Tutaenda kuangalia maana fupi ya maombi na matokeo ambayo
mwamini huyapata kupitia maombi.
(i) kupitia maombi mwamini anakuwa na uwezo wa kusoma Neno.
(ii) Mahusiano ya karibu na Mungu hujengwa.
(iii) Majukumu ya ki-Mungu uyapokea.
(iv) Humwezesha mwamini kushinda majaribu.
Maombi ni mawasiliano kati ya mwanadamu na Mungu
au ni mazungumzo
Ambayo hufanyika baina ya
mwanadamu na Mungu.
Yeremia 33:3”Niite, nami
nitakuitikia, nami nitakuonyesha mambo makubwa, magumu usiyoyajua’’
Tambua Mungu ni roho.
MWANADAMU---------{MAOMBI}----------MUNGU
MUHIMU: Tambua mawasiliano
yanayo fanyika baina ya mwanadamu na Mungu ni tofauti sana na mawasiliano ya
kawaida kwasababu.
(i) Mawasiliano ya kawaida hutumia mirango
mitano ya fahamu.
(ii) Mawasiliano ya kawaida unapo wasiliana na mwingine na yeye
anapo jibu hapo ndipo mawasiliano huanza. Unapo
mwomba Mungu haya ni Mawasiliano ya
Upande mmoja kwa wakati huo
wa kupeleka hoja zetu. Isaya 41:21”Haya,leteni maneno
yenu,asema Bwana; toeni Hoja zenu zenye Nguvu, asema mfalme wa Yakobo.”
Mwamini huweza kutambua
kama mawasiliano baina yake na Mungu kama
yapo vizuri pale tu Amani moyoni Inapo tawala wakati wa kufanya maombi. Pale
mwombaji anapo omba na Moyoni mwake anakosa Amani hapo tambua kuna mambo mawili
ya Msingi,yawezekana hayupo safi au yupo safi lakini shetani huweza kumsonga
mwombaji na kumshuhudia uongo na kusababisha amani kutotawala vizuri. Mwombaji huweza pokea majibu ya maombi
yake kupitia;-
mawazo
mapya, Unabii, Ndoto, Neno,Yohana 1:1,15:7,17:17, Zaburi 119:105.
FAIDA /UMUHIMU UNAOPATIKANA KUPITIA MAOMBI
(i) Humwezesha mwamini kusoma Neno.kupitia maombi mwamini huweza kupata nguvu ya kusoma
Neno la Mungu kwasababu Mungu hutumia
Neno kutujibu mahitaji yetu tuliyo yapeleka kwake.kupitia Neno la Mungu,huweza
kutuonya,kutufariji na kutuelekeza.Faida kubwa tunayo pata ni kwamba Roho
Mtakatifu ndiye Anaye tusaidia kulijua Neno
baada ya kumwomba Mungu.1Timotheo 2:1
Ebrania 4:12”Maana Neno la Mungu li
hai,tena lina Nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo
na mafuta yaliyo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudu ya moyo.’’ Shetani huweka vizuizi vikubwa sana kwa
waamini katika swala la kupata muda wa maombi na kusoma Neno. Pia yapo mahusiano makubwa sana
kati ya vitu hivi viwili Maombi na Neno kwasababu Maombi bila Neno hayana nguvu
pia kusoma Neno bila ya kumwomba Mungu akufundishe hakuna faida pia. Neno ni
chakura cha mwamini pasipo Neno
hakuna kukua kwasababu mtu
wa ndani hudumaa anapo kosa Neno/chakula na hupelekea kufa.
(ii) Mahusiano ya
karibu na Mungu hujengwa.Mawasiliano hukuza Mahusiano kwa hiyo kupitia maombi
mahusino makubwa huzaliwa baina ya Mwamini na Mungu .mfano katika hali ya
kawaida kabisa Inajulikana
pale ambapo mahusiano ya
watu yanapo kuwa mazuri zaidi ndipo watu hawa huwa karibu sana .lakini pale
ambapo hakuna maweasiliano pia mahusiano huwa mabaya ambapo watu hawa hawawezi
kujuana vizuri kwa undani ukiringanisha na wenye ukaribu.Ndivyo hivyo kwa Mungu
,Mahusiano huwa makubwa sana
hata mwamini kutambua siri
nzito kutoka kwa Bwana ni pale tu ambapo mahusiano yanapo kuwa makubwa.Mungu
huachilia siri/maelekezo mengi kwa Yule mwamini Ambaye yuko naye karibu
sana.soma 1samweli 3:10,Daniel 9:21.
(iii) Majukumu ya k i-Mungu huyapokea. Ipo siri kubwa
sana juu ya mawasiliano[maombi] kati
ya mwamini na Mungu, kupitia Maombi Mungu huachilia majukumu yakufanya kwa mwamini.
mfano ; Samweli , Musa ,Yakobo. Yakobo-kupitia ndoto Mungu aliachilia
majukumu mengi kwa mtumishi wake huyu. Ibrahimu, Mwanzo 22:1-4,
Mungu alimpa majukumu ya
kufanya Ibrahimu pale alipo kuwa na mawasiliano mazuri naye.hata wewe Mtu wa
Mungu tegemea kupewa majukumu mengi zaidi endapo tu utadumisha na kukuza
mahusiano na Mungu. Musa, kutoka 3:4-10.mtumishi wa Mungu huyu
alipo kuwa na mahusiano mazuri na Mungu kupitia Maombi Mungu alimweshimu na
kumpatia majukumu ya kufanya.rejea mstari wa 10;Mungu alimpa majukumu mtumishi wake Musa baada ya kukubali
na kuonesha nia ya kweli
katika upande wa mawasiliano.Note;Mjukumu wakati wote mtu huweza kupewa kulingana na umri
alio nao.hasa katika uwezo wa kiakili.swali je,anaweza kutunza siri na
kumbukumbu vizuri,vivyo hivyo katika Mambo ya Ki-Mungu,Mungu huachilia majukumu kwa waamini kulingana na kiwango
cha kiroho cha mtu husika.Waefeso 3:20. Kiwango chako cha nguvu
za Mungu zilizopo ndani yako huwa sababisho kwa Mun gu kuachilia mambo makubwa
au madogo.Mwanzo 18:16-17.
(iv) Humwezesha Mwamini
kushinda Majaribu.
kupitia mahusiano mazuri
na Mungu kwa njia ya maombi Mungu
huweza kumwonekania mwamini kwa namna ya tofauti sana pasipo hata yeye kujua. Zaburi 50:15.‘‘Ukaniite siku ya mateso,nitakuokoa, na wewe utanitukuza’’.
Bwana mwenyewe
anathibitisha kuwa kupitia
mawasiliano(maombi)utamwita nay eye atakuokoa katika hilo jambo ambalo utakuwa
unapitia.
Ayubu 22:27-30; Utawasiliana na Mungu
na yeye atakusikia,kupitia maombi mipango
na ratiba Bwana ataionesha hata kama changamoto zitakuja lakini Bwana atakuvusha na kukuinua tena katika kusudi lako.
Zaburi 22:23-24. Bwana anapenda
mawasiliano yetu na yeye yawe katika uhusiano
ulio safi kabisa na hakika Mungu lazima Afanye.
MUHIMU: Kama ilivyo katika
maisha ya kawaida watu
wawili wanapo kuwa karibu ndipo huanza kujuana kwa undani sana mfano,mambo ya
kufahamu,kimahusiano na kimichezo.
kama hawana mahusiano usitegemee kujuana kwa undani zaidi but juu juu
tu.kiroho lazima ifike sehemu
kama kanisa la kristo tuamke na kumtambua Mungu wetu kwa namna hii.Mungu anahitaji
uhusiano mkubwa na sisi ili aweze kuachilia majukumu mbalimbali ndani yetu ya
kufanya.
Pia unaweza soma machapisho
zaidi na zaidi kwa faida ya kukuza imani yako :- fungua hapa.
Ni mimi ndugu yako; Mwl Nicholaus
Simon.
Kiungo katika mwili wa kristo.
Kwa msaada zaidi na ushauri.
Mawasiliano: +255 766 635 382
pataufahamu@gmail.com
Mawasiliano: +255 766 635 382
pataufahamu@gmail.com
Ubarikiwe sana Na nakuomba nisaidie
kuishare kwa marafiki zako ili na wao wajifunze Neno la Mungu.
Post A Comment:
0 comments: