Kukua kiroho ni tendo la taratibu linalotokea hatua kwa hatua ambapo
huchukua maisha ya mwamini yote akiwa hapa duniani. Si tendo la mara moja au
linalotokea lenyewe tu. kwa kawaida mwili unahitaji chakurabora,mazoezi ili uweze kukua vizuri
pia Roho zetu zinahitaji Neno la Mungu ,maombi pamoja na kumtumikia
Mungu kwa
namna mbalimbali ili iweze kukua vizuri. Mfano: kwa hali ya kawaida
wewe ukiwa kama Mzazi unapokuwa na Mtoto ambaye hakui- kiukweli haifulahishi
kabisa
Mungu [mzazi] Baba
&Mama
Siri
Mtoto wa kiroho Mtoto
wa kimwili
Siri ni ufahamu uliofichika usiojulikana kwa Mtu
kabla ya kufahamishwa lakini akisha fahamishwa unakuwa sio siri.
Mzazi wa kibinadamu haweza kumwambia mtoto wake baadhi ya Mambo
kulingana na uwezo wa akili pamoja na umri .
Wakati mwingine mtoto huweza kumuuliza Mzazi
wake baadhi ya mambo na Mzazi akashindwa kumjibu
mtoto moja kwa moja kwasababu Uwezo wa yule mtoto bado ni
mdogo.Lakini kadri anavyozidi kukua huyo mtoto ndivyo atakavyozidi kujua mambo
mengi sana.
Mungu wetu kwetu sisi waamini tukiwa kama watoto wake zipo siri ambazo
hawezi kumpa mwamini asiyekua kiroho kwa sababu siri nyingine
huwa kubwa kuzidi uwezo wake.kwahiyo kadri tunavyozidi kukua kiroho ndivyo
tunavyozidi kujua siri nyingi katika mambo ya Mungu. 1Wakorintho 14:20
ZINGATIA: Lengo la Mungu kwa
maisha yako ya hapa duniani siyo upate faraja bali ni kukuza tabia ,anapenda ukue
kiroho na uwe kama kristo. Waefeso 4:13
Kukua kiroho siyo tendo linalotokea tu ,bali huitajimaamuzi kutoka kwa mtu
binafsi .
MAMBO YANAYOSABABISHA KUTOKUKUA KIROHO.
1. Kukosa Ushirika.-kutokujumuika na waamini wengine katika ibada.
Waebrania 10:25, Matendo 2:42, 44.
Matokeo kwa mwamini anayekosa ushirika
- Uvivu
wa kufanya maombi.
- Uvivu
wa kusoma Neno.
- Kukosa
nguvu ya kuhubiri injili.
- Kukosa
huakika wa wokovu.
2. Kuvunjwa Moyo ni hali ya kukatishwa tamaa
Mfano: wazazi, Marafiki,
na Viongozi.
Mithali
1:10-16, 1Wakorintho5;9-12
3. Ujuaji/kujikinai-kutoitaji msaada wowote wa kiroho. Mithali
16:18-19
SABABU ZINAZOFANYA MWAMINI AKUE KIROHO.
-
Uamuzi binafsi wa kuitaji kukua .
Ni hatua ya mwamini yeye mwenyewe kuamua wala siyo kulazimishwa na
mtu,lazima nia yake ibadilike iwaze kukua kiroho. Waefeso4:23,
wafilipi2:5
-
Bidii/juhudi-niuamuzi wa kumtafuta Mungu kwa nguvu zote, akili pamoja na
moyo wote.
Mithali 8:17, 13:4, Tito 2:14
- Kudumu
katika kukua-ni tendo la kukaa moja kwa moja katika kukua.
Pia unaweza Tembelea website zenye mafundisho ya Neno la Mungu kwa kupata kujifunza
zaidi:- mwalusambo
Ni mimi ndugu yako; Mwl Nicholaus
Simon.
Kwa msaada zaidi na ushauri.
Mawasiliano: +255 766 635 382
pataufahamu@gmail.com
pataufahamu@gmail.com
Ubarikiwe sana Na nakuomba nisaidie
kuishare kwa marafiki zako ili na wao wajifunze Neno la Mungu.
Post A Comment:
0 comments: