MIONGONI MWA MAKOSA YANAYOFANYWA NA VIJANA KABLA YA KUELEKEA NDOA TAKATIFU.
Counselor Nicholaus Simon.

Usijiunganishe na mtu asiye okoka. (Wala usimsaidie Mungu kazi/kuokoa)
nami nitakuapisha kwa BWANA, Mungu wa mbinguni, na Mungu wa Nchi, kwamba hutamtwalia mwanangu mke  katika binti za Wakaani ambao nakaa kati yao; [Mwanzo 24:3]
kama kijana uliye okoka ni kosa kubwa kuoa/kuolewa na mtu asiye okoka, ukisoma Andiko hilo katika Mwanzo, utaona jinsi gani Mungu alipiga marufuku kwa mwisrael kuoa/kuolewa na mkaanani , katika maisha yetu ya sasa Mtu yeyote akiokoa naye ni mwisrael na lile Agano linaendelea kwake ,na mkaanani ni sawa na mtu asiye okoka.

Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu; ninyi mliokuwa kwanza si taifa, bali sasa ni taifa la Mungu; mliokuwa hamkupata rehema, bali sasa mmepata rehema.[1petro 2:9-10]
Kwahiyo mkristo yeyote aliye okoka ni mwisrael. Kama kijana uliye okoka kuoa/kuolewa na mkaanani mtu asiye okoka ni kosa na haitakiwi.
Kuna madhara makubwa pale kijana aliye okoka anapokuwa ameolewa/kuoa na kijana asiye okoka. Mfalme sulemani akawapenda wanawake wengi waeni, pamoja na binti yake Farao, wanawake wa Wamoabu, na wa waamoni, na wa waedomi, na  wa sidoni, na wa Wahiti, na wa mataifa BWANA aliyo waambia  wana wa Israeli, Msiingie kwao, wala wasiingie kwenu; kwa kuwa hakika wataigeuza mioyo yenu kuifuata miungu yao. Sulemani akaambatana nao kwa kuwapenda.Akawa na wake mia saba binti za kifalme,na Masuria mia tatu; nao wakeze wakamgeuza moyo. Maana ikawa, sulemani alipokuwa mzee, wake zake wakamgeuza moyo wake , afuate miungu mingine, wala moyo wake haukuwa mkamilifu kwa BWANA, Mungu wake, kama moyo wa Daudi baba yake. Kwa kuwa sulemani akamfuata Ashtorethi, mungu mke wa Wasidoni na Milkomu, chukizo la Waamoni. Sulemani akafanya yaliyo mabaya machoni pa BWANA, Wala hakumfuata BWANA kwa utimilifu, kama Daudi baba yake. Sulemani akamjengea kemoshi, chukizo la Wamoabi,mahali pajuu, katika mlima uliokabili Yerusalemu, na Moleki, chukizo la wana wa Amoni. Na kadhalika ndivyo alivyowafanyia wake zake wan chi za kigeni, waliofukiza uvumba, wakawatolea miungu yao dhabihu.Basi BWANA akamghadhibikia  sulemani kwa sababu moyo wake umemgeuka, naye amemwachqa BWANA, Mungu wa Israel, aliye mtokea mara mbili. [1Wafalme 11:1-8]
Kama mfalme sulemani, alishindwa kuwageuza wanawake ambao alikatazwa asioe, Tambua hata wewe kama kijana endapo utakubali kumuoa/kuolewa na mtu asiye okoka Mungu hukuacha.
Msifungiwe nira pamoja na wasioamini, kwa jinsi isivyo sawasawa; kwa maana pana urafiki gani kati ya haki na uasi? Tena pana shirika gani kati ya haki na uasi ? Tena pana shirika gani kati ya haki giza? Tena panaulinganifu gani kati ya kisto na Beliari? Au yeye aaminiye ana sehemu gani pamoja na yeye asiyeamini?Tena pana mapatano gani kati ya hekalu la Mungu na sanamu? Kwa maana sisi tu hekalu la Mungu aliye hai; kama Mungu alivyosema, ya kwamba, Nitakaa ndani yao, na kati yao nitatembea, nami nitakuwa, nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu. Kwa hiy,  Tokea kati yao, Mkatengwe nao, asema Bwana, Msiguse kitu kilicho kichafu, Nami nitawakaribisha. Nitakuwa Baba kwenu, Nanyi mtakuwa kwangu wanangu wa kiume na wa kike, asema Bwana Mwenyezi.  [2Kor 6:14-17].
Bado msisitizi kutoka kwa  mtume paul kwa wakorintho ni kutochangamana na watu wasio waaminio katika maswala ya ndoa na mambo yanayohusu kuabudu.
Kwa hiyo nawasihi, mimi niliye mfungwa katika Bwana, mwenende kama inavyoustahili wito wenu mlioitiwa; kwa unyenyekevu wote na upole, kwa uvumilivu, mkichukuliana katika upendo; na kujitahidi kuuhifadhi umoja wa Roho mmoja, kama na mlivyoitwa katika tumaini moja la wito wenu. Bwana mmoja, imani moja, ubatizo mmoja. Mungu mmoja, naye ni Baba wa wote , aliye juu ya yote na katika yote na ndani ya yoye. [waefeso 4:1-6.
Ni mimi ndugu yako Counselor Nicholaus Simon.
Kiungo katika mwili wa kristo.
Kwa msaada na ushauri.
whatsap 0654-623492.
pataufahamu@gmail.com

Ubarikiwe sana Na nakuomba nisaidie kushare kwa marafiki zako ili na wao wajifunze Neno la MUNGU. 


Axact

Axact

Vestibulum bibendum felis sit amet dolor auctor molestie. In dignissim eget nibh id dapibus. Fusce et suscipit orci. Aliquam sit amet urna lorem. Duis eu imperdiet nunc, non imperdiet libero.

Post A Comment:

0 comments: