SEMINA YA NENO LA MUNGU NA MWL MWAKASEGE.
UWANJA WA TANGAMANO TANGA 5 JUNE 2017
SOMO MBINU ZA KUOMBEA NDOTO ILI USIKWAME KIMAISHA.
Siku ya Kwanza.
Hii ni semina ya neno la Mungu kwa hiyo kaa mkao wa kujifunza. Hakikisha unakuwa na Biblia na daftari yako. Uwe kama watu wa Beroya waliokuwa wanayachunguza maandiko.
Lengo: Kuimarisha uhusiano wako na Mungu katika Kristo Yesu.
Lengo la kukutangazia somo si suala la kufundisha kuhusu ndoto bali ni kutumia somo la Ndoto ili kuimarisha uhusiano wako na Mungu katika Kristo Yesu uwe mzuri
Mungu hana dini na hili somo halina dini haijalishi wewe ni mkristo sio mkristo unaota ndoto. Kwa hiyo fuatilia hili somo vizuri kabisa na Mungu akusaidie kujua namna ya kuombea juu ya ndoto unazoota.
NDOTO INA VYANZO VISIVYOPUNGUA VINNE
Ndoto ninayosema hapa si ile vision yaani kile unachokiona kwa ajili ya hali yako ya baadae. Nazungumza ndoto unayoota usiku ukiwa umelala.
1.CHANZO CHA KWANZA NI MUNGU
Kwa kuwa Mungu hunena mara moja, Naam, hata mara ya pili, ajapokuwa mtu hajali.   Katika ndoto, katika maono ya usiku, Usingizi mzito uwajiliapo watu, Katika usingizi kitandani;AYU. 33:14-15 SUV
Mungu huleta Ndoto mara moja au mara mbili na utaona akirudia hata zaidi ya mara moja japo watu hawajali na wengine husema ni ndoto tu.
  1. CHANZO CHA PILI NI SHETANI.
Kukizuka katikati yako nabii, au mwotaji wa ndoto, akikutolea ishara au ajabu, ikatukia hiyo ishara au hiyo ajabu aliyokuambia akisema, Na tuifuate miungu mingine usiyoijua, tuitumikie hiyo; wewe usiyasikize maneno ya nabii yule, au yule mwotaji wa ndoto, kwa kuwa BWANA, Mungu wenu, yuawajaribu, apate kujua kwamba mwampenda BWANA, Mungu wenu, kwa mioyo yenu yote na roho zenu zote.KUMBU KUMBU. 13:1-3
Si ndoto zote anazoota mtu huwa zinatoka kwa Mungu bali pima vizuri kwa neno la Mungu kile ulichoambiwa kutoka katika ndoto hizo  haijalishi kimetokea kiasi gani,usitishike sana bali angalia sana matokeo yake yaani mwisho wake unakupeleka wapi
Angalia kama hicho kilichosema kama kinakutoa kwenye maombi au kukuweka mbali na Mungu.  Shetani naye anaweza sema vitu na vikatokea  kwa hiyo isikupe shida ila pima na neno la Mungu utajua ukweli.
3.SHUGHULI NYINGI.
Kwa maana ndoto huja kwa sababu ya shughuli nyingi; na sauti ya mpumbavu kwa njia ya wingi wa maneno.
MHUBIRI. 5:3.
Mtiririko wa shughuli nyingi huleta ndoto za aina fulani. Na shughuli nyingi kwa Biblia maana yake ni Naye aliyepandwa penye miiba, huyo ndiye alisikiaye lile neno; na shughuli za dunia, na udanganyifu wa mali hulisonga lile neno; likawa halizai.Mathayo 13:22
Maana yake ni masumbufu ambayo hayapo katika mapenzi ya Mungu.  Mungu anatumia ndoto kukuambia kuwa hukutumia vizuri siku yako na hujamzalia Mungu matunda ndio maana Mungu atasema na wewe kwa njia ya ndoto ili kukuonesha kuwa unavyotumia muda wako si sawa.
4.MAZINGIRA YA KIROHO YA MAHALI UNAPOLALA
_Yakobo akatoka Beer-sheba, kwenda Harani. Akafika mahali fulani akakaa huko usiku kucha, maana jua lilikuwa limekuchwa; akatwaa jiwe moja la mahali pale akaliweka chini ya kichwa chake, akalala usingizi pale pale. Akaota ndoto; na tazama, ngazi imesimamishwa juu ya nchi, na ncha yake yafika mbinguni. Tena, tazama, malaika wa Mungu wanapanda, na kushuka juu yake. Na tazama, BWANA amesimama juu yake, akasema, Mimi ni BWANA, Mungu wa Ibrahimu baba yako, na Mungu wa Isaka; nchi hii uilalayo nitakupa wewe na uzao wako. Na uzao wako utakuwa kama mavumbi ya nchi, nawe utaenea upande wa magharibi, na mashariki, na kaskazini, na kusini; na katika wewe, na katika uzao wako, jamaa zote za dunia watabarikiwa. Na tazama, mimi nipo pamoja nawe, nitakulinda kila uendako, nami nitakuleta tena mpaka nchi hii, kwa maana sitakuacha, hata nitakapokufanyia hayo niliyokuambia.   Yakobo akaamka katika usingizi wake, akasema, Kweli BWANA yupo mahali hapa, wala mimi sikujua. Naye akaogopa akasema, Mahali hapa panatisha kama nini! Bila shaka, hapa ni nyumba ya Mungu, napo ndipo lango la mbinguni.
MWANZO. 28:10-17_
Sasa fikiria hapa Yakobo alilala mahali ambapo pana miungu mingine maana tunaona alipolala Mungu wa eneo lile alijifunua katika Ndoto.  Na yule Mungu akasema mimi ni Mungu wa baba yako na akasema atamfuatilia kila mahali.
Sasa geuza upande wa pili. Mtu kajenga hapo ambapo kuna madhabahu ya miungu au  kaweka kitu kibaya na wewe hujajua hata namna kuombea eneo unalola maana kuna vitu vingine ni vigumu na angalia namna ndoto unazoota hapo ukilala ( kama ni nyumba uliyopanga au uliyonunua au nyumba ya kulala wageni). Angalia aina ya ndoto unazoota ukilala hapo utajua hiki ninachokuambia
Mtu mmoja alisema Mwalimu napata shida kulala kwa sababu ndoto ninazoota ni ngumu. Na alipokuwa anaomba Mungu  amsaidie  ili kumfanikisha, akilala hapo nyumbani kwake usiku alikuwa anaona nyoka kwenye ndoto. Na saa nyingine akitaka kuingia katika baadhi ya vyumba katika nyumba yake anaona kama kuna mtu anamzuia kuingia na akuchungulia katika chumba alichotaka kuingia anaona nyoka kajiviringisha hapo  kwa hiyo haingii katika hicho chumba maana nyoka anatumika kama zuio kwenye hicho chumba.
Na alikuwa hajui maana yake nini, nikamuuliza  hii nyumba ulijenga au ulinunua akasema nilinunua na haikukaliwa na watu muda mrefu kwa hiyo nikamuambia namna ya kuomba na akaomba na ile shida yake ikatoweka siku hiyo hiyo.
MAENEO MUHIMU MATATU.
  1. Kuombea Ndoto zile ambazo umeota na usingependa yatokee kama ulivyoota.
Unaombaje….
Si kila  unachoota lazima kitokee kama unajua maandiko unaweza zuia kisitokee.
Mimi, Nebukadreza, nalikuwa nikistarehe katika nyumba yangu, nikisitawi katika nyumba yangu ya enzi. Nikaota ndoto iliyonitia hofu; mawazo niliyokuwa nayo kitandani mwangu, na njozi za kichwa changu, zikanifadhaisha. Basi nikatoa amri kwamba wenye hekima wote wa Babeli, waletwe mbele yangu, ili kunijulisha tafsiri ya ndoto ile. Ndipo wakaingia waganga, na wachawi, na Wakaldayo, na wanajimu; nikawahadithia ile ndoto; wao wasiweze kunijulisha tafsiri yake. Bali hatimaye Danieli akaingia mbele yangu, ambaye jina lake ni Belteshaza, kwa kufuata jina la mungu wangu; tena ndani yake inakaa roho ya miungu watakatifu; nikamhadithia ile ndoto, nikisema,DANIEL. 4:4-8
Wale wachawi wakashindwa kutafsiri ndoto ndio maana jifunze  kutotafuta tafsiri yake  nje ya neno la Mungu bali fuatilia katika biblia .
Ile miaka ya 85 / 86 na Mungu aliposema na Mimi kwa njia ya ndoto  na zilikuwa zinakuja miaka ile ya 82 /83 (nilikuwa bado sijaokoka) na nilikuwa naenda kwa waganga kutafuta tafsiri na nilikuwa chuo kikuu. Na walitafsiri  wanavyojua wenyewe katika miungu yao  na hawakunipeleka kwenye tafsiri halisi kama  Mungu   alivyo maanaisha.
Angalia tena mstari wa 17    Hukumu hii imekuja kwa agizo la walinzi, na amri hii kwa neno la watakatifu; kusudi walio hai wapate kujua ya kuwa Aliye juu anatawala katika ufalme wa wanadamu, naye humpa amtakaye, tena humtawaza juu yake aliye mnyonge.DAN. 4:17
Sasa ile ndoto iliishia kutangaza hukumu ile hukumu iliyotangazwa ilikuwa kwa nyakati saba tunaweza sema kwa miaka 7. Swali la kujiuliza  je kwani ilikuwa lazima itokee? Maana tunaona Nebukadreza akiondolewa kwenye nafasi.
Kama unasoma Biblia yako vizuri ilikuwa si lazima itokee maana kuna vitu kama vitatu hivi unaviona hapo
1.Aliambiwa kwanini adhabu imekuja (hakumpa Mungu heshima) kwa hiyo alihitaji kutambua tu na kutoa heshima kwa Mungu.
2.Mstari wa 26-27
Na kwa kuwa waliamuru kukiacha kisiki cha shina lake; ufalme wako utakuwa imara kwako, baada ya wewe kujua ya kuwa mbingu ndizo zinazotawala. Kwa sababu hiyo, Ee mfalme, shauri langu lipate kibali kwako; ukaache dhambi zako kwa kutenda haki, ukaache maovu yako kwa kuwahurumia maskini; huenda ukapata kuzidishiwa siku zako za kukaa raha.DAN. 4:26-27
Na ile Ndoto ilimwambia na kitu cha kufanya ili asiingie kwenye shida na ili jambo  lisitokee lile lilotabiriwa kwenye ndoto.
Kulikuwa na faida gani akapokea tafsiri na kupuuuzia ujumbe  uliokuwemo kwenye ndoto.
Watu wengi sana wanapokea tafsiri na wanapuuzia ujumbe.  Hawafuatilii kilichomo ndani ya ndoto.
3.Hayo yote yakampata mfalme Nebukadreza. Baada ya miezi kumi na miwili, alikuwa akitembea ndani ya jumba la kifalme katika Babeli.DAN. 4:28-29
Mungu alimpa miezi 12 ili kutambua mambo yale mawili yaani kutambua kuwa Mungu  ndiye anayetawala na kufuata ushauri aliopewa na Daniel.
Na mambo yote yaliyotokea ni kwa sababu alipuuzia ujumbe uliokuwa kwenye ndoto  alyopewa na Mungu.
Nebukadreza alikuwa mtumishi wa Mungu  kama askari magereza wa kuwafunga wana wa Israel miaka 70 na apewe na vyombo vya hekaluni ili avitunze
Baada ya miaka 70 Mungu alikuwa anadai na vyombo alivyotakiwa kutunza. Na mtoto wake Nebukadreza alivunja mashart na ndio maana alipigwa Mene mene ….  kiti cha enzi cha Nebukadreza kilikuwa na pingu kwa sababu kilikuwa kiti cha askari magereza.
Kwa hiyo katika siku kadhaa tutajifunza  namna ya mambo haya. Na nia ya Mungu sio kukupeleka jela anakupa taarifa ili huenda ukabadilika na ukabadilisha msimamo wako ili utende mema.
Katika Daniel 3   Nebukadreza unaona  alipewa na Mungu   nafasi ya kuwa mfalme na alitengeneza sanamu. Mungu alisema naye kwa njia ya ndoto  kuwa Nebukadneza umeenda mbali unahitaji kutengeneza (sura ya nne) na Mungu anasema nao kwa njia ya ndoto lakini wengi sana wanapuuzia. Wanasema ni ndoto tu ndoto tu. Hakikisha hufanyi kosa la aina hiyo.
  1. YALE ULIYOOTA YAMETOKEA KAMA ULIVYOOTA LAKINI UNATAKA KUYABADILI YASIENDELEE KAMA YALIVYOTOKEA.
Hayo yote yakampata mfalme Nebukadneza. Baada ya miezi kumi na miwili, alikuwa akitembea ndani ya jumba la kifalme katika Babeli. Mfalme akanena, akasema, Mji huu sio Babeli mkubwa nilioujenga mimi, uwe kao langu la kifalme, kwa uwezo wa nguvu zangu, ili uwe utukufu wa enzi yangu? Hata neno lile lilipokuwa katika kinywa cha mfalme, sauti ilikuja kutoka mbinguni, ikisema, Ee mfalme Nebukadneza, maneno haya unaambiwa wewe; Ufalme huu umeondoka kwako. Nawe utafukuzwa mbali na wanadamu, na makao yako yatakuwa pamoja na wanyama wa kondeni; utalishwa majani kama ng’ombe, na nyakati saba zitapita juu yako, hata utakapojua ya kuwa Aliye juu ndiye anayemiliki katika ufalme wa wanadamu, naye humpa amtakaye, awaye yote. Saa iyo hiyo jambo hilo likatimizwa, likampata Nebukadneza; alifukuzwa mbali na wanadamu, akala majani kama ng’ombe, na mwili wake ulilowa maji kwa umande wa mbinguni, hata nywele zake zikakua, zikawa kama manyoya ya tai, na kucha zake kama kucha za ndege.   Hata mwisho wa siku hizo, mimi, Nebukadneza, nikainua macho yangu kuelekea mbingu, fahamu zangu zikanirudia; nikamhimidi Yeye aliye juu, nikamsifu na kumheshimu Yeye aishiye milele; kwa maana mamlaka yake ni mamlaka ya milele, na ufalme wake hudumu toka kizazi hata kizazi; na watu wote wanaokaa duniani wamehesabiwa kuwa si kitu, naye hufanya kama atakavyo, katika jeshi la mbinguni, na katika hao wanaokaa duniani; wala hapana awezaye kuuzuia mkono wake, wala kumwuliza, Unafanya nini wewe? Basi wakati uo huo fahamu zangu zikanirudia, na kwa ajili ya utukufu wa ufalme wangu, enzi yangu na fahari yangu zikanirudia; na mawaziri wangu, na madiwani wangu, wakaja kunitafuta; nami nikathibitika katika ufalme wangu, nikaongezewa enzi kupita kiasi. Basi mimi, Nebukadneza, namhimidi Mfalme wa mbinguni, namtukuza na kumheshimu; maana matendo yake yote ni kweli, na njia zake ni za adili; na wale waendao kwa kutakabari, yeye aweza kuwadhili.DAN. 4:28-37
Ina maana alikuja kuwa kichaa na alipewa taarifa mwaka mzima na ile hukumu ilimpata na alifungwa porini.(sababu kuu alipuuzia ndoto aliyoambiwa)
Na kulikuwa hamna sababu ya kukaa nyakati saba  maana aliambiwa tu hadi atakapotambua ina maana asingetambua hizo nyakati, miaka ingeongezeka ya kukaa jela ( porini) na angetambua mapema ina maana hizo nyakati zingepungua.  Katika kipindi hiki cha agano jipya ni bora sana maana hamna sababu za kukaa utumwani au jela miaka 7 wakati una nafasi ya kupunguza au kuombewa kufutiwa  hicho kipindi.
Fikiria Nebukadneza   hana uwezo wa kujiombea mwenyewe  je watu wake wa karibu kwanini hawakuomba kwa ajili yake?.. omba kwa Roho  Mtakatifu atajua umuombee kwa namna gani. Angalia
Yakobo 5:15 Na kule kuomba kwa imani kutamwokoa mgonjwa yule, na Bwana atamwinua; hata ikiwa amefanya dhambi, atasamehewa.
Kwa hiyo unaweza ukaomba toba kwa ajili ya mtu mwingine hata kama yeye hataki kufanya toba ila kwa sababu wewe umeomba Mungu atakusikia na kumsamehe. Na hii ndio nafasi ya kikuhani ndani ya kanisa na kuomba kwa kanisa kama kuhani  ili mwenye dhambi aponywe na asamehewe.
A.Kwa hiyo kama Daniel angeweza omba kwa imani kama Yakobo 5:15 uwe na uhakika Nebukadneza   angetoka mapema kwenye adhabu.
Lakini sijajua kwanini Daniel hakumuombea Nebukadneza  .  Katika Biblia sijaona katazo lolote ila Samwel aliambiwa asimuombee Sauli *Bwana akamwambia Samweli, Hata lini utamlilia Sauli, ikiwa mimi nimemkataa asiwamiliki Israeli?*1 Samweli 16:1a
Ila tunaona Daniel akitoa  Ushauri kwa Nebukadneza   lakini hakufanya maombi ya rufaa. Kwa  mwombaji yoyote  lazima ajue namna ya kutumia neno la Bwana kama sheria kwenda  nalo kwa Mungu kwa ajili ya kukata rufaa ili utoke kwenye adhabu.
B.NJIA NYINGINE NAMNA YA KUFANYA
26 Kadhalika Roho naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa.
Warumi 8 :26
27 Na yeye aichunguzaye mioyo aijua nia ya Roho ilivyo, kwa kuwa huwaombea watakatifu kama apendavyo Mungu.
Warumi 8 :27
Mstari wa 26 ni wa wewe kujiombea wewe mwenyewe na mstari wa 27 wa namna ya kuwaombea wengine.
  1. KUOMBA KWA KUSIMAMIA KUSUDI LA MUNGU.
Angalia Warumi 8: 28 Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake.
Kwa hiyo Daniel angeomba kwa Mungu juu ya kusudi alilomsimamisha Nebukadneza   kwa nafasi yake. Na kama unaomba juu ya kusudi la Bwana.. na katika matendo ya mitume tunaona  Kwa maana Daudi, akiisha kulitumikia shauri la Mungu katika kizazi chake, alilala, akawekwa pamoja na baba zake, akaona uharibifu.Matendo ya Mitume 13:36
Ina maana hakulisimamia kusudi la kwake bali alisimamia kusudi la Bwana. Hujiulizi kwanini Sauli alifukuzwa kazi na aliendelea kupata mshahara wake na kwanini Nebukadneza hakufukuzwa moja kwa moja. Daniel angeendelea kuomba na Mungu angeweza msamehe Nebukadneza
22 Na kama siku hizo zisingalifupizwa, asingeokoka mtu ye yote; lakini kwa ajili ya wateule zitafupizwa siku hizo.
Mathayo 24 :22
Watwule ni waliotengwa kwa ajili ya kusudi la Mungu, kutengwa maana yake kuweka maalum au wakfu kwa ajili ya kazi ya Mungu  (kusudi) kwa hiyo ukiomba kufuata kusudi la Mungu utaona hata shetani kama alikusudia kukukwamisha Mungu atakupromote.
Mteule anayesimia kusudi la Bwana utaona Mungu anamsaidia kwa hiyo shetani asikutishe ukiona umechafuka nenda katafute damu ya Yesu kukusafisha. Akikuangusha inuka.endelea mbele.. usishindwe na shetani pambana hadi mwisho.
Mtu mmoja alinijia na kusema  alipokuwa anamuomba Mungu ili amfanikishe basi aliota ndoto na akaona yupo nyumbani kwao na katika uwanja wa kwao  mara akamwona nyoka kasimama usawa wake na alijaribu kumkemea kwa jina la Yesu lakini akawa haondoki na Mara akamuuma kidole chake na alipoamka toka usingizini  akaona kidole chake kinatoa damu. Na kesho yake alienda kanisani kwake maana alikuwa kaokoka na alipoulizwa na mchungaji wake hata kabla hajamiliza kueleza akaanguka chini  wakakemea pepo lilitoka pepo la mauti  lakini baada ya pale uchumi wake ukawa mbaya sana na kila alipokuwa anapanga nyumba alikuwa anafukuzwa.
Akaniuliza sasa hapa Mwakasege ndio nafanyeje sasa.  Nilielewa moja kwa moja unapoona umetumia jina la Yesu  unashindwa hakikisha damu ya Yesu inafanya kazi kwanza kabla ya jina la Yesu.  Damu ya Yesu ndio ilifunuliwa kwanza maana jina la Yesu ni la agano kwa hiyo ukiona kitu katika ulimwengu wa roho kimetokea hakijakaa sawa usijaribu kukemea kama hauko sawa sawa bali tubu kwanza.( kama hujakaa vizuri na Mungu wako)
Kaangalie kwa wana wa Skewa walikemea pepo lakini walishindwa na pepo liliwavuruga sawa sawa. Walikuwa hawanajulikani katika ulimwengu wa Roho maana unapewa authority na damu ya Yesu kutumia jina la Yesu. Wenyewe walikuwa hawana hiyo authority siku hiyo ya kutumia jina la Yesu
Na Mungu  alikuwa anamuambia kuwa kuna kitu cha kushugulikia  ambacho hakijakaa sawa sawa. Na japo aliombewa ila walisahau kuondoa  ile sumu ambayo iliingia na yule nyoka maana ilikuwa ni sumu ya Kiroho ndio maana iliua uchumi wake na kumletea roho ya kukataliwa.
  1. KUOMBEA NDOTO AMBAZO UNALETEWA TAARIFA ZA MAMBO YAJAYO AMBAYO UNAHITAJI KUJIANDAA NAYO NA HUWEZI KUYABADILI.
Mwanzo 41:1-37  Ndoto za farao za masuke saba na ng’ombe saba. Yananza masuke mazuri yanaliwa na mabaya na ng’ombe hivyo hivyo.
Wachawi walishindwa kutoa tafsiri na Yusufu ndio alikuja kutoa tafsiri  Na ndoto ya Farao kwa vile ilivyokuja mara mbili, ni kwa sababu neno hilo Mungu amelithibitisha, na Mungu atalitimiza upesi.MWANZO. 41:32 .
Sababu ya kuleta ndoto mara mbili Mungu amelikusudia ili kulitimiza kwa hiyo yalihitajika maandalizi. Ya kujiandaa na alikwambia na kitu cha kufanya.
Ndoto kama hiyo uwe na uhakika kuna maandalizi ya muhimu unayotakiwa kuyafanya ili uvuke hapo.
Farao alitii na hakupuuzia, maana nae alitaka kupuuzia kwa kusema ni ndoto tu . Basi Farao akaamka, kumbe! *Ni ndoto tu.*MWANZO. 41:7b
Alitaka kudharau lakini Mungu alimuongezea kitu kingine  Hata asubuhi roho yake ikafadhaika; akapeleka watu kuwaita waganga wote wa Misri, na watu wote wenye hekima walioko. Farao akawahadithia ndoto yake, wala hakuna aliyeweza kumfasiria Farao mambo hayo.MWANZO. 41:8
Ndipo alianza kufuatilia.
Kuna watu wanaohitaji  kufanikiwa na wanaota wako shuleni  unakuta mtu yuko chuo kikuu ila anaota yuko primary maana yake kuna  mahali umekwama  na unahitaji maandalizi maana shule ni sehemu ya maandalizi. Kwa hiyo  hapo usitafute muujiza bali fanya maandalizi
Kuna mtu mmoja alinisikia nilikufundisha  na akaweka kwenye matendo  mara akaanza kuota yuko primary nikaomba na akasema akaota yuko secondary na akaona tena yuko chuo kikuu   na basi nikasema  na yule mtu endelea kuomba hadi uone graduation yako .
Tufanye zoezi hapa.  Wangapi hapa wanaota wanakula chukula kwenye  ndoto? Na hizi ndoto sio nzuri kutegemea na umeota nini. Mfano ukiota ndoto unakula na mzazi wako na unampa Chakula na anasema nimeshiba maana yake ni _Kwa siku nyingi nitamshibisha, Nami nitamwonyesha wokovu wangu.
ZAB. 91:16_
Ina maana yuko tayari kuondoka (kufa) sasa kama unakula chakula kwa jinsi ya kawaida  na watu waliokufa ni chakula cha miungu. Wana wa israel walitengeneza ndama na wakala na kunywa (sakrement)
Ukila namna hiyo unakula na kushirikiana na mapepo.  Na kuna agano unaingia hata kama hujazaliwa miungu huwa inaingia agano ndio maana Mungu aliwafuatilia watu ambao walizaliwa kwa uzao wa Ibrahim.  Yesu alimfuata Zakayo kwa sababu ya agano maana Biblia inasema nae ni mwana wa Ibrahimu.
Kuna maagano yapo kwenye ulimwengu wa Roho Mungu anataka kukuweka sawa upate kufuatilia na kuvuka
Maombi kama kuna watu wamekula chakula kwenye ndoto haijalishi ni kizuri kibaya Ngoja  tupime na neno la Bwana kwa maombi. Kama ni uwe na uhakika kitatoka tu. Baada  hapo Mwl alifanya maombi sana na nguvu za Mungu zilishuka na kuwafungua watu.
Ni siku ya kwanza ya semina na   hakikishag unampata huyu Yesu maana ni mtaji muhimu sana katika maisha yako maana bila Yesu semina hizi hazitakuwa na msaada kwako hivyo basi hujaokoka hakikisha unaokoka au uliokoka ukarudi nyuma tengeneza na Mungu. Hamna sababu ya kuendelea kukaa dhambini wakati msahama upo msalabani rudi kwa Bwana.
Baada ya hapo nenda pale juu bonyeza kile kitabu cha Hongera kwa kuokoka kisome kitakusaidia pia kuna sala ya toba mule (hatujaandika hapa ili kwenye kile kitabu kipo.
Ubarikiweee sana na YESU  mkaribishe na mwingine kwenye semina hii kwa njia redio au mtandao au kufika moja kwa moja kwenye semina (Tangamano Tanga)
==Glory to God, Glory to God==

Axact

Axact

Vestibulum bibendum felis sit amet dolor auctor molestie. In dignissim eget nibh id dapibus. Fusce et suscipit orci. Aliquam sit amet urna lorem. Duis eu imperdiet nunc, non imperdiet libero.

Post A Comment:

0 comments: