Popote palipo na
ushindi lazima kuwe na nguvu iliyotumika katika kuleta ushindi ule.Nguvu ile
inaweza kuwa nguvu ya kifkra ,silaha,maneno na ibada.Ukristo mpaka ulipo hapa
leo na ulivyo leo hii si kwamba umefika fika tu ,kuna nguvu kubwa ilitumika
katika kuueneza,wengi walisimama kuupinga,na hata wengi waliumizwa ,kwa kuteswa
na kuuwawa kwa vifo vya kutisha.
Kwa mfano, ukifuatilia
historia utaona kuwa Yakobo yule mkubwa aliuawa kwa kukatwa kichwa na herode
mfalme(rejea mdo 12:1-2) ,mtume Petro aliuawa kwa kusurubiwa miguu juu , kichwa
chini na Kaisaria Nero mwaka 67 B.K na mtume paulo aliuawa kwa
kukatwa kichwa na kaisaria Nero mwaka wa 65 B.K na wengine wengine waliofuatia
kutokana na utawala dharimu wa Kirumi.Hata hivyo nguvu ya kushinda iliyokuwemo
ndani ya Mitume ilikuwa kubwa sana kuriko hofu na changamoto zilizokuwa
zinazunguka huduma zao.Mtume paulo anaeleza mateso mengi aliyapata kutokana na
kujitahidi kwake kuieneza injili,anasema kuwa “Lakini,ndugu zangu,nataka
mjue ya kuwa mambo yote yaliyonipata yametokea zaidi kwa kuieneza
injili.hata vifungo vyangu vimekuwa dhahiri katika Kristo,miongoni mwa
askari,na kwa wengine wote pia” Wafilipi 1:12 pia katika ,2kor 11:23-27
“katika taabu kuzidi sana ;katika vifungo kuzidi sana ;katika mapigo kupita
kiasi,na katika mauti mara nyingi.Kwa Wayahudi mara tano nalipata
mapigo arobaini kasoro moja.mara tatu nalipigwa na bakora;mara moja
nalipigwa kwa mawe;mara tatu nalivunjikiwa na jahazi;kuchwa kucha nimepata
kukaa kilindini;katika kusafiri mara nyingi;hatari za mito;hatari za
wanyang’anyi;hatari kwa taifa langu;hatari kwa mataifa mengine;hatari za
mijini;hatari za jangwani;hatari za baharini;hatari kwa ndugu za uongo;katika
taabu na masumbufu;katika kukesha mara nyingi;katika njaa na kiu;katika kufunga
mara nyingi;katika baridi na kuwa uchi”.Paulo anadhihirisha pia kuwa
utendaji wake wa kazi ulikuwa unatokana na nguvu iliyokuwemo ndani
yake,ukisoma,Kol 1:29.
Kwahiyo katika safari
ya maisha lazima kila mwanadamu ajenge nguvu ya kushinda kwani bila hivyo
atajikuta ameondolewa katika ulimwengu kama mwanasayansi Charles Darwin
aliyeleta hoja ya “survive for the fittest” yaani “ishi kwa uzuri/uimara”
akidai ya kuwa, uzuri au uimara wa mtu ndio unaomwezesha aendelee kuishi
duniani kwasababu utamsaidia kujipatia mahitaji yake ya mhimu ya kumwezesha
aendelee kuwa hai.
Kuna
msemo wa kiswahili husema kuwa “ukiona vyaelea, jua vimeundwa” maana yake nini?
Hii inatuonyesha kuwa kila kitu tunachokiona humu duniani kuna nguvu fulani
ilitumika ili kukitengeneza ,hata Mungu alipokuwa anaumba duniani ,hakuitokeza
tu,alitumia nguvu ya kinywa kuweza kuiumba.
Tukumbuke
kuwa, Adamu baada ya kutenda lile kosa la kula tunda katika bustani ya
edeni,alipewa jukumu la kufanya kazi ili aweze kuishi duniani,nalo ni la
kutumia nguvu,baada ya kuambiwa kuwa “atakula kwa jasho lake(Mwanzo 3:17-19)”.
Nguvu ile
ndiyo inayomwezesha mwanadamu kufanya kazi,wanasaikolojia wanaiita ile
nguvu”libido”.
Katika safari ya maisha
tumekuwa tukipitia maisha ya aina mbalimbali,lakini yamegawanyika katika sehemu
mbili ambazo ni masha ya kushinda na maisha ya kushindwa.
Tunaweza
kujiuliza kwanini wakati mwingine tunashinda na kwanini wakati mwingine
tumekuwa tukishindwa huenda ni jambo lile lile? Au tunaweza
kujiuliza kwanini watu wengine wamekuwa mbele yetu katika mambo mbalimbali ya
kimaisha?
Nguvu ya
kushinda ni uwezo unaomwezesha mtu ili aweze kushinda anapokuwa anatembea
katika dunia hii akipitia maisha mbalimbali.Maisha yetu yamegawanyika katika
sehemu kuu mbili ,sehemu ya kwanza ni maisha ya furaha baada ya ushindi na
upendo na maisha ya huzuni baada ya kushindwa kutokana na ugonjwa ,kifo,ajari.
Kumbuka
kuwa uwezo wa kushinda umekaa ndani ya akili ya mtu mwenyewe,mwanafalsafa mmoja
alisema kuwa “kiwango cha mafanikio ya mtu kinapimwa au kinajengwa katika fikra
za mtu” maana yake, jinsi mtu anavyowaza ndivyo atakavyofanikiwa. Ninaweza
kusemakuwa, aina ya mafanikio na kiwango cha mafanikio aliyonayo mtu ni matokeo
ya fikra na juhudi za mtu katika kuyawaza yale mafanikio na kujitahidi
kuyapigania mpaka kuyapata.
Yapo
mambo mengi yanayochangia kuunda nguvu ya kushinda kama yakifuatwa.
Jambo la kwanza
na kubwa kuriko yote ni, Neema ya Mungu maishani mwa mtu, tunaweza
kuzania ya kuwa baada ya mwanadamu kuondolewa katika bustani ya
edeni akapewa jukumu la kutafuta mahitaji yake kwa nguvu zake,huenda Mugu
alimwacha mwanadamu pekee yake asimsaidie hata kidogo,lakini ukweli ni kwamba
bado Mungu amekuwa akiachilia nguvu zake kwa mwandamu ili kumsaidia katika
harakati zake za kujitafutia mahitaji yake.
Mtume Paulo
katika kitabu cha Waraka wa pili kwa wakorintho sura ya kumi na tano mstari wa
kumi, anasema kuwa ameweza kufanikiwa kupita hata mitume waliomtangulia
kutokana na neema ya Mungu inayoizunguka huduma yake “Lakini
kwa neema ya Mungu nimekuwa hivi nilivyo;na neema yake iliyo kwangu ilikuwa si
bure,bali nalizidi sana kufanya kazi kupita wao wote;wala si mimi ,bali ni
neema ya Mungu pamoja nami”.1Kor 15:10.
Hapa
ninaposema neema ya Mungu ninamaanisha nguvu ya uwezo anayopewa mtu na Mungu au
miungu kutokana na kufuata taratibu za ibada au kutokana na upendo wa Mungu au
miungu. Kuna wakati mwingine tunaweza kuwashuhudia marafiki zetu wakifanikiwa
sana au waking’ara sana tukashindwa kuelewa kuwa ni kwa sababu gani.Lakini hii
ndiyo neema ya Mungu au miungu ,kumbuka, hata shetani naye ana neema yake
anayoiachilia kwa watu wanaomwabudu kama anavyomwambia Bwana wetu Yesu Kristo
katika Luka4:6- 7 akisema “Ibilisi akamwambia ,nitakupa wewe enzi
hii yote,na fahari yake ,kwa kuwa imo mikononi mwangu,nami humpa ye yote kama
nipendavyo.Basi ,wewe ukisujudia mbele yangu yote yatakuwa yako”.
Kwa hiyo si kwamba
tunapoona watu wanafanikiwa tunazania huenda ni kwasabu ya uwezo wao wa
kufikiria au juhuda zao ,la, bali ni nguvu fulani iliyonyuma
yao.Ndiyo maana leo tunasikia mara Freemasons na wengine mara wanaenda kwa
waganga wa kienyeji, na wengine kuombewa, yote haya ni kwa ajiri ya kutafuta
usaidizi wa Mungu au miungu.Kumbuka kuwa uwezo wa mwanadamu unampaka au
unamwisho.Kuna mwanafalsafa mwingine alisema kuwa “maisha ya mwandamu yako
chini ya uangalizi au usimamizi wa Mungu,miungu”.Labda niweke sawa hapa kuwa
,kwa kila mtu ipo neema ambayo Mungu huiachilia kwake ili kumsaidia
kudumu katika dunia hii au kushinda upinzani unaojitokeza katika maisha
yake,kinachotofautiana ,ni aina ya neema ,kiwango cha utendaji wa ile neema na
jinsi mtu anavyoitumia ile neema.
Hili nilieleze
kwa kukumbusha kuwa, wakati ukiwa bado uko darasani au kazini kwako ,kwanini
kuna wanafunzi wenzetu wamekuwa wakiwa na uwezo mkubwa kimasomo na
hata tukitumia nguvu nyingi sana lakini bado hatuwezi kufikia uwezo wao. Lakini
makazini tunaweza kujiuliza juu ya uwezo wa wafanyakazi wenzetu
,wapo wamekuwa na uwezo mkubwa wa kufanya kazi na kuzisaidia taasisi au
makampuni kuweza kukua kwa haraka sana.Lakini kibiashara tunaweza kujiuliza
kwanini biashara za watu wengine zinakuwa kwa kasi sana na zetu zinakuwa kwa
kasi kidogo au inatokeaje mtu kukubalika kwa watu na mwingine kukataliwa na
watu?
Hapa
ndipo tunapoongelea neema ya Mungu, inakupa nguvu ya kufanikisha jambo Fulani
kwa wakati Fulani kwa kukupa kibali mbele za watu kwa kazi unayoifanya au
kuzidisha juhudi yako ya kupigania mafanikio.Kuna mtu mmoja alisema hivi “uweza
na utajiri wa mwanadamu ni matunda ya neema ya Mungu” .
.Mfano ,tunaona
viongozi ,wasanii ,wachezaji na wafanyabiashara waking’aa, si kwa juhudi zao tu
bali kwa ile neema ya Mungu inayoandamana nao.
Kwahiyo
kwa kifupi “mwanadamu amekuwa vile alivyo kutokana na kiwango na aina ya neema
inayomzunguka”
.
Jambo la pili ni mtazamo.Mtazamo ni jinsi
unavyowaza na kuhisi juu ya kitu Fulani.Watu wengi wameshindwa kutimiza
ndoto zao au kufikia katika mafanikio ambayo wamekuwa wakiyaota kutokana na
mitazamo yao juu ya hayo mafanikio ,hii inaweza kuwa ni kutokana na mapito
wanayopitia ,mfano wakati mwingine tumekuwa tuna ndoto nyingi sana lakini
kutokana na maisha magumu au changamoto tunazokumbana nazo tumefikia kipindi
tumekata tamaa.
Lakini pia mazingira ya
kuyafikia hayo mafanikio yamekuwa yakichangia watu kukata tamaa.Kulingana na
ugumu ulioko mbele ya safari ya mafanikio tunayoyaendea yamekuwa yakitufanya
tubadili mitazamo yetu ,mfano, wanafunzi wengi wanaacha kusoma masomo ya sayansi
kutokana na kusikia kuwa ni magumu na watu ambavyo wamekuwa wakiyasema. au
kutokana na kuwa kuna kazi zingine ukisoma unapata kazi moja kwa moja, watu
wengine wameacha kusomea kozi ambazo wanazipenda kwasababu ya hofu ya
ajira.Mwanasaikolojia Wiliam James anaseama ,kuwa, “wanadamu wanaweza kugeuza maisha yao ,kwa kugeuza mitazamo ya akili zao”.Mitazamo
yetu inatakiwa kuendana na ndoto zetu au kule tunakotaka kufika.
Kwahiyo
jinsi unavyowaza na kujisikia juu ya mafanikio ndivyo utakavyokuwa. Ingawa
kunaweza kuwa na ukinzani lakini mtazamo wako juu ya yale mafanikio yatakufanya
ufikie mafanikio.Kumbuka kuwa, changamoto si kwamba inakutuzuia tusiweze
kufikie mafanikio yetu ,bali inapunguza kasi yetu kuelekea mafanikio ,ni sawa
na milima na mabonde ,hayaizuii gari kuendelea na safari bali yanapunguza kasi
kuelekea nwisho wa safari.
Mtazamo wa
mafanikio unakupa nguvu ya kuendelea kupigania mafanikio na pia unakufanya
uvumilie.
Tatu,
kubali
kubadilika,katika safari ya kuelekea katika mafanikio unatakiwa wakati
mwingine kuwa kama kinyonga ,ninaposema kubadilika si manisha kuondoka au
kuacha njia uliyokuwa unaipita bali pia kuboresha ile njia .Kwa mfano kama
ulikuwa unafanya kazi kwa masaa sita lakini unaona kabisa kuwa masaa hayo hayatoshi
kukufanya ufanikiwe unatakiwa kuongeza masaa mengine,mfano uanze kufanya kwa
masaa tisa.Kwa mwanafunzi kama ulikuwa unatenga muda wa masaa mawili kwa ajili
ya kujisomea unapaswa kuongeza lisaa moja.Kwa mwombaji kama ulikuwa unaomba
mara mbili kwa siku unatakiwa kuongeza iwe mara tatu kwa siku au kama ulikuwa
unafunga kwa masaa kumi na mbili unatakiwa kufunga kwa masaa ishirini na nne.
si hivyo tu, unaweza ukatafute njia nzingine za kuongeza kipato,mfano kama wewe
ni mwalimu,unaweza ukaanzisha kilimo au ufugaji wa kuku. Unaweza kuanzisha
kampuni wakati ukiwa umeajiriwa, lengo ni kukuza kipato chako.
Ubunifu
unatuwezesha kushinda changamoto mbalimbali tunazokumbana nazo katika safari
yetu ya maisha.
Nne ,kutumia
fursa,Katika maisha ,watu wengi wamekuwa wakishindwa kutimiza ndoto zao
kutokana na sababu ya kwamba wameshindwa kutumia fursa zinazokuja mbele yao.Kwa
mfano watu wengi wanalia leo hii kwasababu ya kuchezea fursa ya kupata
elimu,kwa kuacha shule au kuacha kujituma katika masomo na hatimaye kushindwa mitihani
au kuendekeza tabia zisizofaa na hatimaye kufukuzwa shule.Siku moja nikiwa
sehemu moja jijini Arusha nikinyolewa,kinyozi aliyekuwa akininyoa alikuwa
akilalamika sana kwa kudai kuwa anajuta kwa kukataa kusoma kutokana na ushawishi
wa rafiki zake,wakaendekeza madawa ya kulevya. Lakini leo hii anatamani apate
mtu atakayemwambia arudi shuleni, atafurahi sana na ataenda kujituma ili
atimize ndoto zake.
Katika maisha zipo
fursa nyingi zinazojitokeza katika maisha yetu,kama ,fursa za elimu,ajira na
fursa za kutumia mali asili.
Katika nchi nyingi za
Afrika ,kuna tatizo kubwa la serikali kushindwa kutumia fursa zilizopo ili
kukuza kipato cha nchi kwa mfano katika taifa letu la Tanzania kuna tatizo
kubwa la kushindwa kutumia fursa za mali asili kama madini,gesi na misitu.Ndiyo
maana kipato cha nchi kimekuwa kidogo kiasi cha kwamba kuifanya serikali
kutegemea kukopa kwenye benki za duniani au nchi za magharibi ili kupata pesa
za bajeti.
Ukiangalia nchi nyingi
za ulaya ziliweza kuendelea kwa kasi sana kutokana na kutumia fursa zilizokuwa
mbele yao ,hasa ardhi kwa kilimo na ufugaji ,karne ya tano baada ya kuanguka
kwa utawala wa Rumi.Walifanya kazi kwa bidii na kwa ushindani sana,tofauti na
nchi zetu za Afrika ,leo hii ingawa watu ni maskini ,lakini hawajitumi kabisa
katika kazi,uvivu na uzembe kazini ni mkumbwa.Wengi wetu tunapenda starehe tu kuriko kazi utazania tuko peponi.
Lakini pia ,Wakati,
Mwanadamu hupita katika nyakati za aina mbalimbalia kama inavyosema katika
mhubiri 3:1-8 imeandikwa”Kwa kila kila jambo kuna majira yake,na wakati wa
kila kusudi chini ya mbingu. Wakati wa kuzaliwa ,na wakati wa kufa;wakati wa
kupanda,na wakati wa kung’oa yaliyopandwa;wakati wa kuua,na wakati wa
kupoza;wakati wakubomoa na wakatiwa kujenga;wakati wa kulia na wakati wa
kucheka;wakati wa kuomboleza na wakati wa kucheza…..wakati wa kutafuta na
wakati wa kupoteza…”.
Kwa maana hiyo kuna
wakati tumekuwa tukishindwa kutokana na sababu ya kuwa tupo katika wakati wa
kushindwa. Inawezekana usinielewe vyema lakini ukikaa chini na kutafakari
utaelewa,j iulize kwanini kuna wakati biashara yako ilichangangaya,ukafurahi
sana ,lakini kwanini kuna wakati biashara yako ilikwama ukaanza kuhuzunika
,ukitaka kutafuta hata mchawi.Kwanini inafikia kipindi tunakwama katika mambo
yetu tunayoyafanya?j ibu ni kwamba ,wakati.
Zaidi
,Uvumilivu,Uvumilivu
ni kitendo cha kuwa na subira au kustahimili ukinzani anaokumbana nao mtu.Kama
nilivyosema hapo mwanzo kuwa, safari ya maisha ni safari inayochangayikana na
changamoto,kwahiyo kama unataka kushinda lazima uzishinde changamoto.Ninaweza
kusema kuwa “katika kila hatua moja unayotaka kuvuka ya kimaisha ili uingie
hatua nyingine ya kimaisha unatakiwa kutegemea kukutana na changamoto”.
Unapovuka changamoto
moja si kwamba ndio umekuwa salama unatakiwa kujua kuwa unapovuka changamoto
moja kuingia hatua nyingine ya mafanikio,kuna changamoto nyingine katika hatua
hiyo,kwa hiyo jiandae kuikabili.Kwa kifupi ,katika kila hatua ya maisha ipo
changamoto yake.D.k Robert H.Schuller anatufundisha kuwa “wakati mgumu huwa
haudumu bali watu wagumu au wenye nguvu ndio wanaodumu”.Kwa hiyo katika maisha
changamoto utakutana nazo tu,lakini weka katika akili yako kuwa,hiyo changamoto
haitadumu milele,ipo siku itazimika kama mshumaa.Walter Chrysler ,yeye anasema
kuwa “siri ya mafanikio ni kuwa na shauku”.
Kwahiyo shauku yetu juu
ya mafanikio inatakiwa kuzidi kuwa kubwa hata tunapokutana na mapingamizi ya
kila namna.Hapo mwanzo tumeona kuwa Mtume Paulo alikutana na changamoto za
kila namna ,hata hivyo hakukata tamaa,hii inatokana na shauku yake
ya kuieneza injili na kukamilisha huduma yake.Anasema kuwa aanendelea kukaza
mwendo ,bila kuangalia ya jana ,ila yeye anayachuchumilia yaliyo
mbele(Wafilipi 3:12-13).
Na,Uthubutu,
watu wengi wanashidwa kuvuka hatua moja ya mafaniko kwenda mbele
kutokana na kujaza maneno ya “siwezi” ndani ya fikra zao.Hiii inatokana na hofu
kubwa iliyojaa ndani ya mioyo yao.Watu wengi hutamani kujua ngazi zote
wanazopaswa kuzipanda,lakini Mkuu Martin Luther King jr mwanafalsafa na
mwanaharakati wa watu weusi amerika anasema kuwa “chukua hatua ya kwanza kwa
imani,si lazima uone ngazi zote,chukua tu hatua ya kwanza”.Methali ya wachina
inasema kuwa “safari ya maili elfu,huanza kwa hatua moja”.Kwahiyo lazima
tushinde hofu inayotuzuia kuanza kwani bila kuanza hatuwezi kufika tunakotaka
kufika. Rais wa kwanza wa Afrika Kusini kutokana na kuhangaika kwingi na
hatimaye kushinda, alisema kuwa “Nimejifunza kwamba,ujasiri si kwamba haukuwa
na hofu ndani yake,lakini shangwe ndani yake.Mtu shujaa si kwamba hana hofu
,bali ni Yule anayeishinda hofu”.
Kwahiyo
tunapotaka kuchukua hatua na mazingira yetu yanayotuzunguka
yanatudokeza kuwa, hatuwezi si kwamba tukate tamaa bali tutafute
namna ya kuanza, hata kama ni kwa unyonge sana. Unapoanzisha kitu Fulani si
lazima kiwe kimetimilika kwa asilimia mia,bali hicho ambacho hakijakamilika
kinawezakuwa mtaji wakukupeleka katika kitu kilichokamilika.Mfano; unapotaka
kuanzisha biashara Fulani ,si lazima uwe umekamilika kila kona,hiyo hiyo
biashara nyonge inaweza kuwa mtaji wa kupata biashara kubwa.Mfano siku moja
katika kipindi cha televisheni cha klauds fm kinachoitwa “siz kitaa” kuna bwana
mmoja alisimulia namna ambavyo aliweza kupata mafanikio makubwa(kuwa na
kiwanda),anasema kuwa alianza kwa magunia matano tu ya mpunga,lakini
baada ya jitihada kubwa ,sasa anakiwanda.
Hivyo,
katika kile ulichonacho unaweza kukitumia kuwa mtaji wa kukufanya ufike pale
ambapo umekuwa ukiota.Watu wengi wameshindwa kufika katika mafanikio ambayo
huyatamani kwasababu ya kushindwa kutumia mitaji waliyonayo kwa kuona kuwa ni
midogo sana, mfano kujenga nyumba.
Nakumbuka
baba yangu mzazi alipokuwa akishauriwa kujenga nyumba, alikataa sana kwa kudai
kuwa hana pesa, kwani yeye alitaka apate pesa ya kujenga moja kwa moja na si
kidogo kidogo,kipindi hicho mimi nilikuwa bado mdogo sana.Lakini baada ya mama
yangu kuamua kuanza ujenzi yeye kama yeye ,naye ameamua kuungana naye ,ingawa
kidogo kidogo ,kutokana na kuwa na pesa kidogo,hata hivyo hivi sasa wako mbioni
kumaliza ujenzi wote.
Kama
ulikuwa hufahamu ,nikudokeze siri hii,mara nyingi unapoanzisha jambo,ndipo hata
akili ya namna ya kuliendeleza huja na hata milango hufunguka kwa ajiri ya
kufanikisha jambo hilo.
Rais marafu sana
wa sasa duniani,nikimaanisha Baraka Obama alisema kuwa,”mabadiliko hayatakuja
kama tukisubiri wakati mwingine au watu wengine,sisi ndio tuliosubiriwa kwa
ajiri ya hayo,sisi ndio mabadiliko tunayoyatafuta”
Nihitimishe
kwa kusema kuwa kila mtu anao utajiri wa mafanikio na
nguvu,inategemea ni jinsi gani anautumia huo utajiri na kwa namna gani ili
kupata matokeo chanya.
IMEANDALIWA NA Emmanuel & Jonathan.
Brother i'm much blessed with such a post so nive and very powerful doctrine emerging people to get onto their knees and pray. God bless you. Endelea usikate tamaa.
JibuFutaAmen, mtu wa Mungu nitajitahidi zaidi kuweka machapisho kama hayo.
JibuFuta