Maana kwa ufupi. Mambo ya Rohoni na  Mwilini? 
Mambo ya kiroho ni mambo yote yanayofanyika pasipo kuonekana  na macho ya kimwili. 
Mambo ya kimwili ni mambo yanayoonekana na macho ya kimwili. mfano, tunaona Nyumba ,magari.  
‘‘Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.’’Waefeso 6:12
Tambua kwamba ulimwengu wa roho ndio unao jenga ulimwengu wa kimwili ,Kushinda au kushindwa huanzia rohoni na baadaye kuna dhihirika kwa uhalisia wa nj’e.
    Mambo waliyo agizwa kupeleleza na kuleta kutoka kaanani.
   Hesabu 13:17
1.     Nchi ya namna gani ?
2.     watu wanao kaa humo ?
3.     Njema  au mbaya ?
4.     wana kaa kwenye matuo au ngome ?
5.     Nchi ni Nono au ina njaa ?
6.     Inamisitu au haina ?
7.     walete Matunda .

Rejea mstari wa Hesabu 14:24-30, Unaona mitizamo ya wapelelezi baada ya kurudisha habari ikiwa inatofautiana, wapo Ambao mitizamo yao ilikuwa CHANYA na wengine mitizamo yao ilikuwa HASI.
Mtizamo chanya Hesabu 14:5-10  huu ni mtizamo mzuri ambao huangalia ushindi tu. 
CHANGAMOTO MOJA INAYO WEZA SABABISHA MAMBO YA KIROHO YASIWE DHAHIRI.
Mtizamo Hasi. Hesabu 14:1-4. Swali la kujiuliza kitu gani kiliwaliza wanaisraeli? Je , waliona kweli?   
     MADHARA YATOKANAYO NA MTIZAMO HASI 
(a)Bwana uchukizwa sana  na hughailisha mambo yote aliyo yakusudia kwako.
     Hesabu 14:10-20
(b) Bwana huruhusu Adhabu. 
    Hesabu 14:21, 37-38
                                           JAMBO LA KUFANYA  
Tunapo enda kumaliza mwaka na kuingia mwaka mwingine jitahidi ,kuandaa mipango yako kibinafsi, huku ukijaribu kupeleleza moyoni mwako (kupeleza moyoni mwako). ni kuombea mipango yako kwasababu kupitia kuombea hapo unafanya kiroho na baadaye mwaka ujao yote uliyo ombea yatadhihiika dhahiri.
AMEN 
Ni mimi ndugu yako; Mwl Nicholaus Simon.
Kiungo katika mwili wa kristo.
Kwa msaada zaidi na ushauri.
Mawasiliano: +255 766 635 382
pataufahamu@gmail.com
 

Ubarikiwe sana Na nakuomba nisaidie kuishare kwa marafiki zako ili na wao wajifunze Neno la Mungu.




Axact

Axact

Vestibulum bibendum felis sit amet dolor auctor molestie. In dignissim eget nibh id dapibus. Fusce et suscipit orci. Aliquam sit amet urna lorem. Duis eu imperdiet nunc, non imperdiet libero.

Post A Comment:

0 comments: