Counselor Nicholaus Simon.
      Kwanini tujifunze somo hili.
     1. Watu wengi ndani ya kanisa na n’je ya kanisa hawajifahamu jinsi walivyo.
     2. Unapo jifahamu kuna mchango mkubwa katika maisha ya kiroho.
     3. Unapo jifahamu kuna mchango mkubwa katika maisha ya kimwili.

      1. Watu wengi ndani ya kanisa na n’je ya kanisa hawajifahamu jinsi walivyo.
Usipo jifahamu jinsi ulivyo huwezi kujua wajibu wako au nini kinachokufaha ukifanye.
Kiuhalisia ni kwamba, wewe jinsi ulivyo mpaka unazaliwa upo ndani ya mpango mkubwa wa Mungu.
Yeremia 1:5 Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa mataifa.
Mungu amekujua kabla ya mtu yeyote kukujua wewe!
Mungu amekujua Zaidi ya Wazazi wako waliohusika kukuzaa wewe!
Mpendwa, Tambua haupo kwa baati mbaya kabisa na hili swali jiulize maeneo yote unapo kuwepo! Ni kwaajili gani nipo hapa iwe katika ofisi, shule, chuo n.k
Haujazaliwa ili uishi tu…..!!
 
Scientific prove that! Six hundred million of sperm go direct to Eggs through sexual, But Five hundred and nitynine mil dead.
Swali ni hili kwanini zife mbegu zote hizo na moja ipone!!!
Upo kuleta UTOFAUTI HAPA DUNIANI.
UPO KULETA VITU VIPYA AMBAVYO HAVIKUWEPO.

Zaburi 139:13-16 Maana Wewe ndiwe uliyeniumba mtima wangu, Uliniunga tumboni mwa mama yangu. 14 Nitakushukuru kwa kuwa nimeumbwa Kwa jinsi ya ajabu ya kutisha. Matendo yako ni ya ajabu, Na nafsi yangu yajua sana, 15 Mifupa yangu haikusitirika kwako, Nilipoumbwa kwa siri, Nilipoungwa kwa ustadi pande za chini za nchi; 16 Macho yako yaliniona kabla sijakamilika; Chuoni mwako ziliandikwa zote pia, Siku zilizoamriwa kabla hazijawa bado.
          1.  Kabla hujawa bado kuwepo duniani ulikuwa kwenye fikra za Mungu.
Kwahiyo Mungu kabla ya kukuumba wewe alikwisha weka kila miundo mbinu ya wewe kufanikiwa katika maisha yako yote ya kiroho na kimwili huku ukitimiza kusudi la wewe kuzaliwa.
         2. Maisha yako yalianza rohoni kwanza. 
Unapo pata akili ya kujifahamu jinsi ulivyo ni lahisi sana kujikwamua katika vifungo mbalimbali vya kijamii.   
Usidanganyike Hakuna mtu yeyote anaye kufahamu vizuri Zaidi ya Roho Mtakatifu.
Kwahiyo kuwa makini;-
1. Maneno yanayo kuzunguka hasa ya negative. (unacho sikia, kuona huwa vina mchango wa kukufanya uwe vile ulivyo). 
2.  Kujilinganisha na watu uwezo wa kufanya mambo mbalimbali.,hili ni kosa kubwa sana katika maisha.
MUHIMU: Roho Mtakatifi peke yake ndiye anaye kufahamu Mwombee sana.
Secret / Siri: Unapo tamkiwa maneno mabaya kemea au kata direct-Maneno yana umba.

2. Unapo jifahamu kuna mchango mkubwa katika maisha ya kiroho.
Baada ya kuokoka si kwamba unabadilika kimwili jinsi ulivyo kuwa la hasha si kweli bali tukio hili huwa la kiroho, mabadiliko huanzia ndani ya moyo wako na kuleta matokeo ya n’je.
Mfano. (a) Mvuta bangi. (b) Aliyekuwa anapenda muziki ya kidunia.
Kwahiyo hata baada ya kuokoka lazima ujifahamu vizuri kuwa mwanzoni, ulikuwa unatumikwishwa eneo gani hasa ili ukilifahamu vizuri ni lahisi kupambana nalo.
Waebrania 12: 1 Basi na sisi pia, kwa kuwa tunazungukwa na wingu kubwa la mashahidi namna hii, na tuweke kando kila mzigo mzito, na dhambi ile ituzingayo kwa upesi; na tupige mbio kwa saburi katika yale mashindano yaliyowekwa mbele yetu.
Hakuna kitu hatari kama dhambi tena hasa kwa wewe uliye okoka.
1. Huondoa ujasiri mbele za Mungu. 
2. Huondoa kibali cha kiungu juu yako. 
3. Shetani hupata nafasi ya kukutesa.  Mfano FRIEND FROM MBEYA.
4. Huleta maumivu makali sana ndani ya moyo kwa mtu anaye mfahamu Mungu kweli kweli.

MAELEZO MAFUPI NAMNA YA KUPATA MAJIBU:
 Toba ya kweli kwa kukubali kosa na si kila dhambi unaweza jiombea peke yako.
Baadhi ya dhambi ni lazima utoe taarifa kwa kiongozi wako wa kiroho ili akuombee toba ndipo utapata upenyo wa kiroho.

Baada ya hapo  Sahau / forgetting ni funguo kubwa ya kumwacha mtu huru.
Mfano: Saul ~Paul.   (MKAZO MKUBWA HAPA)
Matendo ya Mitume 9:1 Lakini Sauli, akizidi kutisha na kuwaza kuwaua wanafunzi wa Bwana, akamwendea Kuhani Mkuu, 2 akataka ampe barua za kuenda Dameski zilizoandikwa kwa masinagogi, ili akiona watu wa Njia hii, waume kwa wake, awafunge na kuwaleta Yerusalemu.
3 Hata alipokuwa akisafiri, ikawa anakaribia Dameski; ghafula ikamwangaza kote kote nuru kutoka mbinguni. 4 Akaanguka chini, akasikia sauti ikimwambia, Sauli, Sauli, mbona waniudhi?
5 Akasema, U nani wewe, Bwana? Naye akasema, Mimi ndimi Yesu unayeniudhi wewe.
Paul alisomea ualimu wa Sheria (yaani wa Torati) huko Yerusalemu chini ya mwalimu maarufu Gamalieli wa madhehebu ya Mafarisayo.
Akishika dini yake kwa msimamo mkali akawa anapinga Ukristo kwa kuwakamata, kuwatesa na hata kuwaua Wakristo, kama vile Stefano Mfiadini.
Alifanya hivyo mpaka alipotokewa na Yesu Kristo mfufuka akiwa njiani kwenda Damaski, Syria (kwa umuhimu wake katika Historia ya Wokovu habari hii inasimuliwa mara tatu katika kitabu cha Matendo ya Mitume: 9:1-19; 21:12-18 na 22:5-16). Jibu lake kwa Yesu lilikuwa (Mdo 22:10): "Nifanye nini, Bwana?"
Baada ya kubadilika na kusahau: MATOKEO YALIKUWA HIVI:-
(kwa makanisa ya Thesalonike, Korintho, Galatia, Roma, Filipi, Kolosai, Efeso, kwa viongozi Wakristo kama Timotheo na Tito, tena kwa Filemoni), katika Agano Jipya zinatunzwa 13.
Ukubwa na ubora wa mchango wa Paulo unaeleweka tukizingatia kwamba alifanya kazi na kuandika kabla ya vitabu vya Agano Jipya kupatikana. Ndiye aliyeanza kuliandika akipanua mawazo aliyoyapokea katika Kanisa kwa kuzingatia Agano la Kale na mang’amuzi yake mwenyewe.
Hapo alifafanua vizuri ajabu maisha ya Kikristo kama neema ya kumshiriki Yesu kwa imani, sakramenti na juhudi za kushinda umimi hadi kugeuka sadaka hai, takatifu na ya kumpendeza Mungu.
Wokovu huo, utakaokamilika katika ufufuko wa mwili, unapatikana katika Kanisa, ambalo Paulo alilitambulisha kama bibiarusi wa Kristo na mwili wake.
Haijalishi umefanya kosa gani au dhambi gani lazima ifike hatua usahau.
Pia usisahau Kusamehe ukisha jifahamu vizuri tambu wewe binafsi usingeweza kuapata neema ya wokovu bali ni kwa neema tu ya Mungu, nawe una budi kusamehe.
Mathayo 6:12 Utusamehe deni zetu, kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu.


3. Unapo jifahamu kuna mchango mkubwa katika maisha ya kimwili.
Maisha haya tuliyo nayo ni matokeo ya jinsi tulivyo ndani ukianzia (rohoni, na kwenye fikra/mtizamo wako).
Usipo jigundua uwezo wako always huwezi kugundua Vipawa ambavyo Mungu amekupa.
  •  Karama, kipawa na Huduma.
Neno karama hili ni neno linalo maanisha Zawadi/Gift na hutumika hasa katika Biblia likielezea”Gracious gift from God.” Or a thing given willingly to someone without payment; a present. Ambapo anaye toa ni ROHO MTAKATIFU kwa Mtu kwa faida ya kanisa.
--Huu ni uwezo wa kiMungu unao fanya kazi ndani ya Mtu.(Karama)

Muhimu: Mtu asiye okoka hazimuhusu hizi karama.
Iwakorintho 12:4 Basi pana tofauti za karama; bali Roho ni yeye yule. 
1 Corinthians 12:4 now there are varieties of gifts, but the same Spirit;
Kibiblia zipo karama tisa (9) 
    1.   Kundi la kwanza KARAMA ZA UFUNUO
           a. NENO LA HEKIMA
           b. NENO LA MAARIFA
           c. KUPAMBANUA ROHO.
    2.   kundi la Pili KARAMA ZA NGUVU.
            a. IMANI
            b. UPONYAJI
            c. MATENDO YA MIUJIZA.
   3. Kundi la tatu KARAMA ZA USEMI.
           a. KARAMA YA UNABII
           b. TAFSIRI ZA LUGHA
           c. AINA ZA LUGHA
Kipawa ni ni uwezo binafsi ambao mtu anazaliwa nao. Or
 a natural ability or talent.  mfano Kuimba/kuimba/kuchora/kucheza mpira.
(http://Karamaismyname.ning.com)
Huduma ni kitendo cha kusaidia kitu fulani or is the action of helping some things.
Katika mwili wa kristo huduma zipo kuu tano ila zipo nyingi Zaidi ya hizo tani za msingi.
1. Uchungaji, 2. Ualimu, 3.Uinjilisti, 4.Unabii na 5.Utume. Nyinginezo mfano, kupamba, usafi ndani ya kanisa n.k
       Waefeso 4:12, 1wakorintho 12:4-31.
MUHIMU: karama ni kama kifaa kinacho wezesha huduma ifanye vizuri, yaani karama ni kama kinoleo cha panga.
PANGA—HUDUMA
KINOLEO—HUDUMA
Mfano: Huduma ya Uinjilisti inayotumika na karama na isiyo na karama.
àUsipo kuwa na ujuzi katika haya maeneo upo uwezekano wa kupoteza Huduma, karama au kipawa chako kisiendelee kikafa.
Unapo jua na kutendea kazi lazima ufanikiwe watu walio wengi eneo la Vipawa halifahamiki kabisa na kama linafahamika halitendewi kazi kifasaha.
KUPITIA KIPAWA CHAKO   
  1.  Utastawi sana hasa kiuchumi.
  2.  Utainua watu wanaokuzunguka.
  3.  Utamtumikia Mungu kwa uhuru na upana mkubwa.
  4.  Akiba yako mbinguni itaongezeka. utakuwa na uwezo mzuri wa kiuchumi.
Mathayo 6:21   kwa kuwa hazina yako ilipo, ndipo utakapokuwapo na moyo wako.
Matthew 6:21 For where your treasure is, there your heart will be also.
Note: Take care Mungu huachilia Ideas hasa tunapo mwomba kupitia ideas ndipo tunafanikiwa katika maeneo yote ya kiroho na kiuchumi n.k

USIPO JUA KIPAWA CHAKO.
1. Kuishi chini ya kiwango, ambacho Mungu anaitaji uishi. 
2. Utakuwa mtumwa maishani mwako.
3. Utamtumikia Mungu kwa uchovu sana.
4. Akiba yako mbinguni itakuwa dhaifu sana.

  NIMALIZIE KWA KUSEMA: 
     (a)  Jikubali, usijizalahu hata kidogo vile ulivyo.
     (b) Wewe ni wathamani sana hapa duniani.

SPECIAL PRAYER / MAOMBI MAALUM.
 (a) Kuokoka Kama bado haujaokoka jitahidi sana, kuchukua maamuzi haya ambayo ni yamuhimu sana katika maisha ya mtu akiwa hapa duniani.
 (b) Swala la Muziki, kama eneo hili linakusumbua kila ukijaribu kuacha kusikiliza muziki wa kidunia, imekuwa ngumu.
 (c) Dhambi ikuzingayo/ulikaa kimya pasipo kusema, yawezekana upo kwenye kipindi kigumu sana baada ya kutenda dhambi na kushindwa kusema ili upate msaada.
 (d) Swala la kusamehe, eneo hili ni gumu japo kwa Mungu hakuna gumu kama mpaka sasa kuna jambo limekuwa gumu kusamehe.
 (e)  Karama, huduma na vipawa.

Ni mimi ndugu yako Counselor Nicholaus Simon.
Kiungo katika mwili wa kristo.
Kwa msaada na ushauri hasa kwenye eneo hilo la Maombi.
whatsap 0654-623 492. & Call: 0766-635 382
pataufahamu@gmail.com
Ubarikiwe sana na nakuomba nisaidie kushare kwa marafiki zako ili na wao wajifunze Neno la MUNGU. 








Axact

Axact

Vestibulum bibendum felis sit amet dolor auctor molestie. In dignissim eget nibh id dapibus. Fusce et suscipit orci. Aliquam sit amet urna lorem. Duis eu imperdiet nunc, non imperdiet libero.

Post A Comment:

0 comments: