Shalom!!
Ni matumaini yetu kwamba kwa Neema nyingi sana za Bwana Yesu upo Salama na umepata Neema ya kuingia mwaka Mpya wa 2018 pamoja na familia yako nzuri.

Ni  Maombi yetu mbele za MUNGU katika mwaka 2018 ,ukawe mwaka wa kicheko ,Bwana akabariki kazi za mikono yako, Akupe afya njema na kukuepusha na kila ugonjwa , Kibali  cha Kiungu kiwe Juu yako.

Mwaka 2018 Bwana Yesu akawe mfadhili wako,wema wa Bwana ukufuate kwa siku  zote 365 za mwaka 2018.

Bwana Yesu akakuepushe na kila hila na mitego yote ya shetani na wajumbe wake wote, kila mtego watakao kutegea watanasa wenyewe,na kila shimo watakalo kuchimbia wataingia wenyewe.
Hakutakuwa na silaha yoyote itakafanyika Juu yako ikafanikiwa ,na pia usiwepo ulimi wowote utakao inuka kinyume nawe,

Damu ya Bwana Yesu ikanene mema  Juu yako na kila anayekuhusu au chochote kile .
Ulinzi wa Kiungu ukawe Juu yako, hautakufa kwa ajali, wala kwa magonjwa, wala kwa Bahati mbaya ,wala kwa uchawi ,wala kwa bunduki, UTAISHI Uyasimulie matendo makuu ambayo BWANA YESU atakufanyia katika mwaka huu wa 2018 kuanzia Leo tarehe 1/1/2018 mpaka Mwisho wa mwaka huu.

Tunakuombea malaika wema wa Bwana wakafanye kituo mahali popote utakapo kuwepo.
Tunakuombea baraka za Bwana Yesu zikakufate, na Habari njema zikuandame katika mwaka wote huu wa 2018.

Bwana Yesu akasimame upande wako daima na kuwa mchungaji wako katika mazingira yote utakayopita mwaka huu.

Neema nyingi sana za Bwana YESU zisikupungukie katika mwaka huu mzima wa 2018.
Zingatia sana.
Mahusiano yenye Afya kati yako na Bwana Yesu, Jitunze sana sana sana , usije ukamhuzunisha Roho Mtakatifu au usije ukamfanya kuzima ndani yako.
Bwana YESU Anakupenda sana .

Tunakuombea sana Utukufu wa Bwana uwe  Juu yako .
Ukabariwe kila uingiapo na utokapo.
Bwana yu pamoja nawe daima.

         Happy New Year 2018.

By.Pastor Gregory & Happy
Axact

Axact

Vestibulum bibendum felis sit amet dolor auctor molestie. In dignissim eget nibh id dapibus. Fusce et suscipit orci. Aliquam sit amet urna lorem. Duis eu imperdiet nunc, non imperdiet libero.

Post A Comment:

0 comments: