Swali: "Biblia Inasema Nini Juu Ya Kushirikiana Katika Ngono Kabla Kuoana?"
Jibu: Pamoja na matendo mengine ya uchafu, kufanya kitendo cha mapenzi
kabla kuoana kumekatazwa katika maandiko; -
Matendo
15:20;
” bali tuwaandikie kwamba wajiepushe na unajisi wa sanamu, na uasherati, na
nyama zilizosongolewa, na damu.”
Warumi 1:29;
“Wamejawa na udhalimu wa kila namna, uovu na
tamaa na ubaya; wamejawa na husuda, na uuaji, na fitina, na hadaa; watu wa nia
mbaya, wenye kusengenya,”
2Wakorintho 12:21;
“nami nitakapokuja tena, Mungu wangu asije
akanidhili kwenu, nami nikawasikitikia wengi waliokosa tangu hapo, wasiutubie
uchafu, na uasherati, na ufisadi walioufanya.”
Wagalatia 5:19;
“Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya,
uasherati, uchafu, ufisadi,”
Waefeso 5:3;
Lakini uasherati usitajwe kwenu kamwe, wala
uchafu wo wote wa kutamani, kama iwastahilivyo watakatifu;
Wakolosai 3:5;
Basi, vifisheni viungo vyenu vilivyo katika
nchi, uasherati, uchafu, tamaa mbaya, mawazo mabaya, na kutamani, ndiyo ibada
ya sanamu;
1Wathesalonike 4:3;
“Maana haya ndiyo mapenzi ya Mungu, kutakaswa
kwenu, mwepukane na uasherati;”
Yuda 1:7).
“Kama vile Sodoma na Gomora na miji iliyokuwa
kando-kando, waliofuata uasherati kwa jinsi moja na hawa, wakaenda kufuata
mambo ya mwili yasiyo ya asili, imewekwa kuwa dalili, wakiadhibiwa katika moto
wa milele. “
waebrania 13:4
“Ndoa na iheshimiwe na watu wote, na malazi
yawe safi; kwa maana waasherati na wazinzi Mungu atawahukumia adhabu.”
Utaongezea:
1Wakorintho 5:1; 6:13, 7:2; 10;8;
Biblia inasisitiza
kuepuka kitendo hicho kabla ya ndoa. hii ina maana ya kuwa ni dhambi kama ya
uzinifu kwa kuwa hujaunganishwa na unayefanya naye kitendo hicho. Mapenzi baina
ya mume na mke waliooana ndiyo mapenzi yanayokubalika mbele za Mungu.
Kushirikiana katika ngono kabla ndoa kumeenea sana kwa sababu nyingi kwanza
Mapenzi yanastarehesha. Mungu aliyaumba hivyo. Anawataka wanaume na wanawake
wafurahie kitendo cha ngono (ndani ya ndoa). Hata hivyo, lengo la msingi la
ngono si starehe bali kuzaana tukaongezeke. Hivyo tunazuiwa kufanya kitendo cha
ngono kabla ndoa ili tusijipatie watoto tusiowatarajia. Kujizuia kunaokoa
maisha, kunalinda watoto wachanga na kuleta ladha halisi ya ngono pamoja na
heshima kwa Mungu.
Jibu: Pamoja na matendo mengine ya uchafu, kufanya kitendo cha mapenzi kabla kuoana kumekatazwa katika maandiko; -
Kushirikiana katika ngono kabla ndoa kumeenea sana kwa sababu nyingi kwanza Mapenzi yanastarehesha. Mungu aliyaumba hivyo. Anawataka wanaume na wanawake wafurahie kitendo cha ngono (ndani ya ndoa). Hata hivyo, lengo la msingi la ngono si starehe bali kuzaana tukaongezeke. Hivyo tunazuiwa kufanya kitendo cha ngono kabla ndoa ili tusijipatie watoto tusiowatarajia. Kujizuia kunaokoa maisha, kunalinda watoto wachanga na kuleta ladha halisi ya ngono pamoja na heshima kwa Mungu.
Tafakari hayo kwa kina.
Nikutakie Wakati mwema ndugu yangu.
By; Counselor Nicholaus Simon.
Source:jifunzenauelimike
Nashukukuru kwa mafundisho mema
JibuFuta