Counselor Nicholaus |
MABADILIKO
KATIKA USHAURI
Kushauri kunahusu
kubadilika. (Counseling is all about Change)
1. Inahusu watu
wanaotaka kubadilika.
2. Inahusu watu
wasiojua watabadilika kwa jinsi gani.
3. Inahusu watu
wanaohitaji msaada wa kubadilika .
4. Huduma ya ushauri
Inahusu watu wasiotaka mabadiliko pia.
5. Inahusu watu wasio
tayari kuacha mazingira yao mabaya ya sasa na kupokea msaada kutoka kwa
wengine.
MABADILIKO
Ni kuhusu watu ambao
wanataka kubadilika, watu ambao hawajui namna gani wabadilike, watu ambao
wanahitaji msaada wa kubadilika, watu ambao wanapingana na mabadiliko, na watu
ambao wameonekana kana kwamba hawawezi
kuacha mambo yao ya sasa na kukubali msaada wa wengine kubadilika. Washauri
huwa wanashughulikia na wale ambao wamezidiwa na hali za maisha yao au
mabadiliko, watu ambao hawajui namna ya kuweza kuendana au wanaweza kufanya
nini kuweza kubadilika. Pamoja na mkanganyiko na kutokufahamu watu ambao huwa
tunashauriwa huwa wanaishi katika dunia iliyo gubikwa na mabadiliko ya haraka
huwa yanaathiri maisha yao yote, mazingira ya kazi, huduma na jamii.
JINSI
YA KULETA MABADILIKO BINAFSI YANAYODUMU
1. Weka matarajio yako
binafsi ambayo yanaweza kufikika kuhusiana na muda kiasi gani utakao tumika (Mara nyingi vitu huwa vinachukua muda
mrefu kuliko ilivyofikiliwa.
2. Weka malengo
yanayoweza kufikika na yanayowezekana.
3. Weka matarajio kuwa
mabadiliko yatatokea (ingawa kwa kawaida huwa ni ngumu kuliko inavyo talajiwa)
4.Weka mazingatio
katika mafanikoa kuliko katika kushindwa, Hii inaweza kujumuisha kuweka takwimu
za mafanikio na kuandaa pongezi pale ambapo malengo yamefikiwa.
5.Tegemea kurudia
rudia, Lazima itajitokeza, panapokuwa upya maa moja baada ya kukamilisha kwa
hatua ya kwanza.
6. Kuwa mwangalifu na
hali zinazo shawishi na kuziepuka.
7. Pata msaada wa
kijamii, kupewa moyo na msukumo kutoka kwa mshauri au rafiki unaye mwamini ili
usiache hatua za kufanya ukiwa peke yako. Pale ambapo tunajaribu kufanya
mabadiliko pasipo kuwa na uangalifu wa kijamii ni rahisi kuacha utaratibu, bila
kuwepo kwa mtu mwingine ni rahisi kudanganya na kujikuta umefaulu kwa
kushindwa.
8. Zipatie
changamoto sababu za kushindwa.
Jambo hili huwa ni
rahisi pale ambapo mtu mwingine atakuwa
kahusiswa na akaweza kukosoa sababu zako za kushindwa au kurudia tena.
KWA
NINI MABADILIKO NI MAGUMU SANA.
Na kwanini watu
wanakataa kubadilika, hata pale ambapo wanasema kuwa wanataka? kuna sababu
nyingi, lakini zifuatazo ni miongoni mwa sababu amabazo ni maarufu sana. Huenda
ukaziona baadhi katika kazi yako ya kushauri. kwa wakati huu unaweza kuziona
hata kwako mwenyewe.
MABADILIKO
HUZUIWA KWASABABU ZIFUATAZO.
1. Huwa hawako tayari
kutoa kile ambacho ni salama, kinachojulikana, anakizoea.
2.Hawana uhakika kuwa
mabadiliko ni bora kuliko hali halisi.
3. Wanaogopa jinsi gani
maisha yatakavyo kuwa baada ya mabadiliko, kwa hakika huwa wanajisikia salama
kubakia pale walipokuwa, japo kuwa hawana furaha, kuliko kukubali kufanya
mabadiliko na kukabiliana na kile ambacho hukifahamu hujakizoea na
kinachoogopesha.
MBINU
ZA KULETA MABADILIKO YA KUDUMU.
Tunapo tilia maanani
ugumu huu, tunaweza kuhitimisha mabadiliko hayo hasa mabadiliko ya kudumu, je
ni karibu na kutokuwezekana kabisa. Lakini kuna ushindi wakutosha kwamba
mabadiliko ya kudumu yanawezekana, ukisha pata mazingira na hali sahihi.
1.
Utayari na kujitoa.
Mabadiliko ya kudumu
yanahitaji utayari wa mtu binafsi.
Utayari ndicho ''
kiungo muhimu katika kuharakisha mabadiliko yanayodumu.
Utayari na kujitoa
inahusu ni kwa kiasi gani mtu anataka mabadiliko.
Utayari unaonyesha ni
kwa kiasi gani mtu huyo ameshawishika na kukubali kupokea mabadiliko.
Utayari huonyesha ni
kwa kiasi gani mtu yupo tayari kudumisha hayo mabadiliko pale yatakapo tokea.
Kujiamini kupita kiasi
ni sumu ya Mabadiliko ya kudumu.
Mara nyingi watu wengi
hupenda mambo mengi yabadilike na huweza kufanya lolote ili mradi tu wafikie
malengo hayo. Kisha wanajisahau, Huwa wanafikiri kuwa wameshafika na kusahau
kutambua kuwa wanaweza kurudi tena hatua ya nyuma walikokuwa kwa urahisi
kabisa.
Ni sawa na mgonjwa wa
mareria aliyepewa dozi ya dawa akaambiwa kunywa vidinge 3 sasa na baada ya wiki
moja unakunywa vingine. Baada ya kunywa vile vidonge 3 na kujihisi kama
amepona anasahau na kuamua kutoendelea
na vile vidonge vingine 3 baada ya wiki moja mareria inarudi tena kali sana kuliko
ile ya mwanzo.
Kwa wao kujiamini
kupita kiasi ni adui wa mabadiliko ya kudumu.
2.
Malengo yanayofikika.
Mabadiliko yakudumu
yanahitaji kuweka malengo yanayoweza kutekeleza.
Hii ilisha tajwa hapo
awali lakini hakuna kinacho haribu juhudi za kutaka mabadiliko ya kudumu kuliko
kuweka malengo yale ambayo hayawezi kufikika.
Mabadiliko
yanahitaji malengo yenye ''mashiko''
Malengo ambayo yanaweza
kufikika huwa yako bayana na mahsusi kuliko ya jumla.
Malengo ya kudumu
yanapaswa kuwa sehemu ya maisha ya mhusika.
Malengo huwa yanadumu
muda mrefu kama mhusika anapata taarifa sahihi kuhusu maendeleo yake. Kwa mfano
kufanya vipimo vya uzito katika kituo cha kupunguza uzito kila wiki, inaweza
kukupa taarifa mahususi kuhusu jinsi gani uzito unapungua.
3.
Kuzuia kurudi Nyuma.
Mwanzo nilisema kuwa
kurudi nyuma huwa kunaweza kutokea katika mchakato wowote wa mabadiliko.
Hili ni jambo la
uhakika kabisa. Lakini kuna njia ya kupunguza jambo hili mpaka katika hali
ndogo sana kumsaidia mtu kupata nafuu na kuendelea wakati unapotokea kushindwa.
Yule anaye shauriwa anaweza kusaidiwa kuchambua kushindwa kuliko pita na
anawezaa kujua ni kitu gani kilichokuwa kimekosewa mpaka kumfanya kurudi nyuma
tena.
Na kuweza kujua kwa
jinsi gani makosa ya namna hii yanaweza kuepukwa hapo baadae ili mshauriwa
asirudi nyuma tena mara kwa mara.
Mshauriwa anapaswa
kufahamu kuwa kurudi nyuma sio jambo geni au baya ili kuwafanya wasikate tamaa
pale wanaposhindwa kufikia malengo.
Hakikisha
pia kuwa wanafahamu vile vile kuwa njia nzuri ya kufungua na kuendelea kurudia rudia kufanyia kazi
tabia njema ambayo unaitaka haraka iwezekanavyo.
Ni mimi ndugu yako counselor Nicholaus Simon.
Kwa msaada zaidi na ushauri.
whatsap: 0654-623492
pataufahamu@gmail.com
Ubarikiwe sana Na nakuomba nisaidie kushare kwa marafiki zako ili wao wajifunze.
Kwa msaada zaidi na ushauri.
whatsap: 0654-623492
pataufahamu@gmail.com
Ubarikiwe sana Na nakuomba nisaidie kushare kwa marafiki zako ili wao wajifunze.
Post A Comment:
0 comments: