Madhara haya ni matokeo ya kusambaa kwa uozo ulionzia kwenye roho, kupitia nafsi na hatimaye kuonekana katika mwili, Madhara yanayojulikana wazi ni pamoja na mimba bila familia, ambayo matokeo yake ni mtoto bila familia.
Mengine ni pamoja na magonjwa na kifo, yaani magonjwa yanayosambazwa kwa ngono, pamoja na ukimwi. pia kuna kuvunjika kwa ndoa ya familia kwa sababu ya kukosa uaminifu. Na tena kuna kuwa  mtumwa wa mtu, yaani unapolazimika kuoa au kuolewa na mtu kwa sababu tayari kuna mimba. Wengine wanatambua uzito kamili wa utumwa huumiaka michache baada ya kufunga ndoa na mtu amabye hakuwa chagua lake. Ndoa za namna hii zimekuwa mzigo mzito kwa ndoa yenyewe na kuleta madhara kwa watoto pia ambao wanajikuta katika nyumba isiyo na upendo.
Baadhi ya watoto wanakuwa wakijitambua kwamba ‘‘JANGA’’ la kutungwa mimba kwao, ndiyo jambo lililolazimisha ndoa ya mateso ambayo wazazi wao wanapitia.  Hiki ni kidonda  kibaya  sana kwa mtoto au hata mtu mzima pale anapo gundua jambo kama hili, hakika linaumiza sana..
Jambo nzuri ni kwamba katika yote haya Mungu bado ni mwema, kupitia washauri ambao Mungu uwatumia kusaidia kuwatoa watu au mtu katika maumivu makali..

Ni mimi ndugu yako Counselor Nicholaus Simon.

Kiungo katika mwili wa kristo.
Kwa msaada na ushauri.
whatsap 0654-623492.
pataufahamu@gmail.com
Ubarikiwe sana Na nakuomba nisaidie kushare kwa marafiki zako ili na wao wajifunze Neno la MUNGU. 

Axact

Axact

Vestibulum bibendum felis sit amet dolor auctor molestie. In dignissim eget nibh id dapibus. Fusce et suscipit orci. Aliquam sit amet urna lorem. Duis eu imperdiet nunc, non imperdiet libero.

Post A Comment:

0 comments: