Counselor Nicholaus |
Ni
maombi yangu kwako, Mungu afungue ufahamu wako uweze kupata maarifa haya,
ambayo yawe msaada kwako binafsi na jamii inayo kuzunguka..
Amen.
MAELEZO YA DARASA HILI LA USHAURI.
Darasa
hili nimeliandaa, kwaajili ya kutoa utangulizi wa elimu ya ushauri juu ya kujua
kanuni za msingi na mbinu za kushauri zilizo bora.
MAKUSUDI YA DARASA HILI.
Ni
kutoa fursa kwa watu mbalimbali wenye wito na huduma hii, Waweze kujifunza
mbinu za msingi za kutumia katika kushauri kwa kiwango kizuri pasipo
ubabaishaji.
MALENGO YA DARASA HILI.
1.
Kupata uelewa wa Msingi wa maana ya ushuri.
2.
kupata uelewa wa msingi wa mbinu za kusaidia wakati wa kushauri.
3.
kubadilisha mtizamo wa watu juu ya elimu ya ushuri.
MAHITAJI YA DARASA.
1.
Ushiriki wako kikamilifu kwa kufatilia vipindi vyote.
2.
kijarida cha kuandikia. Hiki kitakusaidia kuandika baadhi ya vitu vya muhimu
kwako.
SEHEMU
YA KWANZA
UMUHIMU WA ELIMU YA USHAURI
1. Elimu
ya ushauri huliponya taifa na kuleta msaada mkubwa.
2. Ushauri
unasaidia kupambana na mambo yasiyofaa na kuleta wokovu katika maisha ya
mwanadamu.
3. Ushauri
unaleta njia ya kutokea.
4. Wanaotafuta
ushauri, hupata amani na furaha.
5. Mshauri
akitoa ushauri mbaya usiojenga afanya machukizo mbele za Mungu.
Unapokuwa
unahitaji msaada wakati wa shida, kuchanganyikiwa, tunapaswa kutumia maneno
yenye hekima ya Ki-Mungu ndani yake kwasababu Mungu ndiye mshauri wetu, kwa
urahisi kabisa kushauri ni kule kutembea katika misingi iliyo sahii chini ya
uongozi wa Mungu, pasipo Mungu kuhusika katika ushauri wowote, matokeo yake huwa
siyo mazuri..
Ushauri
ni nini?
Ni
matumizi ya ujuzi ulionao kwa makusudi kuwasaidia watu wengine kuweza kugundua
na kutekeleza masuluhisho katika matatizo yao. (Manthei, 1997)
Ni
mchakato ambao unajumuisha majibizano
kati ya mshauri na mshauriwa katika sehemu
maalum kwa nia ya kumsaidia mshauri kabadili tabia yake ili kuweza
kupatikana suluhisho la kutosheleza
linalohitajika.
-katika mazungumzo haya, mshauriwa anapaswa kujihisi
yuko salama. .
Kwasababu
kushauri huwa inarejea katika utaratibu wa kuwasaidia watu waweze kutatua
matatizo yao wenyewe.
Ushauri
huwa unawasaidia watu kuhakikisha kuwa wanafikia mafanikio yao binafsi (kwa
lengo la kuweza kumudu maisha yao ya baadae). Kwahiyo, mshauri anapaswa kuwa na
ujuzi unaotakiwa.
Ni mimi ndugu yako counselor Nicholaus Simon.
Kwa msaada zaidi na ushauri.
whatsap: 0654-623492
pataufahamu@gmail.com
Ubarikiwe sana Na nakuomba nisaidie kushare kwa marafiki zako ili wao wajifunze.
Kwa msaada zaidi na ushauri.
whatsap: 0654-623492
pataufahamu@gmail.com
Ubarikiwe sana Na nakuomba nisaidie kushare kwa marafiki zako ili wao wajifunze.
Post A Comment:
0 comments: