Counselor Nicholaus Simon |
Kwanza tuanze kwa kujua kuwa Watoto wadogo mbele za
Mungu huwa hawana hatia yeyote, ni mpaka pale tu ufahamu utaanza kujua jema na
baya, hapo ndipo mototo mdogo ufahamu wake huanza kubadilika na Mungu naye
huanza kumuangalia kama mtu anayeweza kujisimamia.
Sababu za
kuwahubiri watoto wadogo ni hizi zifuatazo:-
1. Agizo la Mungu.
Hatufanyi kwa kujisikia au kufuata agizo la kanisa
au vinginevyo.
Kumb 6:6-7.
Hapa Msingi unawekwa kikamilifu juu ya madhabahu ya
nyumbani
Ni kawaida ya watoto kupokea chochote wakati wowote
kutoka kwa mtu anayewapenda au anayeonyesha upendo juu yao.
2. Vitabu
vya hekima vinatoa Ushauri juu ya malezi na kumlea mototo vizuri.
Mithali 22:6.
Muhimu: kulea ni kuumba.
“Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo”, kwasababu ya
malezi yako yanatoa mwongozo mkubwa kwa mototo unaye mlea.
3. Yesu anasema watoto waudumiwe na wapewe habari
njema.
Marko 16:15
Mathayo 28:19.
Mathayo 19:14
4. Huleta Baraka za Mungu.
Jambo la muhimu la kufahamu ni kwamba watoto wadogo
wanaulinzai wa malaika ambapo kwa upande mwingine watoto wadogo wapo na Mungu
karibu sana, kwahiyo kupitia ukaribu huo upo uwezekeno mkubwa wa wewe
kubarikiwa kupitia motto wako, lakini pia Mungu anapo mtazama huyo motto huwa
hamtazami kama sisis binadadmu yeye hutazama kilichopo ndani yake.
Kumb 5:29, 33
5. Huathiri kizazi kijacho / kingine.
Amosi 2:10-11
Zaburi 78:2-7
Mathayo 18:14,
21:14-16.
Zaburi 51:3
- Lazima watoto wetu wajazwe na Nguvu za Roho Mtakatifu.
Yoel 2:28
Matendo 1:8
Mzazi naomba sana katika eneo hili uwe makini sana
na watoto wako, wanasikia nini? na wanaona nini?.kwasababu kila kinachoingia
ndani yake kinaifadhiwa na kwa asilimia kubwa kinamfanya awe vile alivyo.
Ni mimi ndugu yako Counselor Nicholaus Simon.
Kiungo katika mwili wa kristo.
Kwa msaada na ushauri.
whatsap 0654-623492.
pataufahamu@gmail.com
Ubarikiwe sana Na nakuomba nisaidie kushare kwa
marafiki zako ili na wao wajifunze Neno la MUNGU.
Post A Comment:
0 comments: