Ngono iko kwenye Mabango na luninga, magazeti na
sinema. watangazaji wanaitumia kutuuzia bidhaa zao. Iko kwenye muziki tunaosikiliza na imejaa kwenye tovuti.
Ngono huathiriwa kwenye mitindo ya mavazi.
Imetumika kuharibu unyofu wa watoto na imechafua maisha mengi mno. Ngono kwa
hakika itakuwepo, Rahisi kuipata, wakati wowote na mtu yeyote, bila kumaanisha
na hakuna kuwajibika. Lakini, ngono imeenda mbali na mpango halisi uliokusudiwa
na Mungu. Hii ni kweli –amini usiamini, ngono ilibuniwa na Mungu. Aliumba
wanaume na wanawake tofauti kimaumbile makusudi wawe na uhusiano wa karibu wa
kimapenzi. Japo kuwa kusudi moja wapo la kujamiiana ni kuzaa watoto, Mungu
alinuia ngono ilete raha kwa walengwa.
Kila alichokiumba Mungu kina kusudi. Ila kina
taratibu pia. Mpango wa Mungu juu ya ngono lazima ufurahiwe ndani ya mipaka ya ndoa, upendo na
nadhiri ya maisha. Kinyume na hilo, matokeo ya
ngono huwa ugomvi, kuchanganyikiwa, na michafuko.
Nj’e ya ndoa, ngono haijengi kujidhamini, bali
inabomoa. Wale wanaoitumia kama fedha ya kununua wanavyo hitaji huishia
kufilisika kihisia na kimwili. Wapenzi wanaoamua kutongojea hadi ndoa hujiletea
mzigo wa hatia, kupoteza heshima zao, na kutoamini na katika uhusiano wao.
Ngono inayofanywa nje ya mpango wa Mungu
inamadhara ya muda mref.mfano; machungu ya mimba zisizotarajiwa, kutoa mimba,
ubakaji na aina nyingine za ngono zisizokubalika. Pia kuna orodha ya magonjwa
hatari yaenezwayo na ngono zembe kama vile VVU/UKIMWI.
Mpango wa Mungu juu ya ngono ni tofauti kabisa
tena bora sana. Wale wanaongoja hadi ndoa wanajiepusha sio tu na hatari za
ngono ya mapema, bali pia wanajiweka katika maisha ya uvumbuzi, kuridhika na utosherevu katika upendo wa ndoa. na, hilo ni jambo bora kabisa kungojea..
TAFAKARI, TWAWEZA SEMA KWA UJASIRI NI VIBAYA
KUTUMIA NGONO KUPATA YALE UNAYO HITAJI.
Ndio, kwanza kabisa, ngono si hatua ya kimkakati
kama kwenye mchezo. Ni zaidi ya hilo. Mungu aliumba ngono kwa ajili ya mke na
mme. Ni sehemu kubwa ya nadhiri yao, upendo na urafiki wa ndani.
Pili, ngono inauwezo mkubwa sana, ‘’kutumia’’
kupata unachotaka. Nje ya ndoa Inaweza ‘’kukulipukia’’ na kukusababishia
kushuka kihisia, hatia, mimba zisizohitajika, au hata magonjwa. Kwa matokeo
bora –itunze kwa makusudi iliyoumbiwa.
Ni mimi ndugu yako Counselor Nicholaus Simon.
Kiungo katika mwili wa kristo.
Kwa msaada na ushauri.
whatsap 0654-623492.
pataufahamu@gmail.com
Ubarikiwe sana Na nakuomba nisaidie kushare kwa
marafiki zako ili na wao wajifunze Neno la MUNGU.
Post A Comment:
0 comments: