Tutaangalia katika maeneo matatu.(a) Familia (b) Kanisa (c) Nchi
Wajibu ni hali ya kuwajibika juu ya jambo fulani kwa wakati
sahihi. Yoshua 1:1-9
Ukiangalia yote haya asemayo Bwana na Mtumishi wake, Yoshua ambaye
kwa sasa ni wewe.
Mstari wa 5.''Hapatakuwa na mtu yeyote atakayeweza
kusimama mbele yako siku zote za maisha yako; kama nilivyo kuwa na Musa, ndivyo
ndivyo nitakavyo kuwa na pamoja na wewe; sitakupungukia wala sitakuacha.''
Tambua wewe ni mtu wa thamani na pekee sana, katika hii dunia. Hakuna kama
wewe, Mungu alivyo kuumba amekuumba kwa kipekee na kukuweka vitu ndani yako ambavyo vitakusaidia kufanikiwa katika hii dunia. Zaburi 139:14-18
Mstari wa 6.''Uwe hodari na moyo wa ushujaa, maana ni wewe
utakayewarithisha watu hawa nchi hii niliyowaapia baba zao yakwamba nitawapa.'' Wewe ni hodari, hakuna binadamu yeyote
katika hii dunia. anayeweza kukukosoa kwa kusema, huwezi kufanya jambo fulani
kwasababu yeye hajakuumba na ajui uwezo uliopo ndani
yako.
Tambua ulivyo umbwa Bwana alikuchagua kati ya mbegu za kiume
milioni tano, Mungu amekuchagua wewe. 1kor 2:7-8,11.
Hakuna mtu anayeweza kumjua mwenzake zaidi ya Mungu peke yake.
Mstari wa 7 ''Uwe hodari tu na ushujaa mwingi, uangalie kutenda
sawasawa na sheria yote aliyokuamuru Musa mtumishi wangu;usiiache, kwenda
mkono, au wa kushoto, upate kufanikiwa sana kila uendako'' Unapo
wajibika sawasawa na mapenzi ya Mungu hakika LAZIMA UFANIKIWE.
UKIWA KAMA KIJANA WAJIBU WAKO NI NINI NDANI YA FAMILIA.
Mambo ya kuangalia ili uwajibike sawasawa na mapenzi ya Mungu.
(i) Ijue hali ya Familia yako. –maskini au tajiri, kabila
lenu katika upande wa mila na desturi.
(ii) Ijua haiba ya wazazi wako na ndugu zako. Kama ni
sanguine, melancholic, flegimatic na choleric.
(iii) Tambua mila na desturi za jamii inayo wazunguka.
mafamo, baadhi ya makabila ni wakali sana, pia makabila mengine ni waongeaji.
Ukiyatambua haya naamini utajua ni jinsi gani ya kuishi vyema bila
makwazo yeyote na utapata ufahamu wa kuwa msaada mkubwa wa kuwasaidia
ndugu zako. Mfano: Yusuph aliwatambua ndugu zake na baadaye
aliwasaidia. Mwanzo 37:1-5
MUHIMU: Hata kama utafanikiwa heshimu wazazi wako na ndugu zako.
''Waheshimu baba yako na mama yako; amri hii ndiyo amri ya kwanza
yenye ahadi.'' Waefeso 6:2
Usilipe ubaya wowote anaye lipa ubaya ni Mungu mwenyewe,wakati
wote kuwa mtu wa kusamehe. ,1petr 2:17, kut 20:12, mith 13:1.
Jambo la muhimu la kujua,jamii yako hukudharau kwasababu kugundua
kilichopo ndani yako ni vigumu mno. ''Wakachukizwa naye. Yesu akawaambia , nabii hakosi kupata heshima, isipo kuwa katika nchi yake, na nyumbani mwake
mwenyewe.'' Mathayo 13:57
UKIWA KAMA KIJANA WAJIBU WAKO NI NINI NDANI YA KANISA.
Kijana katika Biblia takatifu ameelezwa kama, ''Mtu awaye yote
asiudharau ujana wako, bali uwe kielelezo kwao waaminio, katika usemi na
mwenendo, na katika upendo na imani na usafi.''1Tim 4:12
Kama kijana usijidharau wewe ni wathamani
sana jikubali mwenyewe.
''Jitahidi kujionyesha kuwa umekubaliwa na Mungu,
mtenda kazi asiye na sababu ya kutahayari, ukitumia kwa halali neno la kweli.'' 2Tim 2:15
Tambua kwamba vijana ndio walio leta mapinduzi makubwa katika kanisa la kwanza.
Mambo ya Muhimu ya kuyafahamu
(i) Jikubali wewe binafsi. Usijizalau na kuona huwezi
kutumika. 2Tim 2:15 -16
Wewe ni mzuri kwasababu Mungu ndiye aliye kuumba hivyo
ulivyo.
Zingatia: kila asubuhi jiwekee ratiba ya kumshukuru Mungu kwa
jinsi hivyo ulivyo.
(ii) Acha mizaa kabisa.
''Heri mtu yule asiyekwenda katika shari la wasio haki;
Wala hakusimama katika njia ya wakosaji; Wala hakuketi barazani pa wenye
mizaha.'' Zaburi 1:1.
MUHIMU: Acha mizaa na jinsia tofauti kwasababu jinsia
tofauti ni hasi na chanya pale zinapo kutana lazima matokeo yatokee.''Wala
msimpe Ibilisi nafasi.'' Efe 4:27
ZINGATIA: unapo luhusu mizaa katika maisha yako, shetani hupata nafasi ndani ya moyo wako.
''Wala si ajabu, Maana shetani mwenyewe hujigeuza awe mfano wa malaika wa nuru.''2kor 11:14
(iii) jigundue uwezo wako binafsi katika mwili wa kristo.
Katika huduma tano zilizopo ndani ya kanisa jitahidi kujua
upo kwenye nafasi gani.
Je, wewe ni mchungaji, mwalimu, mwinjilisti, mtume na nabii. Pia
jambo lingine la msingi la kifahamu ni kwamba kuna karama za Roho Mtakatifu
zipo Tisa. 1kor 12:4
Nazo ni (i) KARAMA ZA UFUNUO. Ambapo ndani yake zinapatikana hizi tatu ;- Kunena, kutafsiri na Unabii.
(ii) KARAMA ZA
UFUNUO. Ambapo ndani yake zinapatikana hizi tatu ;- maarifa, neno la
heekima na kupambanua roho.
(iii) KARAMA ZA NGUVU.Ambapo ndani yake zinapatikana hizi tatu ;- Imani ,Uponyaji na
matendo ya miujiza.
Baada ya kupata ufahamu ju ya karama na huduma,
tambua karama ni kifaa kinachowezesha huduma ikue .
MUHIMU: usibahatishe huduma
yako.
Kwahiyo kutimiza wajibu wako ndani ya
kanisa Lazima utembee katika kusudi la Mungu.''Kwa kadiri ya
kusudi la milele alilolikusudia katika kristo Yesu Bwanawetu.'' Efe
3:11
Vitu vya kuzingatia unapo chagua mahali
pa kumwabudu Mungu ukiwa ugenini.
- Ondoa
mtizamo mgando wa kimadhehebu, tambua kanisa la kristo wote ni mwili
mmoja.
- Omba
kwa Mungu akusaidie kukuongoza mahali sahihi.
UKIWA KAMA KIJANA WAJIBU WAKO NI NINI NDANI YA
NCHI.
Tambua kwanza kuwa kanisa ndilo linalo ongoza nchi, kanisa
likiharibika nchi nayo imeharibika.
Mungu anapo angalia nchi huangalia kanisa kwahiyo kama tulivyo
angalia kama kijana, una umuhimu mkubwa sana ndani ya kanisa na nchi kiujumla.
Wajibu wako ni nini.
(i)bidii katika masomo. Mith 4:13
(ii) bidii katika shughuli zako zote mfano,
mashambani,maofisini, hii itakuwezesha kuwajibika vizuri katika Taifa .1Samweli
13:1,9-11.
MAMBO MAWILI YA MUHIMU KWA KIJANA
Kama kijana ombea Taifa
kwa mzigo na ufanye kazi kwa nguvu, akili na moyo wako wote.
Kama kijana kila mwisho
wa mwaka laziam ufanye tathimini ya mipango yako uliyo weka unapo anza mwaka.
Ni mimi ndugu yako; Mwl Nicholaus
Simon.
Kiungo katika mwili wa kristo.
Kwa msaada zaidi na ushauri.
Mawasiliano: +255 766 635 382
pataufahamu@gmail.com
Mawasiliano: +255 766 635 382
pataufahamu@gmail.com
Ubarikiwe sana Na nakuomba nisaidie
kuishare kwa marafiki zako ili na wao wajifunze Neno la Mungu.
Post A Comment:
0 comments: