Potential |
1TIMOTHEO 6:7, 10.
Kwa maana hatukuja na kitu
duniani, tena hatuwezi kutoka na kitu. Maaana shina moja la mabaya ya kila
namna ni kupenda fedha; ambayo wengine hali wakiitamani hiyo wamefarakana na
Imani, na kujichoma kwa maumivu mengi.
Ndugu yangu, ukisoma vizuri
hilo Neno la Mungu, unaona jinsi ambayo linaonesha kuwa mimi na wewe hatukuja na
kitu chochote hapa duniani wala hatuwezi kuondoka na kitu, natamani
nikushirikishe kitu fulani, Maisha siku
zote ni kuchagua Je, unatamani uishi tu au uishi kwa kutekeleza kusudi la
Mungu katika maisha yako, tunapo kuwa hapa duniani kiukweli pesa huwa
inaonekana ni kitu cha thamani sana na wakati mwingine huweza kutufanya
tuondoke kwenye kutekeleza kusudi la Mungu, si kwamba pesa ni mbaya hapana bali
tunapo ipenda sana, huwa mungu kwetu, Jitahidi sana kuwa makini unapo itafuta
hiyo pesa isichukue nafasi kubwa ndani ya moyo wako kuzidi nafasi ya Mungu.
Tafakari hayo kwa kina.
Nikutakie Wakati mwema ndugu
yangu.
By; Counselor Nicholaus
Simon.
Post A Comment:
0 comments: