Na Mchungaji Peter Mitimingi, mkurugenzi wa The Voice of Hope Ministries (VHM).

Funguo -1
Onyesha Upendo usio na MASHARTI.
i. Usionyeshe upendo wenye masharti.
ii. Usionyeshe upendo wenye ubaguzi
iii. Uonyeshe upendo hata kwa watoto wanaoonekana kuwa ni watukutu.
Funguo - 2
Panga ratiba ya kuwa na wakati wa kutosha na WATOTO
i. Dunia ya leo imejaa shughuli nyingi, usipoamua hakuna siku utapata nafasi.
ii. Kutumia muda na watoto ni matofali ya kujenga mahusiano na watoto.
iii. Jenga tabia ya kuwa na muda wa MATEMBEZI(outing) pamoja nao mara chache chache inapowezekana.

iv. Jiulize swali watoto na mwenzi wako wanaingia wapi katika kalenda yako ya kila siku?
Funguo ya - 3
Uwe mzazi mwenye malengo yanayo TEKELEZEKA.
i. Ukiahidi kumletea mtoto wako kitu Fulani, hakikisha unatekeleza ulicho ahidi.
ii. Kamwe usimuahidi mwanao kitu ambacho unajua kamwe huwezi kumtekelezea.
iii. Weka malengo kwa watoto wako na uyatekeleze.

Funguo - 4
Usione aibu kuzungumza naye MAMBO YA NDANI yatakayo msaidia.
i. Kama mtoto ni Msichana azungumze na mama, au mvulana na baba kama ikibidi.
ii. Watoto wafundishwe mambo mazuri ya kufuatwa na mambo mabaya ya kuepukwa.

Funguo - 5
Mle chakula cha jioni PAMOJA n.k
i. Jitahidi kadri iwezekanavyo mle chakula cha pamoja.
ii. Kama kunawatoto wengine unaoishi nao, hao pia wawepo mezani.
iii. Usimbague house girl na kumnyanyapaa, yeye pia awepo mezani pamoja na wengine.

Funguo - 6
Uwe na WAKATI hadithi / stori na maombi pamoja.
i. Jitahidi kupata muda wa kusoma neno na watoto.
ii. Jitahidi kupata muda wa kufanya maombi na watoto.
iii. Pata muda wa kuwaelekeza watoto mambo ya msingi.

Funguo - 7
Zungumzeni mambo ya UZOEFU pamoja. Mweleze mambo uliyoyapata uzoefu wake.
i. Washuhudie watoto wako mambo uliyopitia kama uzoefu utakao wasaidia na wao.

Funguo – 8
Kujenga Mipaka mizuri kati ya mzazi na mtoto.
i. Katika maongezi mtoto ajue anazungumza na nani na kwa namna gani.
ii. Mtoto asiwe huru kukujibu kama anavyotaka yeye.
iii. Mtoto asichukue na kutumia vitu vya wazazi bila ruhusa ya wazazi.

Funguo - 9
Jiunganishe mwenyewe kwa mtoto (Connect yourself to a child)
i. Kujiunganisha kutakupa wewe haki ya kutoa mwongozo. (Correct and Instruct (connection will give you the rights “keys” to do correction and give instruction).
ii. Heshima itakuwa matokeo ya hayo juu. (Respect (It is a results of the above)
iii. Upendo ni Matokeo ya hayo ya juu. (Love (it is a results of the above)

Funguo – 10
Uonyeshe Upendo kwa Mama yao au Baba yao
i. Watoto wanachukia wakijua kwamba humpendi mama yao au baba yao.
ii. Watoto wanatamani kuona baba na mama wanaishi maisha ya furaha na upendo.
iii. Usionyeshe ukali na kumfokea au kumpiga mama yao au baba yao mbele yao.


Kwa maoni.
whatsap 0654-623492.
pataufahamu@gmail.com

Axact

Axact

Vestibulum bibendum felis sit amet dolor auctor molestie. In dignissim eget nibh id dapibus. Fusce et suscipit orci. Aliquam sit amet urna lorem. Duis eu imperdiet nunc, non imperdiet libero.

Post A Comment:

0 comments: