UPENDO
1. Maana ya Upendo.
2. Kwanini tujifunze
somo hili.
a.
Upendo ni kitu cha thamani sana hasa katika maisha ya mwamini.
b.
Kupungua kwa kasi kubwa ya upendo ndani ya kanisa.
c.
Tujue wajibu wetu ndani ya Upendo wa Mungu.
3. Nini cha
kufanya.
Maana ya Upendo.
Upendo
ni uhitaji mkubwa mno katika maisha ya wanadamu Tangu wanapozaliwa hadi kufa,
watu hutamani kupendwa, wanaishi kwa furaha wanapopendwa na hata wanadhoofika
na kufa wasipopendwa. Bila shaka, watu huongea sana kuhusu Upendo. Hata
hivyo, jambo la kushangaza ni kuwa sio rahisi kuelezea maana ya Upendo.
Baadhi
ya wachambuzi wamefikia kukata kauli kuwa Upendo unaweza kuonyeshwa tu
kupitia matendo.
o Kulingana na Biblia,
kuna aina nne za upendo.
Mosi, ni shauku
changamfu, ya kibinafsi kumwelekea mtu fulani; aina ya upendo ulioko kati ya
marafiki wa karibu (Yoh 11:3).
Pili, Upendo ulioko kati ya washiriki wa kifamilia
(Rum 12:10).
Tatu, Upendo wa kimapenzi ambao mtu
anaweza kuwa nao kumwelekea mtu mwingine wa jinsi tofauti (Mith 5:15-20).
Mwishowe
ni upendo ulio na maana zaidi kuliko hizo aina nyingine tatu. Huo ni upendo
mkubwa zaidi kwani huongozwa na kanuni; kanuni zinazofaa-zinazopatikana katika
neno la MUNGU.
(Zab
119:105). Upendo huo, ni kufikiri kusiko na ubinafsi wa kuwafanyia wengine
lililo sawa na jema kutokana na maoni ya MUNGU, iwe mwenye kupokea anastahili
au la! Zaidi ya yote Upendo huo hauna ubinafsi.
Tunaweza kupata ufahamu wa ndani wa neno hilo kutokana na maneno ya awali (ya Kiyunani) yaliyotafsiriwa “Upendo” katika Biblia (ya Kiswahili). Neno UPENDO linatokana na kutafsiri maneno manne (ndio aina nne za upendo) ya Kigiriki cha mwanzo/awali.
Tunaweza kupata ufahamu wa ndani wa neno hilo kutokana na maneno ya awali (ya Kiyunani) yaliyotafsiriwa “Upendo” katika Biblia (ya Kiswahili). Neno UPENDO linatokana na kutafsiri maneno manne (ndio aina nne za upendo) ya Kigiriki cha mwanzo/awali.
Maneno
hayo ni;
i. PHI·LE´O
ii. STOR·GE´
iii. E´ROS
iv. A·GA´PE
i. PHI·LE´O
ii. STOR·GE´
iii. E´ROS
iv. A·GA´PE
i. PHILEO: Kitenzi kinachomaanisha kuwa na shauku, kuthamini au kupenda (kama mtu anavyompenda rafiki wa karibu au ndugu).
ii.
STORGE:
Upendo ulio kati ya watu wa familia moja. Huu ndio upendo ambao Paulo mtume
alisema una/utakuwa haba katika siku za mwisho (2Tim 3:3).
ii. EROS: Upendo wa Kimapenzi kati ya watu wa
jinsi tofauti. Upendo huu hautajwi katika Agano Jipya bali katika Agano la Kale
(Mith 5:15-20).
iv. AGAPE: Upendo unaoongozwa na kanuni na
unatia ndani mambo mengi; unahusisha fikira na una kusudi fulani na hauna
ubinafsi. Upendo huu sio hisia tunayokuwa nayo bila kufikiri. Mara nyingi
huhusisha uhusiano wa karibu wenye upendo. Agape ndilo neno linaloelezea Upendo
kwa njia nzuri zaidi. Aidha kati ya maneno hayo yote kuhusu Upendo; Agape
limetumika mara nyingi zaidi katika Agano Jipya. (Yohana 3:16).
Kwa ujumla (mara nyingi) aina zote zinastahili na zinabidi ziende pamoja. Mfano: Ni kweli upendo wa kimapenzi (eros) una sehemu yenye maana sana katika ndoa zenye mafanikio; shauku yenye kina kirefu na urafiki (philia) huongezeka kati ya wanandani na huimarishwa na upendo (agape) ambao hustawishwa kumwelekea Mungu, Kristo na Jirani Yetu (Zetu).
Kwa ujumla (mara nyingi) aina zote zinastahili na zinabidi ziende pamoja. Mfano: Ni kweli upendo wa kimapenzi (eros) una sehemu yenye maana sana katika ndoa zenye mafanikio; shauku yenye kina kirefu na urafiki (philia) huongezeka kati ya wanandani na huimarishwa na upendo (agape) ambao hustawishwa kumwelekea Mungu, Kristo na Jirani Yetu (Zetu).
Kwanini tujifunze somo hili.
(i) Upendo ni kitu cha
thamani sana hasa katika maisha ya mwamini.
Unapo
soma Biblia tunaona kuwa hata ukiwa na Imani kubwa kiasi gani,ila kama hauna
upendo si kitu kabisa, kwahiyo upendo ni kitu cha thamani sana ndani yetu.
(Galatia
5:13,1kor 8:1, 13:1-8.)
MUHIMU:
Je wajua kuwa Upendo
ndio sifa kuu zaidi ya Mungu?
Kama unaupendo utatamani mpendwa mwingine ainuke Zaidi kihuduma na si
kumrudisha chini kwa maneno yasiyo sahihi.
(ii) Kupungua kwa kasi kubwa ya upendo ndani
ya kanisa.
Tunajifunza
somo hili kwasaabu upendo ndani ya kanisa kila uitwapo leo,unapoa Usiwe mmoja
wa kulitiliza andiko,kuwa upendo wa wengi utapoa siku za mwisho.
(iii) Tujue wajibu wetu
ndani ya Upendo wa Mungu.
Fahamu
kuwa Mtu anapo toa kitu Fulani kwa moyo wa kupenda huwa anatalajia kitu Fulani
yaweza kisiwe kinacho onekana.mfano: Utajisikiaje pale ambapo umempa mtu kitu
cha thamani sana,,na baada ya siku chache unakutana naye njiani unapo mpa
salamu, akanyamaza kabisa na huku umekusikia..
Ndivyo,juu
ya Upendo wa Mungu kwetu kwa kumtoa Yesu kristo, tambua haikuwa kitu lahisi
sana ili mgharimu sana,,,kwasasa tumepata neema ya wokovu je, kuna kitu Mungu
anaitraji kutoka kwetu?
Nini cha kufanya ili tuonyeshe tunathamini
Upendo wa Mungu.
(i) Kumtumikia Mungu pasipo
kulazimishwa.
(ii) kujali muda katika
mambo ya Mungu.
(iii) Kuzitendea kazi
huduma tulizo nazo.
‘MUNGU
AKUBARIKI MTU WA MUNGU, JITAHIDI KUTENDEA KAZI ULIYO JIFUNZA”
Ni mimi ndugu yako Counselor
Nicholaus Simon.
Kiungo katika mwili wa kristo.
Kwa msaada na ushauri.
whatsap 0654-623492.
pataufahamu@gmail.com
Ubarikiwe sana Na nakuomba
nisaidie kushare kwa marafiki zako ili na wao wajifunze Neno la MUNGU.
Post A Comment:
0 comments: