Ndugu
yangu nipende kukurabisha katika mfululizo huu wa somo hili, hasa kwa vijana
ambao bado hawajaoa na kuolewa.
Katika
ulimwengu wa leo sana sana katika maisha siku za hivi karibuni, kumekuwa na
kelele na maongezeko makubwa juu ya matatizo ya ndoa katika familia nyingi duniani,
Utakubaliana na mimi kwamba kumekuwa na Idadi kubwa sana ya ndoa zinazofungwa
katika sehemu mbalimbali katika nyumba za Ibada na hata zile zinazofungwa chini
ya usimamizi wa serikali (Bomani) tofauti ni ilivyo fanyika zamani au kipindi
cha miaka ya nyuma kidogo.
Kinacho
nisikitisha Sana ni gharama kubwa ambazo zimekuwa zikitumika kuandaa sharehe
kubwa za harusi ambazo zimekuwa zikigubikwa na huzuni /majuto/simanzi/ugomvi
bayana ya wanandoa baada ya kufungwa.
Katika
ndoa nyingi zinazo fungwa siku za leo imekuwa ni kama jambo la kawaida sana
kusikia wanandoa wapya kabisa kutamka maeneo kama vile ‘‘Najuta kuoa kipindi
hiki’’, Nimefanya haraka au uamuzi mbaya
kuingia katika ndoa kwa sasa,’’ ‘‘Siamini kabisa kama mwenzi wangu katoka kwa
Mungu”, “yaani nimeoa au kuolewa na kituko”, ‘‘Sina jinsi na vumilia tu, najikaza
tu lakini uzalendo umenishinda’’, ‘‘Sina raha kabisa’’, ‘‘Ningeweza ningeolewa tena’’
Ndugu
msomaji fuatilia kwa makini sana mfululizo huu, hakika utakusadia sana kama si
wewe hata ndugu na jamaa wanaokuzunguka, lengo ni kuwa na familia bora ambazo
hazina manung’uniko kila itwapo leo.
-->Usijiunganishe
na mtu asiye okoka. (Wala usimsaidie Mungu kazi/kuokoa)
Mwanzo 24:3 nami nitakuapisha kwa BWANA, Mungu wa mbinguni, na Mungu wa
Nchi, kwamba hutamtwalia mwanangu mke katika binti za Wakaani ambao nakaa kati
yao.
kama
kijana uliye okoka ni kosa kubwa kuoa au kuolewa na mtu asiye okoka, ukisoma andiko
hilo katika Mwanzo, utaona jinsi gani Mungu alipiga marufuku kwa mwisrael kuoa
au kuolewa na mkaanani, katika maisha yetu ya sasa Mtu yeyote akiokoa naye ni
mwisrael na lile Agano linaendelea kwake, na mkaanani ni sawa na mtu asiye
okoka.
1petro 2:9-10, Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu,
watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke
gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu; ninyi mliokuwa kwanza si taifa, bali
sasa ni taifa la Mungu; mliokuwa hamkupata rehema, bali sasa mmepata rehema.
Kwahiyo
mkristo yeyote aliye okoka ni mwisrael. Kama kijana uliye okoka kuoa au kuolewa
na mkaanani mtu asiye okoka ni kosa na haitakiwi.
Kuna
madhara makubwa pale kijana aliye okoka anapokuwa ameolewa au kuoa na kijana
asiye okoka.
1Wafalme 11:1-8, Mfalme sulemani akawapenda wanawake wengi waeni, pamoja na
binti yake Farao, wanawake wa Wamoabu, na wa waamoni, na wa waedomi, na wa sidoni, na wa Wahiti, na wa mataifa BWANA
aliyo waambia wana wa Israeli, Msiingie
kwao, wala wasiingie kwenu; kwa kuwa hakika wataigeuza mioyo yenu kuifuata miungu
yao. Sulemani akaambatana nao kwa kuwapenda.Akawa na wake mia saba binti za
kifalme,na Masuria mia tatu; nao wakeze wakamgeuza moyo. Maana ikawa, sulemani
alipokuwa mzee, wake zake wakamgeuza moyo wake, afuate miungu mingine, wala
moyo wake haukuwa mkamilifu kwa BWANA, Mungu wake, kama moyo wa Daudi baba
yake. Kwa kuwa sulemani akamfuata Ashtorethi, mungu mke wa Wasidoni na Milkomu,
chukizo la Waamoni. Sulemani akafanya yaliyo mabaya machoni pa BWANA, Wala
hakumfuata BWANA kwa utimilifu, kama Daudi baba yake. Sulemani akamjengea
kemoshi, chukizo la Wamoabi,mahali pajuu, katika mlima uliokabili Yerusalemu,
na Moleki, chukizo la wana wa Amoni. Na kadhalika ndivyo alivyowafanyia wake
zake wan chi za kigeni, waliofukiza uvumba, wakawatolea miungu yao dhabihu.Basi
BWANA akamghadhibikia sulemani kwa
sababu moyo wake umemgeuka, naye amemwachqa BWANA, Mungu wa Israel, aliye
mtokea mara mbili.
Kama
mfalme sulemani, alishindwa kuwageuza wanawake ambao alikatazwa asioe, tambua
hata wewe kama kijana endapo utakubali kumuoa au kuolewa na mtu asiye okoka
Mungu hukuacha.
2Kor 6:14-17, Msifungiwe nira pamoja na wasioamini, kwa jinsi isivyo
sawasawa; kwa maana pana urafiki gani kati ya haki na uasi? Tena pana shirika
gani kati ya haki na uasi ? Tena pana shirika gani kati ya haki giza? Tena
panaulinganifu gani kati ya kisto na Beliari? Au yeye aaminiye ana sehemu gani
pamoja na yeye asiyeamini?Tena pana mapatano gani kati ya hekalu la Mungu na
sanamu? Kwa maana sisi tu hekalu la Mungu aliye hai; kama Mungu alivyosema, ya
kwamba, Nitakaa ndani yao, na kati yao nitatembea, nami nitakuwa, nami nitakuwa
Mungu wao, nao watakuwa watu wangu. Kwa hiy,
Tokea kati yao, Mkatengwe nao, asema Bwana, Msiguse kitu kilicho
kichafu, Nami nitawakaribisha. Nitakuwa Baba kwenu, Nanyi mtakuwa kwangu
wanangu wa kiume na wa kike, asema Bwana Mwenyezi.
Bado
msisitizi kutoka kwa mtume paul kwa wakorintho ni kutochangamana na watu wasio
waaminio katika maswala ya ndoa na mambo yanayohusu kuabudu.
Waefeso 4:1-6, Kwa hiyo nawasihi, mimi niliye mfungwa katika Bwana, mwenende
kama inavyoustahili wito wenu mlioitiwa; kwa unyenyekevu wote na upole, kwa
uvumilivu, mkichukuliana katika upendo; na kujitahidi kuuhifadhi umoja wa Roho
mmoja, kama na mlivyoitwa katika tumaini moja la wito wenu. Bwana mmoja, imani
moja, ubatizo mmoja. Mungu mmoja, naye ni Baba wa wote , aliye juu ya yote na katika yote na ndani ya yote.
Ndugu
yangu kijana eneo hili kwa upande mwingine huwa ni gumu sana tena kama upo
kwenye mahusiano na mtu asiye okoka, ila nikutie moyo upo uwezekano wa kujitoa
katika kifungo hicho ambacho mwisho wa siku kitakuwa ni kikubwa Zaidi, kadri
somo litakavyo kuwa linaendelea jitahidi sana kufuatilia mfululizo huu, naamini
utapata maarifa mapya ambayo hukuwa nayo.
Counselor
Nicholaus Simon & Mch Gregoly David.
Viungo
katika mwili wa kristo.
Kwa msaada na ushauri.
piga:
0766 – 635382 / 0654 623 492.
whatsap
namba: 0654-623492.
pataufahamu@gmail.com
Ubarikiwe
sana na nakuomba nisaidie kushare kwa marafiki zako ili na wao wajifunze Neno
la MUNGU.
Post A Comment:
0 comments: