Afya ya Akili yako ni muhimu sana kwa sababu inaweza kuathiri afya yako ya kimwili na ustawi wako wote. Ikumbukwe kuwa asilimia kubwa ya wagonjwa ambao wamelazwa hospital na ambao wapo majumbani  tatizo kubwa haswa huwa na tatizo la afya ya akili inayochangia watu kupatwa na magonjwa mbalimbali katika sehemu za miili yao.

Afya yako ya akili inahusiana na jinsi unavyojihisi na akili yako inavyofanya kazi. Afya yako ya akili ni muhimu sana kwa sababu inaweza kuathiri afya yako ya kimwili na ustawi wako wote.

Wakati mtu ana shida ya afya ya akili, inamaanisha ustawi wake wa akili hauko sawa kama vile mwili wako unapoumia. Kuna sababu nyingi ambazo watu hupata masuala ya afya ya akili. Wanaume wengine huzaliwa katika hatari kubwa zaidi na wengine wana hatari baada ya kukabiliana na mambo kama msongo wa mawazo au shida.

Wakati mwingine matatizo ya afya ya akili yanaweza kuwa madogo na kuisha kwa urahisi. Nyakati nyingine yanaweza kuwa mabaya na kufanya iwe vigumu kwa watu kufanya kazi kama kawaida.

Hebu jiulize, je! Upo salama?

Huwa ukiwa mwenyewe unawazaga nini, umezungukwa na watu wa aina gani na huwa mnazungumza Nini, maana mazungumzo mabaya huharibu tabia njema, na huwa unasikiliza vitu gani na huwa unasomaga vitu gani. Ukishamaliza kujiuliza jipime je, uko salama katika akili yako? Maana watu wengi sana wameharibikiwa kiakili kwa kuwa na makundi mabaya ya marafiki,kwa kusikiliza simulizi mbaya zisizo na mafundisho, kuona vitu vibaya Kama picha au video za  ngono, video za wavuta bangi na sigara, video za uhalifu, kuwafumania wapenzi wao, wazazi wao na kujiskia vibaya, ndugu zao, kuteswa na wanaokaa nao(Kama kusema vibaya, kudharauliwa n.k)

Kutokuwa na Afya ya akili kunachangia sana na wewe mwenyewe jinsi unavyojiona,unavyojichukulia n.k.Ajionavyo mtu nafsini mwake ndivyo alivyo,unavyojiwazia ndivyo utakavyokuwa.Jitahidi sana kuwaza yaliyo mema,yaliyo mazuri ili kusaidia akili yako isiathirike.

Karibu katika AFYA YA  AKILI, pia tunatoa ushauri kwa kila changamoto zozote zinazo kukabili

    Counselor Nicholaus & Jane .
    Kwa msaada na ushauri.
    Kwa msaada zaidi na ushauri. 
    Mawasiliano: 0766 – 635 382 / 0677 880 199
    Whatsap namba: 0755 556 661
    Email: pataufahamu@gmail.com
Axact

Axact

Vestibulum bibendum felis sit amet dolor auctor molestie. In dignissim eget nibh id dapibus. Fusce et suscipit orci. Aliquam sit amet urna lorem. Duis eu imperdiet nunc, non imperdiet libero.

Post A Comment:

0 comments: