MWANZO 1:1
''Hapo
mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi. Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu, na
giza lilikuwa juu yauso wa vilindi vya maji; Roho ya Mungu ikatulia juu
ya uso wa maji.''
Tangu
mwazo Neno alikuwa na Mungu. Kwa njia yake vitu vyote viliumbwa; hakuna hata
kiumbe kimoja kilichoumbwa pasipo yeye. Yeye alikuwa chanzo cha uhai na uhai
huo ulikuwa mwanga wa watu. Na mwanga huo huangaza gizani, nalo giza halikuweza
kuushinda.
Basi
Neno alikuwa ulimwenguni, na kwa njia yake ulimwengu uliumbwa, lakini ulimwengu
haukumatambua. Alikuja katika nchi yake mwenyewe, nao walio wake
hawakumpokea. Lakini wale waliompokea, wale waliomwamini, aliwapa uwezo wa kuwa
watoto wa Mungu, ambao walizaliwa si kutokana na uwezo wa kibinadamu wala
nguvu za mwili wala mapenzi ya mtu, bali kutokana na Mungu mwenyewe.
Chakujifunza
katika ujumbe wetu huu wa wiki ni kwamba, katika maisha lazima uanze na Mungu
kwa mambo yote uyafanyayo, kwasababu yeye ni mwanzo wa vitu vyote vinavyo
onekana na visivyo onekana.
BY
counselor Nicholaus Simon
Post A Comment:
0 comments: