Afya ya Akili yako ni muhimu sana kwa sababu inaweza kuathiri afya yako ya kimwili
na ustawi wako wote. Ikumbukwe kuwa asilimia kubwa ya wagonjwa ambao wamelazwa
hospital na ambao wapo majumbani tatizo kubwa haswa huwa na tatizo la
afya ya akili inayochangia watu kupatwa na magonjwa mbalimbali katika sehemu za
miili yao.
Afya
yako ya akili inahusiana na jinsi unavyojihisi na akili yako inavyofanya kazi.
Afya yako ya akili ni muhimu sana kwa sababu inaweza kuathiri afya yako ya
kimwili na ustawi wako wote.
Wakati
mtu ana shida ya afya ya akili, inamaanisha ustawi wake wa akili hauko sawa
kama vile mwili wako unapoumia. Kuna sababu nyingi ambazo watu hupata masuala
ya afya ya akili. Wanaume wengine huzaliwa katika hatari kubwa zaidi na wengine
wana hatari baada ya kukabiliana na mambo kama msongo wa mawazo au shida.
Wakati
mwingine matatizo ya afya ya akili yanaweza kuwa madogo na kuisha kwa urahisi.
Nyakati nyingine yanaweza kuwa mabaya na kufanya iwe vigumu kwa watu kufanya
kazi kama kawaida.
Hebu jiulize, je! Upo salama?
Huwa
ukiwa mwenyewe unawazaga nini, umezungukwa na watu wa aina gani na huwa
mnazungumza Nini, maana mazungumzo mabaya huharibu tabia njema, na huwa
unasikiliza vitu gani na huwa unasomaga vitu gani. Ukishamaliza kujiuliza
jipime je, uko salama katika akili yako? Maana watu wengi sana wameharibikiwa
kiakili kwa kuwa na makundi mabaya ya marafiki,kwa kusikiliza simulizi mbaya
zisizo na mafundisho, kuona vitu vibaya Kama picha au video za ngono, video za wavuta bangi na sigara, video
za uhalifu, kuwafumania wapenzi wao, wazazi wao na kujiskia vibaya, ndugu zao,
kuteswa na wanaokaa nao(Kama kusema vibaya, kudharauliwa n.k)
Kutokuwa
na Afya ya akili kunachangia sana na wewe mwenyewe jinsi
unavyojiona,unavyojichukulia n.k.Ajionavyo mtu nafsini mwake ndivyo
alivyo,unavyojiwazia ndivyo utakavyokuwa.Jitahidi sana kuwaza yaliyo
mema,yaliyo mazuri ili kusaidia akili yako isiathirike.
Post A Comment:
0 comments: