Mara nyingi viwango vya
mafanikio vinapimwa kwa elimu tuliyopata, kiasi cha fedha tulizonazo benki,
ukubwa wa nyumba zetu, au kiasi gani cha
mali tunamiliki.
Tambua kwamba katika
maisha ya hapa dunia, kila mtu anaweza fanikiwa kulingana na uhitajia alio nao
binafsi, pale tu anapo tosheka na kukidhi uhitaji wake kwa wakati huo, twaweza
sema amefanikiwa.
Wakati mwingine,
mtizamo huu umekuwa tofauti sana kwa baadhi ya watu kwasababu jamii inayo
tuzunguka yenyewe imezoea kuwa Mafanikio ni kuwa na mali nyingi sana. mfano;
kumiliki magari, nyumba kubwa, na makampuni makubwa. si kwamba hawapo sawa la
hasha, ila wamesahau kuwa mtu anaweza akawa na vitu hivyo ila ndani ya moyo
wake, akawa hana amani wakati wote, kwasababu mbalimbali mfano za kifamilia,
ambazo zikamwondolea amani kabisa na hata kuona maisha kwake hayana faida, ila
si kwamba hana pesa, kwahiyo mafanikio yana anzia ndani ya moyo na kutoka nj'e.
Tumia njia hizi nne ili
ufanikiwe katika mambo yako yote.
(1) Jua unacho taka.
huwezi ukapata kitu kama hujui unacho kiitaji, kwahiyo jambo la kwanza
nikutambua uhitaji wako ni nini, hii ni njia bora ya kwanza ya kuanza kufikia
kwenye mafanikio yako yawe ya kiuchumi, kijamii, kiroho.mfano unahitaji
kuwa tajiri sana.
(2) Chagua cha
kufanya. katika ulimwengu huu ziko fursa nyingi sana ila kati ya hizo zote
lazima ifike sehemu uchague moja ambayo unauwezo nayo, na baada ya kuifanya
itazidi kukupeleka karibu na mafanikio yako, haitakiwi kubahatisha. mfano
unahitaji ufanye biashara, ili ufikie mafanikio yako.
(3) jua namna ya
kufanya. Baada ya kuchagua cha kufanya, hicho kitu ulicho ona kwako ni
sawa, swali ni kwamba je, una ufahamu au maarifa ya kutosha juu ya kuendesha jambo hilo, nina
maana elimu yake, mfano unahitaji ufuge samaki je, una elimu ya ufugaji wa
samaki. katika eneo hili pia kuna mikanganyiko ya watu wengi sana ,kuhusu mtaji
wa kuanzia katika jambo lolote ila ukweli ni kwamba Mtaji wa kweli ni ''UBORA WA MAARIFA ALIYO
NAYO MTU, JUU YA JAMBO ANALO
HITAJI KUFANYA''.
(4) Fanya.
hii ni hatua ya mwisho Ambayo hukulazimu kuchukua maamuzi ya kuthubutu, watu
wengi wameshindwa kufanikiwa si kwamba hawana huitaji, au wameshindwa kuchagua
cha kufanya au hawajua namna ya kufanya la hasha, tatizo ni kuthubutu kuanza
kufanya, Maneno yamekuwa mengi sana zaidi ya uhalisia. Hofu imekuwa ni tatizo
la kuwafanya waone hawawezi kufanya.
Tambua Elimu ni muhimu;
lazima tuitafute ile inayopatikana yote. Na hakuna kitu kibaya kuhusu kazi
nzuri na utajiri. Ila ukweli hasa ni, jinsi gani tunawatendea wengine na
tunafanya nini elimu na fedha zetu ndivyo vitakavyokumbukwa, kwa muda mrefu na
watu hata baada ya kufa.
Mafanikio
ya kweli yanaweza kupimwa mwishoni mwa maisha yetu, kwa namna tuliyopata
kuitumia jamii na kumuheshimu Mungu. Hii ni aina pekee ya mafanikio ambayo
huwezi kunyang'anywa.
Unapimaje mafanikio
Tuseme ungelikuwa na
fedha nyingi. Ungeliweza kununua kila ulichohitaji. Sasa, yamkini una orodha ndefu
ya vitu vya kununua. Na kwa fedha hizo
zote, watu wengi wangeweza kusema
umefanikiwa.
lakini, vipi kuhusu ile
orodha nyingine katika upande wa rohoni, nina maana baada ya siku zako za
maisha hapa duniani kufika kikomo, upande wa pili itakuwaje? Orodha halisi ya vitu kama fedha haiwezi
kununua, au kukusaidia kitu katika ulimwengu wa pili, baada ya maisha ya hapa
duniani kufika kikomo. Orodha inayotoka moyoni, iliyo jaa matendo mema ya
kumpendeza Mungu, na wanadamu, hii inaweza kukusaidia.
ni maombi yangu
kwako, Mungu wa mbingu na nchi aliye kuumba wewe kwa jinsi ya ajabu ya kutisha,
akakuangazie nuru yake katika ufahamua wako, akupe maarifa juu ya huduma ,kazi,
familia, na yote utakayo fanya yakawe baraka kwako,. Amen
Ni mimi ndugu yako Counselor Nicholaus Simon.
Kiungo katika mwili wa kristo.
Kwa msaada na ushauri.
whatsap 0654-623492.
pataufahamu@gmail.com
Ubarikiwe sana Na nakuomba nisaidie kushare kwa
marafiki zako ili na wao wajifunze Neno la MUNGU.
Post A Comment:
0 comments: