Billy Graham enzi za uhai wake. |
Akitoa taarifa ya kuondoka kwa Baba yake, Mtoto wa Marehemu Billy Graham aitwaye Franklin Graham alisema hivi;
''
My father Billy Graham was once asked, “Where is Heaven?” He replied, “Heaven is where Jesus is and I am going to Him soon!” This morning, at the age of 99, he departed this world into eternal life in Heaven, prepared by the Lord Jesus Christ—the Savior of the world—whom he proclaimed for nearly 80 years. He will be missed by our family, his colleagues, faithful ministry partners, and, yes, many around the world. But what joy he has to be welcomed by God the Father, and be reunited with my mother in the presence of Jesus who speaks peace to eternal souls.
What about you? When you depart this world do you know with certainty where you will spend eternity? You can know this today. Jesus said, “For God so loved the world, that He gave His only begotten Son, that whosoever believeth in Him should not perish, but have everlasting life” (John 3:16). The One who comforts weary souls has given us this promise, “Let not your heart be troubled; you believe in God, believe also in Me … I go to prepare a place for you … I will come again and receive you to Myself; that where I am, there you may be also” (John 14:1-3).
'' Mwinjilisti huyo mtoto wa mkulima amefariki majira ya saa mbili asubuhi, sawa na majira ya saa kumi jioni kwa saa za Afrika Mashariki, nyumbani kwake, Montreat – Jumatano tarehe 21 Februari 2018.
Takwimu za huduma yake, zinaeleza kwamba Billy Graham ndiye Mhubiri pekee aliyewahi kuhubiria watu wengi zaidi tangu historia kuumbwa, akiwa amefikia zaidi ya watu milioni 210 kwenye nchi 185 duniani, aidha kwa njia ya runinga ama ana kwa ana.
Graham, raia wa Marekani, alieanzia kuhubiri jijini London Uingereza mnamo mwaka 1954, alikusanya maelfu ya watu kila mahali alipofanya mikutano ya hadhara ya injili.
Afrika Mashariki, Graham aliwahi kuhubiri Tanzania, miaka 55 iliyopita, wakati nchi iliitwa Tanganyika, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya Afrika miaka ya 1960. Takriban "watu 40,000 walihudhuria mkutano huo wa siku moja, tarehe Feb 28. 1960", kwa mujibu wa mtandao wa shirika lake.
Kwa zaidi ya miaka 60 inakadiriwa kuwa amehubiri kwa jumla ya watu milioni 210.
Alikuwa Mkristo akiwa na umri wa miaka 16 baada ya kumsikiliza mhubiri mmoja na kuanza huduma ya mahubiri mwaka 1939.
Graham alifahamika sana duniani kutokana na Uinjilisti alioufanya na mahubiri aliyotoa katika nchi mbalimbali duniani kuanzia miaka ya 1950.
Alianza huduma ya kuhubiri baada ya kutawazwa akiwa na miaka 21, mwaka 1939.
Familia yake imesema alifariki dunia akiwa nyumbani kwake katika jimbo la Carolina Kaskazini.
Graham anaelezwa kuhubiri kwa zaidi ya miaka 60, na kubadilisha mitizamo ya Mamia ya Mamilioni ya watu waliokubali ujumbe wake.
Mbali na mahubiri akiwa katika viwanja mbalimbali vya michezo na ukumbi, alitumia pia runinga na redio kuhubiri.
Amesuifiwa kama Mhubiri mwenye ushawishi mkubwa katika karne ya 20.
Wakati wote wa uhai wake, alikuwa na urafiki wa karibu na marais wote wa Marekani tangu rais Truman hadi Barrack Obama.
Rais Donald Trump kupitia ukurasa wake wa Twitter amesema, Graham alikuwa mtu wa kipekee na Wakiristo na watu wa dini nyingine, watamkosa sana.
Billy Graham ambaye ndiye mtoto mkubwa kuzaliwa akiwa na Baba yake mzazi na mama yake mzazi pamoja na ndugu zake wa damu katika Picha ya pamoja mwaka 1962 |
Mnamo mwaka 1950, aliunda Umoja wa Wahubiri wa Billy Graham katika juhudi za kusambaza neno la MUNGU kupitia kile kilichokuja kuwa maarufu hivi leo kama “crusades”, mahubiri ya mfululizo ambayo hufanyika katika viwanja mbalimbali.
Graham aliendesha mahubiri haya katika mabara yote isipokuwa Antarctica, akihubiri yeye mwenyewe kupitia matangazo ya satellite. Alihubiri katika mataifa ya Soviet kabla ya kuanguka kwa ukomunisti.
Na katika msimu wa baridi mwaka 1994, Billy Graham alitoa mahubiri huko China na Korea Kaskazini, ambako alikutana na viongozi wa kisiasa na kidini katika nchi hizo.
Kutokana na safari zake alizofanya katika mataifa mbali mbali ulimwenguni, mhubiri huyu mashuhuri wa Marekani alithibitisha kuwa Ukristo sio tu dini ya nchi za Magharibi.
alisema katika moja ya mahubiri yake kwamba
“Ukristo ni wenye nguvu Afrika na Amerika ya kati na Asia kuliko ilivyo nchi za Ulaya, kwa hatua kubwa. Huko Ulaya , bado unaitwa Ukristo, lakini hauna ukakamavu na nguvu kubwa. Na nilikuwa Rome na kufanya mazungumzo na Papa juu ya suala hili na nafikiri mtakubaliana na hilo – kwamba maisha halisi ya Ukristo hivi sasa yako kule tunakokuita ulimwengu wa tatu,” alisema .
Graham, ambaye kabla hajaanza kazi ya MUNGU alifanya kazi kama afisa wa mauzo, aliendelea na kuwa mmoja wa wahubiri wenye ushawishi mkubwa miongoni mwa watu wa dini zote huku akiwashauri marais na viongozi wengine wengi duniani juu ya imani ya Kikristo.
Mwaka 1949, alipata umaarufu wakati alihubiri kwa wiki nane kwenye hema kubwa huko Los Angeles.
Wakati wa harakati za mashirika ya kupigania haki za binadamu, Graham aliibuka kuwa mkasoaji mkubwa wa ubaguzi wa rangi nchini Marekani.
Mara kadhaa muinjilisti huyo aliyemrithisha huduma mwanaye aitwaye Franklin Graham, amekuwa akinukuliwa akisema, “Nyumbani kwangu ni mbinguni, hapa nilipo ni mpita njia tu.”
Ni muhubiri aliyeepuka kashfa mbalimbali zilizowazonga wahubiri wengi waliotumia runinga kusambaza injili.
Mkutano wake wa mwisho wa hadhara ulikuwa mwaka 2005 jijini New York Marekani akiwa na umri wa miaka 86.
Rais Donald Trump amemuelezea Graham kama "mwanaume wa kipekee".
Akiandika kwenye ukurasa wake wa Twitter, Trump amesema "Mhubiri maarufu wa Injili Billy Graham. Hakuna aliyekuwa kama yeye! Atakumbukwa na Wakristo na watu wa dini zote. Mwanamume wa kipekee kabisa."
Shujaa amemaliza kazi yake duniani, na sasa ni uzima wa milele katika KRISTO YESU.
MUNGU alimtoa na sasa amemtwaa hivyo daima jina la BWANA lihimidiwe.
Billy Graham na mkewe Ruth Graham katika mkutano wa injili New York for mwaka 1957. |
Siku za karibuni nitakuletea mambo kadhaa usiyoyajua kutoka katika kazi ya MUNGU aliyoifanya shujaa huyu hata upate kitu chema cha kujifunza.
Ubarikiwe.
Post A Comment:
0 comments: