Maombi ni mawasiliano kati ya mwanadamu na
Mungu hii ni tafsiri ya kiroho. Isaya 43:26 ‘‘unikumbushe,na tuhojiane; eleza mambo
yako, upate kupewa haki yako’’.
Maandiko matakatifu yanayo onyesha Maombi.
Waefeso 6:18, 2Mambo yanyakt 7:14,
Zabur 17:1.
Kama
ilivyo katika maisha ya kawaida Maombi huwa yana fanywa na muhitaji kwa mtu
Ambaye anachokitu ambacho muhitaji aweza kukipata kupitia maombi hayo na hapo Mawasiliano lazima yatokee kwa sababu pale tu muhusika anapo jibu Mawasiliano
huanza baina ya pande hizo mbili. mfano, katika Maandishi; mtu anapo tuma barua
kuomba kazi asipojibiwa Mawasiliano huishia hapo bali akitumiwa Barua
Mawasiliano huweza kuendelea.,kuongea papo kwa papo; mtu akikuongelesha na wewe
usimjibu upo uwezekano mkubwa wa mtu huyo kutokukupa salamu siku nyingine
lakini kama ukipokea salamu yake mawasiliano huanza kwa ukaribu mkubwa.
Maombi ambayo tunajifunza na tunahitaji kuyajua ni ya kiroho. Mungu wetu tangu
Asili alipo Muumba Mwanadamu alihitaji ukaribu mkubwa wa kuwa na mawasiliano
naye.
Mwanzo 3:8-10. ‘‘kisha wakasikia sauti ya BWANA Mungu, akitembea bustanini wakati
wajua kupunga ;Adamu na mkewe wakajificha kati ya miti ya bustani, BWANA Mungu
asiwaone. 9; BWANA Mungu akamwita adamu ,akamwambia, uko wapi.10; Akasema ,
nalisikia sauti yako bustanini ,nikaogopa kwa kuwa mimi ni uchi; nikajificha.
’’ Adamu anasema Angalia mstari wa 10. Alisikia sauti ya Mungu kwa hiyo hii
ilikuwa destruri yake Mungu kudhuru wakati wa jua kupunga kuwasiliana na
wanadamu hawa.
Kwahiyo
tangu Asili Mawasiliano yalikuwa yanatumika baina ya Wanadamu na Mungu, pia
kupitia Mawasiliano, Mahusiano makubwa yalijengwa kwa ukaribu sana.
Tuangalie mifano ya
watumishi wa Mungu baadhi Ambao walifanya mawasiliano na Mungu kwanjia ya
maombi.
(i) MUSA, kutoka 3:4-14,7:1,40:1 Mawasiliano yalifanyika kati ya Mungu
na Musa kwa muda mrefu ,kupitia mawasiliano haya Mungu alimpa
maagizo mengi mtumishi wake Musa.
(ii)
SAMWELI. 1Samweli 3:10 Samweli kabla hajaelewa
jinsi ya kujibu Mungu hakuweza kuwasiliana naye lakini alipo julishwa na mzee
Eli, jinsi ya kujibu ndipo. 1samweli 3:11 Mungu
akaanza kusema na samweli na kumshirikisha mambo makubwa sana.
Jambo
la muhimu; Mungu huweza sema na maisha yetu pale tu tunapokuwa tayari
kusikiliza/tunapo onyesha nia.
Kutoka 3:3-4,1samweli 3:10.
(iii)
SULEMANI.1Wafalme 3:7-13. Mfalme huyu aliomba
na Mungu akamsikia na kumjibu.
(iv)
ESTER. Ester 4:16 Kupitia maombi ya Ester
na wayahudi wote, Bwana aliwasikia na kuwajibu kwa kufanya mambo makubwa sana.
Hiyo
ni baadhi ya mifano michache tu, Jambo la msingi la kujua ni kwamba Mungu wetu
anapenda tuwe na mahusiano mazuri na yeye kupitia maombi.
Kupitia
blogger hii tegemea kupata mfululizo waumuhimu wa maombi kwa maisha ya Mkristo.
Machapisho
yajayo:-
ii.
Maombi ni mafuta.
iii. Maombi ni uzima wa Mkristo.
iv. Maombi ni vita dhidi ya shetani.
Ni mimi ndugu yako; Mwl Nicholaus
Simon.
Kiungo katika mwili wa kristo.
Kwa msaada zaidi na ushauri.
Mawasiliano: +255 766 635 382
pataufahamu@gmail.com
Mawasiliano: +255 766 635 382
pataufahamu@gmail.com
Ubarikiwe sana Na nakuomba nisaidie
kuishare kwa marafiki zako ili na wao wajifunze Neno la Mungu.
shalom.Mtumishi Mungu akubariki nimelifulahia somo pia nimepata kitu.
JibuFutaAmen, Barikiwa na Bwana.
JibuFuta