabu ya kutisha. Matendo yako ni ya ajabu, Na nafsi yangu yajua sana,
Mifupa yangu haikusitirika kwako, Nilipoumbwa kwa siri, Nilipoungwa kwa ustadi
pande za chini za nchi; Macho yako yaliniona
kabla sijakamilika ; Chuoni mwako ziliandikwa zote pia, siku zilizo
amriwa kabla hazijawa bado. Mungu fikira zako zina thamani nyingi kwangu; Jinsi
ilivyo kubwa jumla yake. Kma
ningezihesabu ni nyingi kuliko mchanga;
Niamkapo nikali pamoja nawe’’.
Hakika
wewe ni wathani sana tena sana, Umeubwa kwa jinsi ya ajabu na kutisha na siku
zako za kuishi zote zimehesabiwambele za Mungu. Katika maisha yako jitahidi
sana kugundua una kipaji au huduma gani ambayo Mungu ameweka ndani
yako kwasababu kupitia hiyo, ndiyo yenye mafaniko yako.
MUHIMU:waliofanikiwa
sana ni wale wote wanaotumia vipawa ambavyo Mungu ameweka ndani yao.
NJIA 10 ZA KUJIANGALIA NA KUJIHISI
BORA.
1.
Mfahamu aliyekuumba.
2.
Lala vyakutosha. Kutolala vya kutosha husababisha siku zisizo na ufanisi an
kudhoofisha kinga ya mwili.
3.
Punguza kutumia sukari, ila kunywa maji sana.
4.
Furahia mafanikio yaw engine,usijiangalie wewemwenyewe tu.
5.
Jitunze vizuri. Uliubwa kwa mikono ya Mungu.
6.
Kuwa wewe halisi. Hakuna haja ya kuigiza.
7.
Usijijenge kwa kuwashusha wengine.
8.
Usikae tu, fanya kazi na maziezi.
9.
Vaa tabasamu.
10.
Tunza mwonekano wako, kwasababu ni wewe tu unayeweza.
Ni mimi ndugu yako; Mwl Nicholaus
Simon.
Kiungo katika mwili wa kristo.
Kwa msaada zaidi na ushauri.
Mawasiliano: +255 766 635 382
pataufahamu@gmail.com
Mawasiliano: +255 766 635 382
pataufahamu@gmail.com
Ubarikiwe sana Na nakuomba nisaidie
kuishare kwa marafiki zako ili na wao wajifunze Neno la Mungu.
Post A Comment:
0 comments: