BIBLIA ISEMAVYO KUHUSU UTATU NA DR
MWALUSAMBO
Utatu wa Mungu
ni moja ya mafundisho yenye utata mkubwa sana katika Biblia, ingawa ni fundisho
maarufu sana katika madhehebu mbalimbali. Neno „Utatu‟ halipatikani katika
Biblia, bali ni neno lililoumbika kifikira tu (imagination). Kutokana na
kukosekana kwa maandiko yanayozungumzia utatu wa Mungu moja kwa moja, fundisho
hili limekuwa na maswali mengi sana yasiyo na majibu. Biblia inamwelezea Mungu
kwa majina matatu, yaani Baba, Mwana au Yesu Kristo na Roho Mtakatifu; majina
haya matatu yanajulikana kama „nafsi‟ tatu katika Mungu mmoja; na hiki ndicho
chanzo cha utata wa somo hili.
Jambo kubwa la kuzingatia ni hili:
Biblia nzima ina umoja wa ajabu sana usioweza kuvunjwa na mwanadamu; yeyote
anayejaribu kufanya hivyo, kamwe hawezi kupata maana halisi ya makusudi ya
Mungu katika kitabu hiki, yaani Biblia. Ili kuipata maana halisi iliyokusudiwa
na Agano la kale, msomaji anapaswa kulinganisha na Agano jipya; kadhalika, ili
kupata maana halisi iliyofichwa katika Agano jipya, msomaji anapaswa
kulinganisha na Agano la kale. Hii ni kanuni muhimu sana kwa kila msomaji
yeyote anayetaka kuielewa Biblia na umoja wake usioweza kutenganishwa kamwe.
Kuna
mafundisho mbalimbali ndani ya makanisa ambayo yamerithiwa kutoka kwa waasisi
wa madhehebu, yaliyojengwa bila kuzingatia kanuni ya umoja wa Biblia ambayo ina
umoja wake unaokubaliana, na majibu yake yasiyopingana; iwe ni Agano la kale,
au Agano jipya. Lakini sasa mambo yamekuwa tofauti kabisa! Kuna maswali mengi
ambayo yanaonekana kuwa hayana majibu ingawa si kweli. Hii inatokana na kwamba
kanuni za Biblia zinavunjwa, na kupata majibu yanayotokana na hisia za wanadamu
tu, na wala si kutoka katika Biblia.
Swali
la kwanza linalojitokeza kuhusiana na utatu wa Mungu ni hili: “Ikiwa kuna nafsi tatu katika Mungu mmoja,
kwa nini isijulikane kuwa ni miungu watatu?”
Kwa
Maswali au Ushauri Wasiliana nasi kwa:
+255
754 041 599, +255 766 635 382
Email:
info@mwalusambo.or.tz
Post A Comment:
0 comments: